REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NYOTA NDOGO. " KUSERMA KWELI, MIMI HUWA NINALALA NA NGUO...NINAOGOPA SANA"

2:20:00 AM Add Comment

Na INSTA COP.
WatuWaMungu Binafsi yangu siwezi kuruhus Eti Mke Wangu alale na mie kitanda kimoja , halafu awe amevaa nguo, hata kama ni nidhamu, aibu na heshima kiasi Gani. Lazima tu uzishushe

Lakini kwa Msanii kutoka Nchini Kenya, ni Tofauti, yeye kadai kuwa, Huvaa Nguo akilala na hata akiingia Toilet a.k.a Chooni, basi lazima achunguzi kwa Umakini zaidi, maana anweza kutana na ambalo halikutaniki

Aliandika Hivi
"Hebu niwaulize.maisha ya sasa unayaonaje hasa kwenye ndoa ama hata mpenzi wako na mitandao hii? Je upo huru na mume wako? Unaweza kutembea nyumba nzima bila nguo mukiwa nyie wawili? Nimeona mitandao yakijamii watu wakikosana unapata mume anatoa picha za mke wake kwa mitandao siri nje yani sikuizi mkikosana utu pia hakuna yote mliokua mukiyafanya pamoja yanakua nje.MUNGU ailinde ndoa yangu but sitawadanganya mimi ulala na nguo.nikienda chooni nachungulia kila sehemu kabla kukalia hio choo nimezidi ama? Je unakua muoga kama Mimi? Naogopa bure?"

MAMBO YA UTALII !!!: WASANII WA ARUSHA WAKUTANA NA MKUU WA MKOA (PICHA)

1:58:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
WASANII Wa Muziki wa aina tofauti kutoka Jijini Arusha, wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mheshimiwa Mrisho Gambo kuzungumza masuala yao ya Muziki na kuhamasisha Utalii.

Kupitia account ya Instagram ya Mkuu wa Mkoa Huyo, Mhe. Gambo alifafanua kuwa kwa alikutana na Wasanii hao akiwemo DOMO KAYA, JCB na wengine kuzungumzia namna ambavyo wanaweza kuhusisha Muziki wao wanaoufanya na Kutangaza Utalii wa Nchi ya Tanzania hasa Mbuga za Wanyama

Tukio hilo lilifanyika Jana katika Ofisi yake huku akidai kuwa, amewaambia waandae andiko Maalum na bora ambalo litaainisha namna ambavyo watautangaza utalii wa Ndani hasa ikiwemo Mbuga mbali mbali za Wanyama

Kwa Upande wake Msanii wa HIP HOP Nchini Tanzania, Domokaya, naye alisistiza kukutana kwao na Mkuu wa Mkoa huyu, huku akiwasihi wasanii pia kujikita katika Sekta ya Utalii ili kuangalia namna ambavyo unaweza kutangazika katika mataifa mengine hasa kupitia Muziki wao








BAADA YA KUKAMULIWA "NDIMU" KUHUSU KUCHEZA NA MWANAUME ALIYEBADILI JINSIA NA KUWA MWANAMKE, HATIMAYE RAPPER DESIIGNER ATOA UFAFANUZI (VIDEOS)

12:59:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
WAUNGWANA Bwana, waliamua kumuanzishia kwa Mara Nyingine Rapper Desiigner baada ya siku kadhaa kumtuhumu kuwa jamaa ni mkali wa Ngoma moja tu, na kwisha Habari yake.

Lakini Hivi majuzi tena, Desiigner aliingia katika Kashfa Nzito kwa kubainika kuwa alicheza na Dume lililojibadilisha Jinsia na kuwa mwanamke, linalojulikana kama SIDNEY STAR, walipokuwa kunako moja kati ya viwanja vya bata

Sasa, baada ya Video kufika mikononi mwa watia Ndimu, walianza kumshambulia Vilivyo bwana Desiigner huku wakidai kuwa safari yake inaelekea mwisho , wengine wakisema kuwa huenda alillitindua Usiku wake, huku wengine wakisema sasa wasanii wanaofulia wanaanza kufukuzia wanaume waliobadili jinsia na kuwa wanawake na mwisho wa siku wanaaibika kama ilivyokuwa kwa Bobby Valentino

