REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BUNGENI: NAY WA MITEGO, SHILOLE WAMEZUNGUMZIWA TENA BUNGENI

8:43:00 AM Add Comment

DODOMA, Tanzania
Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo, imetolea ufafanuzi hatua ambazo zinaendelea katika Tukio la Kutokea kwa Vitendo visivyo na Maadili katika Kumbi na Maonesho mbali mbali ya Starehe.


Ufafanuzi huo umetolewa Mapema Leo Hii Bungeni, katika Kikao cha 25, cha Mkutano wa 15 wa Bunge la 10 La Bajeti Linaloendelea Hivi sasa, baada ya Mheshimiwa Catherine  Magige kuhitaji Ufafanuzi kutoka Wizara Husika, ambapo Majibu yalitolewa na Naibu Waziri, 
Mheshimiwa Juma Nkamia

Katika kutoa Ufafanuzi zaidi, Mheshimiwa Nkamia ametoa Mfano kuwa, moja kati ya watu ambao wamepewa Onyo ni pamoja na wasanii kama Vile NAY WA MITEGO, SNURA na SHILOLE, huku Mashindano ya MISS UTALII yakifungiwa

KUDADADEKI..SASA NI VITA KATI YA OXS OKELLEKY NA J FLANI

7:05:00 AM Add Comment

Baada ya Kutembelea Statistics Katika Account yangu ya Hulkshare, Nimekuja kubaini kuwa, Rapper Oxs Kutoka Mwanza ambaye hivi sasa anashikilia Usukani kwa Kusikilizwa zaidi na Wimbo wake wa HOPE, anafukuzana na Rapper Kutoka Nchini Canada, J-FLANI ambaye hivi sasa ana Siku Mbili tu, tangia ameachia Track yake ya FREEDOM aliyomshirikisha Natty E na Honeya Kutoka Mwanza..

Check Statistics Hizi


Pia unaweza kulinganisha Track zao Kwa Kusikiliza hapa




VIWANGO VYA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI, NA BEI YA MAGARI (USED) YALIYOPO SOKONI

6:24:00 AM Add Comment

1. VIWANGO VYA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI NCHINI TANZANIA WIKI HII, KAMA ILIVYOTOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA (B.O.T)

FEDHA                      INANUNULIWA KWA SHILINGI                INAUZWA KWA SHILINGI
SHILINGI YA KENYA               18.63                                                            18.77
DOLA YA MAREKANI             1634.78                                                        1651.13
PAUNDI YA UINGEREZA         2752.80                                                        2780.83
EURO YA ULAYA                     2229.51                                                        2251.97
YEN YA JAPANI                       16.04                                                             16.20
RANDI YA A. KUSINI                158.05                                                           159.47

( Bank Of Tanzania)


2. BEI ZA MAGARI YALIYOKO SOKONI LEO HII NI KAMA IFUATAVYO

GARI AINA YA…                                                       LINAUZWA  KWA
BMW 8 Series                                                            DOLA 12,800
Mercedes-Benz V-Class                                        DOLA 2,416
Nissan Caravan Van                                             DOLA 3,426
Toyota RAV4                                                            DOLA 20,708
Toyota Vitz                                                               DOLA 900
Toyota Land Cruiser Prado                                   DOLA 34,500

(http://www.tradecarview.com)





KAMPUNI YA APPLE KUANZISHA I PHONE AMBAYO INA UWEZO WA KUKUPIMA BLOOD PRESSURE

6:12:00 AM Add Comment

KAMPUNI ya Apple inatarajia Kuingiza Sokoni simu ya I PHONE itakayokuwa na Uwezo wa Kupima Presha ya Damu/ Blood Pressure kwa Mtumiaji.

Wakifafanua kuhusu hilo katika Mkutano wa WORLD WIDE DEVELOPERS, uliofanyika SAN FRANSISCO Marekani, CEO wa Apple, TIM COOK amesema kuwa, Simu hiyo ama Kifaa hicho kilichopewa jina la iOS8, kitafanya kazi ya Kubaini Blood Presha na Ikibidi Kuonesha takwimu papo hapo ili kufahamu Kinachoendelea.

Naye Naye Makamu wa rais wa SOFTWARE ENGINEERING katika Kampuni ya Apple, CRAIG FEDERIGHI, ameongeza kuwa, Simu hiyo itatoa Taarifa automatically kwa Daktari wa familia, endapo hali ya Mzunguko wa damu itafikia katika hatua Mbaya.


Tofauti na hilo, kifaa hicho kitatoa taarifa kwa Wazazi, Endapo watoto wao watakuwa wakuidownload Miziki Mbali mbali na hata Video Games

HIVI NDIVYO MTOTO ALIVYOBURUZWA KATIKA GAUNI LA BIBI HARUSI

5:17:00 AM Add Comment

UNAWEZA KUJIULIZA kuhusu Hili na hata kutafakari kwanini watu wasiwe na maoni Mengi tena ya Kukosoa katika hili.

Mwanandoa aliyefunga Ndoa yake hivi karibuni, SHONA CARTER BROOKS (SHONA KATA BRUKS),amejikuta akipokea Mzigo wa maoni ya Kumkosoa Vikali hasa Mtandaoni, baada ya Kuweka picha zake siku ya Ndoa, huku akiwa anamburuza mtoto wake wa Mwezi mmoja , Nyuma ya Shera yake.

SHONA alifanya tukio hilo akiwa Kanisani, huku akimuweka Mtoto huyo katika Shera ambayo huwa inaburuzwa Nyuma, na Mtoto huyo kuonekana akiwa anaburuzwa hapo.


Kwa Mujibu wa maelezo yake, Shona anasema kuwa, watu hawatakiwi kuwa na Hofu, maana mtoto huyo, AUBREY, alikuwa akilindwa na damu ya Yesu. Ndoa hiyo ilifungwa jijini New York, ambapo Shona alikuwa akiolewa na Mumewe JONATHAN BROOKS, katika kanisa la Kisabato , lililopo RIPERY

JUMANNE MSETO: LUPITA NYONG'O NA SHAVU KATIKA FILAMU YA STAR WARS

5:13:00 AM Add Comment

NEW YORK, Marekani
BARAKA zinaweza kuwa Ni za Pekee kwa Muigizaji wa Filamu Kimataifa, LUPITA NYONG’O baada ya Kupata Dili linguine la kuigiza katika filamu Mpya ya STAR WARS

Lupita ambaye ni raia wa Nchi ya Kenya na Mshindi wa Tuzo kadhaa ikiwemo ya OSCAR, anatarajia Kuungana na waigizaji tofauti JOHN BOYEGA, OSCAR ISAAC, ADAM DRIVER katika Filamu Hiyo itakayoongozwa na J.J Abrams.


Kupitia account yake ya Instagram, Lupita alionesha Furaha ya aina yake baada ya kupost Picha ya STAR WARS, huku akiongeza maneno kuwa anatarajia kufika Mbali baada ya kupata Deal hilo.

MNADA BANNER