REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

USWAZI-TAKE-AWAY: HATA AKINA MRISHO NGASSA WAMETOKEA HUKU-WATOTO WA BUGARIKA (BUGAZIL)

6:32:00 AM Add Comment
Licha ya Ugumu wa Mazingira Yetu hasa Sie Watoto wa Uswahilini, lakini kubali, ukatae, hata akina MRISHO NGASSA, wametopkea Huku, hii Ndiyo Burudani Yetu
Tunauwezo Mzuri wa kukabiliana na Adui zetu wanathubutu kunyemelea Magoli Yetu, ingawa hatuna Nyavu

VIWANJA vyetu havina Nyasi, lakini Vumbi na Michanga, ni Nyasi tosha, ilimradi tu, tunapata Burudani, kipaji kinaonekana, uzoefu unaongezeka, na Siku Inaenda

Hatuna Uwezo wa kununua Viatu. Na hata Hivyo, Raha ya "Kabumbu" letu, ni kulisukuma bila Viatu wala Socks

Kuna baadhi ya Sheria za Soka huwa hazifuatwi katika Soka Letu sisi watoto wa USWAZZ, lakini baadhi kama PENALTY, CORNER KICKS, FOULS, na HAND TO BALL, tunaziona saaana, maana tunahitaji Ushindi

Huwa hatubagui watizamaji ama mashabiki. Mara Nyingi hutupa Motisha japo ni wachache




Mashabiki wa Jinsia ya Kike, huwa ni ADIMU sna katika Mechi zetu, na Endapo wakitokea kuhudhuria, basi kila mtu hutumia mbinu zake, na ustadi wake, ili mradi Dada huyo atuone, na kujenga sifa, na ukaribu zaidi

Jezi Zetu mara Nyingi huwa ni Arsenal, ama Machester United na Timu Nyinginezo za Ligi ya Uingereza. Tukiona hivi, basi tunaamini ipo siku nasi tutacheza Ligi kubwa kama hao Wengine

Tunajua Mwanza kuna Mawe, Lakini hata siku moja hayatuzuii kusakata Soka letu, ingawa ni hatari hasa kujikwaa, ama unapoanguka katika Jiwe Hilo

Tunatamani Serikali za Mitaa zitutengenezee Viwanja Vizuri vya kucheza Soka huku Uswaz Kwetu, lakini ni Ndoto kwa kweli

Sio Mawe Tu, Viwanja Vyetu vinakabiliwa na Miti hatarishi iliyokauka, Chupa zinazoweza kudhuru miguu yetu maana hatuchezi na Viatu, pamoja na Mazingira Salama Kiafya

ISHU YA VIDEO YA JAY Z AKIMSALITI BEYONCE IKO HIVI……

4:56:00 AM Add Comment

DEAR FACE BOOK USERS, Tafadhari kuna jambo la msingi sana ambalo mnatakiwa kuzingatia, baada ya kuwepo kwa Kitu kinachodaiwa kuwa ni Video ya Jay Z akikunjuka na “Kishtobe” kingine tofauti na “wife” wake BEYONCE, sasa Iko Hivi…

Info Kamili imeshushwa na Kitengo Chimbua Chimbua kuwa, Kunako Mtandao wa FACEBOOK, kuna jombaa mmoja ambaye alifungua account FAKE, na Kupost Link ambayo inazungumzia, Kuvuja kwa Video ya JAY Z akimsaliti Mke wake BEYONCE, na Video hiyo ilikamatwa na SOLANGE, ambaye ni Mdogo wake BEYONCE.

Lakini ukweli ni Kwamba, Ishu hiyo sio ya Ukweli, na Utawala wa Facebook imetoa Taarifa kwa Watumiaji wote kuepukana na Link hiyo, kwani ni moja kati ya Vitu ambavyo vinalenga Kupotosha Umma, hasa wale watumiaji wa Mtandao huu maarufu, pamoja na Mashabiki wa Jay Z na Beyonce.

Aidha Utawala huo umongeza kuwa, endapo utaclick tayari kwa Kuingia katika Link Hiyo, basi hautakutana na Video hiyo ambayo imetajwa na Mwizi huyo wa Mtandao, bali utakutana na mtandao mwingine ambao utakuomba kukubali baadhi ya Masharti ikiwemo kushare Link hiyo kwa marafiki zako, jambo ambalo ni hatua ya kukaribisha wizi wa Mitandaoni, pamoja na Uharifu mwingine hasa wa kimtandao.