Ili kuliweka sawa jambo hilo, Desiigner aliamua kujirecord kunako Video Clip na kudai kuwa, binafsi yeye hakuwa anafahamu kama Yule ni mwanaume aliyebadili Jinsia na kuwa mwanamke, bali alimfuata tu kama Shabiki na kucheza naye, ukizingatia yeye ni mtu maarufu, hivyo watu wa aina mbali mbali ambao humfuata, hawezi kuwachunguza histroia zao hasa wanapokuwa Club au kazini

IMEFICHULIWA !!!: SEAN KINGSTON ATHIBITISHA KUWA ALIWAHI KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA SERENA WILLIAMS KIPINDI CHA NYUMA< NA NDIYE MTU MAARUFU KUTOKA NAYE

12:41:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SEAN KINGSTON kaamua kuanika kile ambacho watu wengi tulikuwa hatukifahamu katika Maisha yake ya Umaarufu na kadharika.

Hitmaker huyu wa "Beautiful Girls" , amedai kuwa katika maisha yake ya kutinduana , ameshawahi kupita na Bibie SERENA WILLIAMS ambaye ni Mcheza Tenis hatari sana kwa upande wa wanawake hapa ulimwenguni.

Akizungumza kwa Ujasiri kabisa, Sean Kingston ambaye Hivi sasa yupo katika Mahusiano ya kimahaba na Mwanamitindo Angela, alidai kuwa, alipata angalau nafasi ya kufurahia naye, japo Serena alikuwa ni Mtu wa gharama sana na alikuwa akinunua vitu vya kampuni yenye gharama

Kingston anaongeza kuwa, hakuona tatizo kutumia Mijihela mingi sana zaidi ya USD Milioni 300 kwa Serena hasa kunako Maduka ya NIKE na kadhalika, maana alikuwa bado ni Mdogo kipindi hicho na alikuwa akispend tu bila mpangilio.

Tunamnukuu
"Alikuwa akipendelea Kuvaa vitu vya gharama, na alikuwa akivaa Mavzi ya Kampuni ya NIKE. na unajua ni nini,nilipokuwa nikienda naye sehemu yoyote, halafu nikatoa kadi yangu ya benki, alikuwa akinipiga mkono na kuniambia niirudishe Mfukoni kadi hiyo, ila nilikuwa nikimuambia, Ooh, Miss Serena Williams, endelea na kile unachotaka kufanya....."

Lakini ukiachilia mbali suala Hilo, Sean Kingston bado kamsifia Serena hasa kipindi ambacho alikuwa akimjali sana wakati yupo katika matatizo, ikiwemo kulazwa Hospitali na Serena alikuwa akija kwa Takriban siku saba mfululizo kumjulia hali.

Pia akaongeza kuwa, Namkubali sana kwa yale ambayo alimfanyia, na bado ni rafiki yake na anajivunia kuwa Serena anafurahia hivi sasa maisha ya Ndoa na familia Nzima kiujumla

YAMEFIKIA HAPA !!!!: KANYE WEST KUANZISHA MTANDAO WAKE WA KU-STREAM ILI KUCHUANA NA TIDAL YA JAY Z

12:13:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Hatimaye inaanza kudhihirika Rasmi kuwa ukaribu ama mahusiano ya Wawili ambao walifanya vziuri kabisa kunako soko la Muziki wa Hip Hop, yanaelekea kupotea rasmi na kuingia katika uhasimu wa hali ya Juu.

Hapa namzungumzia Rapper Jay Z pamoja na Kanye West, ambao waliingia katika uhasama wa hali ya juu huku kila mtu akimtuhumu mwenzake kwa kuanzisha noma hilo

Sasa, Taarifa ambayo tuko nayo ni kwamba, Kanye West ameamua kufungua Mtandao wake wa huduma za Kustream Muziki mbali mbali kwa dhumuni la kupambana na TIDAL: ya JAY Z

Licha ya kuwepo kwa taarifa rasmi kuwa, Jay Z na Kanye West watahusika katika mazungumzo ya moja kwa moja yaani face to face ili kuondoa tofauti zao ambazo zingeathiri mtandao wa TIDAL ambapo Jay Z alimjumuisha Kanye West pamoja na Nyimbo zake kwa ajili ya huduma za kustream, lakini Mambo yamekuwa tofauti baada ya Kanye West kutangaza ujio wa Huduma yake mpya mabyo inaashiria kuchuana vikali na Jay Z

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, Kanye West alitangaza Rasmi kuanzisha huduma hiyo ambayo itaitwa YEEZY SOUND

YEEZY SOUND itajihusisha na masuala ya Recording, Kupromote Muziki, Videos na Audio, lakini pia huduma ya Kustream, na mengineyo

MNADA BANNER