REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TIZAMA PICHA YA JUMBA JIPYA LA RAPA T.I

1:25:00 PM Add Comment


RAPA T.I representing ATL, amenunua jumba jipya kubwa la kifahari, TTM tumezinyaka.

Kwa mujibu wa info tulizonyaka usiku huu ni klwamba Rapa huyo amenunua Jumba hilo ambalo lipo karibu kabisa na Studio yake ya Muziki. Cheki Picha Hizo…






















MISS ILALA 2013 DORIS MOLLEL AKABIDHI VITABU 50 SHULE YA MSINGI PUGU DAR

10:03:00 AM Add Comment







PICHA: CHEKI MASTAA KADHAA WALIVYONG'AA KATIKA TUZO ZA MTV MOVIE AWARDS-2014

9:06:00 AM Add Comment











WAKAZI NA MCHAKATO WA KUFUNGUA STUDIO YAKE

8:57:00 AM Add Comment





RAPPER WAKAZI ANA MPANGO WA KUMILIKI STUDIO YAKE BINAFSI ITAKAYOMSAIDIA KUREKODI NYIMBO ZAKE KWA MUDA ANAOTAKA KUFANYA HIVYO BILA KUSUBIRISHWA.

TTM imezinyaka kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa anataka kufanya albam zake hivyo anataka kuivuka changamoto inayotokana na kufanya kazi katika studio mbalimbali za watayarishaji wenye ratiba zao binafsi.

“Moja kati ya vitu muhimu sana ni hiyo kwamba kuhakikisha kwamba ninatoa albam. Na mimi ninavyoona kwenye process ya kurekodi albam unakuwa unazunguka katika maproducer mbalimbali kwa nia ya kuweka vitu sawa. Halafu ukusanyaji wa kazi zako inaweza kuwa headache.” Amesema Wakazi.

Changamoto ya kuibiana idea na kazi ni sababu nyingine inayomsukuma Wakazi kuwa na studio yake.

“Na vilevile siku hizi kama unaona sijui mtu kaibiwa idea mara nini…kwa sababu kazi tunaziacha kwa watu mbalimbali, hujui nani atakuja kusikia nani anafanya nini. So, cha muhimu nikawa nasema nikiwa na studio mimi mwenyewe namaanisha kwamba ntakuwa nacontrol kitu gani cha kufanya saa ngapi na lini nahikikisha kazi zote ziko tayari na itakuwa rahisi mimi kuzikusanya kazi zote na kuziweka katika CD moja kuhakikisha mashabiki wangu albam wanazipata katika siku ambayo nikisema inatoka.” Ameeleza.

Amesisitiza kuwa anahitaji studio yake iwe imekamilika mwaka huu na kwamba sapoti ya mashabiki wake kununua kazi zake ndiyo itakayosaidia kuhakikisha anakamilisha studio hiyo kwa muda.

PICHA: HIVI NDIVYO KITU KINACHOSADIKIWA KUWA BOMU, KILIVYOZUA TAFRANI ARUSHA HAPO JANA

6:24:00 AM Add Comment

 USIKU WA APRIL 13 2014 KWENYE BAA IITWAYO ‘ARUSHA NIGHT PARK’ ILIYOPO MIANZINI ARUSHA AMBAYO SIKU ZOTE NI MIONGONI MWA SEHEMU ZINAZOKUA NA MKUSANYIKO WA WATU WENGI KUANZIA JIONI, LIMERUSHWA BOMU WAKATI WATU MBALIMBALI WAKITAZAMA MPIRA.

Kwa Mujibu wa Taarifa zaAwali kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.

Pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.



TAARIFA YA MAZISHI YA MAREHEMU MUHDIN GURUMO

2:23:00 AM Add Comment

TAARIFA ILIYOTOLEWA ASUBUHI YA LEO NA MTOTO WA KWANZA WA MAREHEMU MZEE GURUMO, ABDALLAH GURUMO AMESEMA KUWA, LEO SAA MAJIRA YA 10 JIONI KUTAKUWA NA KISOMO NYUMBANI KWA MAREHEMU ENEO LA TABATA KISUKULU AMBAPO WATANZANIA WOTE WANAKARIBISHWA.

Baada ya kisomo saa 3 ya asubuhi kesho April 15 mwili wa Marehemu utaletwa nyumbani kwa ajili ya swala kisha saa 4 asubuhi safari ya kuelekea kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani itaanza kwa ajili ya maziko ya Mzee Gurumo.

Marehemu Muhidin Maalim  Gurumo ni Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma alifariki Dunia Jana  jijini Dar katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Hivi karibuni Marehemu Muhidini Gurumo alitangaza kustaafu muziki baada ya afya ya kutetereka na kuamua kupumzika hadi mauti yalipomfika.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi Amen.


KUFURU: WAGENI WAALIKWA KATIKA NDOA YA BINTI WA RAIS GOODLUCK JONATHAN WA NIGERIA, WAPEWA ZAWADI YA I PHONE 5 YA DHAHABU

2:12:00 AM Add Comment


 JIJINI ABUJA, Nigeria, Habari kubwa ilikuwa Ni Ndoa ya Mtoto wa rais wa Nchi Hiyo, GOODLUCK JONATHAN, anayefahamika kwa jina la FAITH JONATHAN aliyeolewa na GODSWILL.

Wageni waliohudhuria hapo, walipata Zawadi zaI PHONE 5 zeny muonekano wa Dhahabu, na ikiwa imeandikwa majina Yao.
Lakini amini usiamini, Moja kati ya wageni waliofaidika na zawadi hizo, ni pamoja na rais Mstaafu wa Nchi hiyo, OLUSEGUN OBASANJO.
Check Picha hizi














MNADA BANNER