Aidha kama utafuatilia kwa Ukaribu, Picha ambayo imetumika kupamba kichwa cha habari ambacho kinasema VIDEO YA KUSHTUA: KANDA YA VIDEO YA JAY Z AKIMSALITI BEYONCE, IMEKAMATWA NA SOLANGE, ni Picha ambayo JAY Z anaonekana akiwa amekaa na akina dada wawili waliokuwa kwenye Utupu, yaani kama walivyozaliwa.

Katika Kuhitimisha, Utawala wa Facebook umesema kuwa, Video ambayo inatumiwa na Waharifu hao, ni ile ambayo ilifanyika mwaka 1997, katika Interview moja hivi, huku kweli akionekana kuwa na akina dada hao wawili, lakini ilikuwa ni kabla hajamuoa BEYONCE..

So WATCH OUT GUYS……

LICHA YA KUCHIKA MARA KIBAO, JENIFFER LOPEZ BADO ANAAMINI KATIKA NDOA.

4:51:00 AM Add Comment

LICHA ya kuachika Mara 3 katika Ndoa, pamoja na Mara kadhaa katika mahusiano ya kawaida ya Kimapenzi, ladies and Gentlemen, In case hukufahamu, J-LO bado anaamini katika Ndoa mazee.

Akimiminika kunako Interview na Kituo cha Redio cha HOT 97 Nchini Marekani, J-LO mwenye Miaka 44, ambaye hivi sasa amepigana Chini na “Ki-Serenget Boy” chake CASPER SMART, mwenye Umri wa Miaka 27, amesema kuwa, bado hajakata tamaa katika kulisaka Penzi tamu, maana amewahi kuwa katika Ndoa, na alikuwa akitamani kuwa katika Ndoa Imara.

Bibi huyo ambaye alifanya poa sana na Dude la “LOVE DON’T COST A THING”, amesema kuwa ingawa sio kazi rahisi kuwa katika Ndoa na kuhimili mabo zake, lakini anaiamini sana, anaamini katika kujizatiti ndani ya Ndoa, pamoja na kujikita zaidi kwa mtu ambaye unaamini mtaspend maisha yenu yote ndani ya Ndoa.

Pia J-LO ambaye ni mama wa watoto wawili Mapacha, MAX na EMME wenye Miaka 6 Hivi sasa aliozaa na Ex-husband MARC ANTHONY, amesema kuwa, licha ya kwamba amekuwa “USED” sana na watu kadhaa ambao amekutana nao, lakini anaamini yupo Mtu ambaye atampata, na kuishi naye maisha yake yooote katika Ndoa ambayo itakuwa More than Serious.

Aidha, HIT MAKER huyo wa “WAITING FOR TONIGHT” alikanusha kuwa na mahusiano ya Kimahaba na MAKSIM ambaye ni Dancer wake wa karibu, huku akisisitiza kuwa ni Marafiki wa kawaida, pamoja na Kazi…basi

UKO TAYARI "NYOKA" HUYU AKUFANYIE UPASUAJI KATIKA KOO LAKO?..HII HAPA

4:38:00 AM Add Comment

Swali ambalo nitaanza kwa kuuliza, ni Je, ulishawahi kutamani ama kuwaza, Nyoka aingie katika Koo lako kwa ajili ya Matibabu Fulani?...
SASA mseto imekutana na “NYOKA-ROBOTI”, kifaa ambacho kitafanya upasuaji katika Koo lako na Maeneo Tofauti ambayo ni ya Ndani ya Mwili.

Kifaa hicho kilichopewa jina la “FLEX SYSTEM” ama “SNAKE-ROBBOT” kimebuniwa na kutengenezwa na Professor wa masuala ya Robbotics, HOWIE CHOSET, kutoka katika Chuo cha CARNEGIE MELLON, kilichoko PENNSYLVANIA

Aidha Kifaa hicho kilifanyiwa Maboresho zaidi na Kampuni ya Uingereza, inayofahamikla kwa jina la MEDROBITICS CORP, na mpaka hivi sasa, kimeshafanikiwa kutibu wagonjwa wawili katika Hospitali ya Chuo cha DINANT GODINE huko Nchini Marekani

MNADA BANNER