REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

VIDEO: HII HAPA VIDEO MPYA "KINANDA" KUTOKA KWA MESEN SELEKTA AKIWA NA RAYAKO (VERY HOT)

6:56:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
TANZANIA, kama Wasanii Wengi ambao huwa wanaamua kupiga "SILENT" kwa muda Mrefu hatutakiwi kuwapuuzia kwa namna moja ama nyingine

MESEN SELEKTA ni miongoni mwa Producers ambao walitamka kuwa , kabla hata ya kujihusisha na Production, alikuwa ni msanii wa kawaida kama walivyo wasanii wengine, na kadri siku zinavyokwenda, basi anadhihirisha hilo kwa kazi kali ambazo huwa anaachia

WEDNESDAY HOTTEST TRACK (W.H.T) Ni Brand New Video kutoka kwa Mesen Selekta akiwa ameshirikiana na Rayako. Mkwaju unaitwa KINANDA huku Production ikiwa ni ya kwake mwenyewe. LUCA SWAHILI VISUALS ndio waliohusika katika Video.

Itizame hapa

JIDE JAYDEE " NIMECHOKA KUBANA KITUMBO"

6:29:00 AM Add Comment

Na INSTA COP - Lady Menah 
Wale Ndugu zangu ambao huwa tunazunguka katika Social Networks hasa Instagra, naamini hili mtakuwa mnalifahamu vizuri jamani eeh, maana sie masaa 24 macho yetu yapo "kodo" kwa hawa mastaa.

Bahati mbaya sana, huwa hatu-deal na ule udaku wa kiugomvi ugomvi ama useless useless, ila huwa tunaangalia ule ambao unajithibitisha hapo hapo

Leo tumemnasa dada Yetu KOMANDO ambaye alisema kabisa kuwa hivi sasa tusimuite tena BINTI MACHOZI maana halii tena.... naomba niishushe kama ilivyo

HIKI NDICHO KILICHOMKWAMISHA NYOTA NDOGO KUACHIA TRACK ALIYOAHIDI

5:31:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu Sikutaka kuamini lakini hali halisi kumbe ndo iko hivyo aisee, kuna vitu vinaweza kukufanya ukashindwa kukamilisha ahadi zako.

NYOTA NDOGO kutoka Nchini Kenya, ameshindwa kuachia Track kama ambavyo aliahidi kuiachia Katika Siku ya Maadhimisho ya Wapendanao (Valentine's Day) kutokana na kubanwa na Shughuli za Ujenzi.

Kauli hiyo ameitoa kupitia Instagram account yake kama ifuatavyo
"Nimejaribu nimeshindwa wapenzi.i know niliwaaidi nyimbo kabla valentine but imekua ngumu kujigaanya marambili.hizi nyumba tatu nimesema ikiisha naweza kuingia mzikini kabisa but kama unajua mambo ya ujenzi usipokuepo utakwenda hasara nyumba ibaki imesimama na pesa zimeisha.vile mume hayuko na mimi nianze masafa yangu niwaachie tu mafundi itakua twadanganyana.na tageti huu mwezi inshallah ziwe zimeisha hata kabla huu mwezi inshallah then tuingie mbioni.mtanisamehe but imekua ikinila kichwa sana huku nataka kutoa ngoma huku nataka"

MAMBO YA KIKI !!!- "UKITAKA WATU WAKUJUE, KAVUE NGUO KARIAKOO" -SHILOLE

1:38:00 AM Add Comment

Na Baba Juti 
#WaungwanaWenzangu kama tukiulizana Neno "Kiki" limechukua trend kubwa Mwaka Gani, nadhani wengi tunafahamu ni kuanzia mwaka 2016 hivi mwishoni mpaka safari hii, ambapo pia ni kama linapoteza "utamu" hivi

Lakini pia kumekuwa na wengi hasa wasanii ambao waligundua kuwa Neno "Kiki" linweza kuwaletea Faida na hasara katika maisha yao na kazi zao kiujumla. Kiuhalisia, wapo waliopata faida kadhaa kutokana na Kik, lakini kuna wale waliaoambulia za Uso kutokana na Kiki

Leo, Shilole anawataka mjue na kufahamu kabisa, ikibidi muelewe kiundani zaidi kuwa Uhalisia wa Maisha Yake, Ndiyo Kiki yake, maana kuna wengine wameshatafsiri kuwa maisha yake anayatengeneza kumbe yeye ndiye uhalisia wake

Kupitia Instagram account yake, Shilole ambaye hivi sasa anajihusisha na muziki pamoja na biashara ya msosi, amesema kuwa yeye ana zari lake la kik hapa mjini, maana Maisha yake halisia, ni ndiyo Kiki Yake

   Tunamnukuu   
"Watu wenye zari na kiki zetu mjin 😂😂😂😂 wala sihangaikagi masikin ya Mungu ukweli wa maisha yangu ndo kiki yangu #usinitumiewatunjoomwenyeweUkitakawatuwakujuekavuenguokariakooo😂🖕"

BALAA JIPYA MJINI !!! : HACKERS WAPYA WAMEKUJA NA MBINU MPYA YA KUUZA VIDEO ZAO ZA NGONO...RIHANNA NDIYE MUATHIRIKA WA KWANZA

1:04:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
#WazeeWaKazi kuna kitu ambacho hivi sasa inabidi muwe nacho makini kwa sababu mambo yameanza kuwa ndivyo sivyo na unaweza ukajikuta unaamini kile ambacho hutakiwi kukiamini

