REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MFUNGWA MREMBO KULIKO WOTE NCHINI KENYA, HATIMAYE KAEMA UKWELI KUHUSU KUMUUA BOYFRIEND WAKE KWA KISU

2:31:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
Kama utakuwa unakumbuka Vizuri, Kipind cha Nyuma, Mwaka 2016, tulikupatia Taarifa kuhusu Binti Mrembo anayetumikia kifungo Cha Maisha Nchini Kenya kwa kosa la Kumuua Boyfriend wake kwa kumchoma kisu mara kdhaa mwilini.

Binti huyu Mrembo ambaye alishinda taji la MISS LANG'ATA PRISONER 2016 nchini Huo, anaitwa RUTH KAMANDE na alimuua boyfriend Wake FARID MOHAMME mwaka 2015 huko nyumbani Kwao BURU BURU

Baada ya kutokusikia lolote kutoka kwake, hatimaye Binti huyu kaweka wazi kuwa ni kweli alimchoma kisu boyfriend wake huyo mpaka kufa, ikiwa ni baada ya kubaini kuwa boyfriend wake huyo alikuwa ni muathirika wa HIV

Akiwa mahakamani hapo jana, Ruth anadai kuwa, alikuta kipimo cha Ukimwi chumbani kwao kikionesha kuwa jamaa yuko HIV POSITIVE ,

Tunamnukuu  
"Farid aliniambia kuwa angeniua mie na yeye kujiua kuliko kujitangaza kuwa ni muathirika wa HIV. Nilimchoma mara kadhaa kwa kutumia kisu cha kukatia vyakula, ambacho kiliangukia kifuani mwangu kutoka mikononi mwake, ikiwa ni baada ya kumzidi nguvu alipotaka kuniua."


MARIAH CAREY: "SIWEZI KUIMBA BILA MKWANJA"

2:11:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi   
Watu wa Mungu hata kama kafulia kimuziki au sauti imekuwa ni ya kuzingua, ila bado hatoi huduma za Bure Bure hata kidogo

Ingawa tafsri ya haraka itakuwa ni kwamba alifanya Masihala, lakini kama hukufahamu, Mariah Carey alitamka hadharani kuwa hawezi kuimba bila malipo ya aina yoyote.

Kauli hiyo ilitokea katika Birthday party ya Bondia Mstaafu mwenye mkwanja mrefu, FLOYD MAYWEATHER JR ambapo alikuwepo pia Muigizaji Jammie Fox aliyemuomba Mariah Carey aimbe japo Kidogo kwa ajili ya kuifanya Bata hiyo iwe na utamu wake.


Kupitia Microphone hiyo hiyo, Mariah Carey akiwa pembeni pia ya Floyd Mayweather Jr alitamka kuwa hawezi kuimba bila kupewa Check ya mkwanja

NAMNUKUU   
"Nipeni Cheque kwanza ndio nitaimba"

AKON ANATAKIWA KULIPA DENI LA ENEO ALILOPANGA

1:52:00 AM Add Comment




Na RICH SAM  
Watu Wa Mungu mambo sio mazuri kwa upande wa Mkali wa Muziki wa Pop Nchini Marekani ambaye asili yake ni SENEGAL, hapa tunamzungumzia AKON

Hit Maker huyu wa DONT MATTER anatakiwa kuilipa kampuni ya GTFM Dolari za kimarekani 164,786.99, pesa ambazo anadaiwa kushindwa kuzilipa ikiwa ni baada ya kupanga katika Jengo lao kwa ajili ya matumizi ya biashara yake

Kwa Mujibu wa Vielelezo kutoka katika Kampuni hiyo, ni kwamba, Akon alienda katika Jengo la EMPIRE STATE (Empire State Building) akiomba kupangishwa Floor ya 66  kwa ajili ya Biashara yake ya masuala ya Fashion kupitia mavazi yake ya ALIAUNE MILANO.

Katika makubaliano yao, Akon alikubali kulipa USD 25,000 kwa mwezi, na alikuwa akilipa vizuri kuanzia JULY 2012 mpaka JULY 2015 ambapo inasemekana aliacha kulipa ghafla.

Kampui husika ikaongeza kuwa, AKON hakuwahi kulipa tena mpaka alipoondoka January 2016 akiwa anadaiwa deni la Takribani miezi saba.

Hata Hivyo, mahakama imebaini kuwa Akon ana makosa katika hilo na anatakiwa kulipa mkwanja anaodaiwa







MNADA BANNER