Hivi sasa kumetokea Kundi la Hackers Maalum ambao ni hatari kwa asilimia kubwa, wanaotumia Sura za Watu Maarufu, kutengeneza Video za Ngono na kuziuza kwa Watu ambao huamini kuwa wanaofanya ujinga huo ni Mastaa wenyewe

Taarifa za ki-intelijensia zinaonesha kuwa, Hackers hao ambao wanamiliki makampuni ya kuandaa video za ngono, wameanza kutumia mbinu moja inayoitwa DEEP FAKING kwa kuiba Sura za watu maarufu kwa kukopi kila kitu chao, na kuzipachika katika sura ya Mcheza Ngono mwingine

Mmoja kati ya Waathirika mpaka hivi sasa, ni RIHANNA, ambapo inasemekana kuwa Hackers hao wametumia miaka na miaka kutengeneza Sura hiyo bandia, huku wakitoa matamko mitandaoni kuwa wanavideo ya ngono ya Rihanna ili watu wajiandae kuipokea

Tayari Video hiyo inayomuonesha binti anayefanana kwa kila kitu na Rihanna, imeshaachiwa na mpaka sasa hivi Management yake hasa meneja mwenyewe yuko katika harakati nzito za kuhakikisha wanawakamata wahusika na kuondokana na tatizo hilo

Hata Hivyo , Hackers hao wamedai kuwa, bado kuna mtiririko wa Filamu kibao zinazowaonesha mastaa kibao katika Industry ya Muziki na Filamu, zinztarajiwa kuachiwa..so, kaeni chonjo na muwe makini na Hackers hao maana pia hutumia njia hiyo kuchukua Personality ya mtu pamoja na kukuibia wewe unayedanganyika

TAARIFA: MAMA MAZAZI WA NICKI MINAJ AMETOA TAMKO HILI KUHUSU MTOTO WAKE, JELAN MARAJ, AMBAYE PIA NI KAKA YAKE NICKI, KUPIGWA JELA

12:46:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
#WatuWaMungu Mama Mzazi wa Nicki Minaj amekanusha taarifa zilizokuwa zikimuhusu Mtoto wake wa Kiume JELAN MARAJ ambaye pia ni kaka yake na Nicki Minaj kuhusu tukio la kupewa kipondo heavyo huko Gerezani alikofungwa.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri, awali tulikupa taarifa kuwa kumekuwa na Video Clip ambayo anasambaa ikimuonesha mtu anayefanana na Kaka yake na Nicki Minaj, akipewa kipondo kizito na wafungwa wenzake katika Gereza alilofungwa, baada ya kukutwa na hatia ya Kumbaka Binti yake wa kambo mwenye miaka 11.
A post shared by Carol Maraj (@theofficialcarolmaraj) on
Baada ya Taarifa hizo kuzagaa kwa Wungi, CARLO MARAJ alijitokeza kupitia account yake ya Instagram na kudai kuwa taarifa hizo sio za Ukweli, maana liongea na mtoto wake na kubaini kuwa anaendelea vziuri na wala sio muhusika katika Video Clip Hiyo

HAJAKUBALI !!!: RAPPER NELLY KUFUNGUA KESI YA UDHALILISHWAJI

12:25:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi 
TAARIFA "zimepenya" kuwa Rapper Nelly ameamua kufungua mashtaka dhidi ya Bibie ambaye alimtuhumu kuwa alimbaka

Kama utakuwa unakumbuka Vizuri, Hitmaker huyo wa DILEMMA aliingia katika Tuhuma nzito za kumbaka na kumjeruhi Binti anayefahamika kwa jina la MONIQUE GREENER, tukio ambalo inadaiwa lilitokea katika Tour Basi yake

Sasa, baada ya kuingia katika Kashfa hiyo na mtuhumiwa kufuta mashtaka yake, Nelly ameamua kufungua Mashtaka dhidi ya binti huyo akimtuhumu kumuundia skendo kubwa na hata kumchafulia jina ikiwemo kumdhalilisha na kumdhihaki

Kwa mujibu wa Wanasheria wake kutoka ST LOUIS, Nelly ameathirika kwa asilimia kubwa na tuhuma hizo, kitu ambacho hata kisaikolojia kimempatia wakati mgumu sana, hasa baada ya kubainika kuwa amesingiziwa na kuaibishwa mbele ya ulimwengu unaomuamini

Ukiachilia mbali suala hilo, Nelly pia alikwazika baada ya Girlfriend wake SHANTEL JACKSON kuhusishwa katika tuhuma hizo, kuchafuliwa, na kudhalilishwa pia.

Mpaka hivi sasa, haijabainika kuwa Nelly atahitaji kiasi gani cha fedha kama malipo ama atahitaji binti huyo apewe adhabu gani

VIDEO: KENDRICK LAMAR KASHUSHA MZIGO MPYA "ALL THE STARS" YUKO NA SZA

12:10:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
Rapper KENDRICK LAMAR ameachia Brand New Video akiwa amemshirikisha Bibie SZA. Video hiyo inaitwa ALL STARS

Tenga Muda Wako Kuitizama Sasa Hivi

VIDEO: WIZ KID KAISHUSHA VIDEO MPYA "NOWO" AMEMSHIRIKISHA CDQ

12:00:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
Watu Wa Mungu , Msanii aliyefanikiwa vizuri mpaka kufanya Collaboration na wasanii wakubwa Kimataifa, WIZ KID a.k.a STAR BOY, ameshusha Brand New Video inayoitwa NOWO na amemshirikisha Msanii mwingine anayeitwa CDQ

Producer aliyehusika katika mchakato wa AUDIO, anaitwa MASTER CRAFT. Chukua muda wako kuitizama

MNADA BANNER