REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NI MCHEPUKO?: TREY SONGZ KAFUNGULIWA MASHTAKA KWA KOSA LA KUMPIGA MWANAMKE USONI...KISA CHAKE SASA !!!!

1:47:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
INAWEZEKANA ukawa ni mmoja kati ya Watu ambao mnachepuka sana, na kwa bahati kuzingatia "usiri" wa uchepukaji wako, ukawa hutaki kila mtu ajue kuwa unatabia hiyo, lakini cha ajabu ni pale ambapo wivu wako kwa mchepuko wako ndiyo unaokuja kukuumbua bila kificho

Wengi tunamfahamu vizuri TREY SONGZ ambaye husifika vyema kwa kuwa M-QUTE kwa watoto wa kike kuanzia sauti yake mpaka muonekano wake, lakini mkae mkijua kuwa MCHEPUKO wake unamfikisha Mahakamani muda wowote

Taarifa za uhakika kutoka kwa bibie huyo ambaye hajawekwa hadharani mpaka hivi sasa, ni kwamba anamshtaki Trey Songz kwa kosa la kumpiga Usoni na kumjeruhi Jumamosi ya Wiki iliyopita katika Party La Los Angels Huko Marekani kunako Usiku wa ALL STARS WEEKEND.


Madam huyo anadai kuwa, Trey Songz alimfanyia Unyambilisi huo baada ya kumuona akiongea na mwanaume mwingine siku ya tukio, ambapo mwanzo walianza kwa kuzozana kuhusu yeye kuongea na mwanaume huyo

Baada ya ubishi kukolea, Trey alimzibua binti huyo Usoni na sababu kubwa ambayo mwanamke huyo kaitaja, ni Wivu maana ni watu ambao wana uhusiano wa kimapenzi

MKATO WA ROCK CITY: PIDDE MONTANA - "BAADAE"

1:28:00 AM Add Comment
   
Na Baba Juti  
ROCK CITY imezidi kudhihirisha kuwa kuna hazina kubwa ya vipaji ambavyo vingine tayari vimeshafanikiwa kufika mahali pazuri, lakini vingine bado vimejificha

Kupitia MIKATO YA ROCK CITY, leo tunamshusha mkoja kati ya vijana ambao pia wanafanya Vizuri katika muziki wa kizazi Kipya, PIDDE MONTANAH na Video yake inayoitwa BAADAYE.

Video ilikuwa Released officailly June 7 Mwaka 2017 kupitia Mtandao wa Youtube na mpaka hii leo, ina Views TISA tu.

What Do You Say to This?

MDOGO WAKE REMY MA AWEKWA HATIANI KWA KUPIGA RISASI

1:11:00 AM Add Comment
   
Na Rich Sam   
Wanaopenda Muziki wa HIP HOP watakuwa wanamfahamu vyema Kabisa Remy ma, moja kati ya Female Rappers wanaofanya vizuri sana na hata kusifika kupitia utamu wa Flow zake ambazo huwa anazitumia pindi anapoachia zigo

Lakini kuna Taarifa mbaya hasa kwa Remy Ma mwenyewe ikiwa ni baada ya Mdogo wake wa kike mwenye miaka 27, REMEESHA kukamatwa kwa kosa la kupiga Risasi katika Gari ambalo lilikuwa limebeba wanawake Watatu ndani yake

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Jeshi la Polisi Nchini Marekani inadaiwa kuwa Tukio hilo lilifanyika Ijumaa ya juma lililopita, ambapo Rameesha ambaye ni mdogo wake na Rapper Remy Ma alifyatua Risasi katika Gari hilo huku wengi wakiwa hawajui sababu, hali iliyosababisha mtu mmoja kujeruhiwa.

Mmoja wa maafisa wa polisi anataarifu kuwa, baada ya Wanawake hao watatu waliokuwa katika gari iliyofyatuliwa Risasi kadhaa, walipanic na kuondoa gari , hali iliyosababisha mwanamke mmoja kugongwa na kujeruhiwa na Risasi

Baada ya Polisi kupata Taarifa hizo, walimkamata binti huyo anayefanana kabisa na Remy Ma siku ya Jumatatu ya Wiki hii nyumbani kwao.

Familia ilijitahidi kuweka dhamana kwa Rameesha, lakini ilishindikana kutokana na mambo mawili makubwa, MOJA ikiwa ni kuhofia kuhatarisha maisha ya Wahusika endapo angeachiwa huru, na MBILI ni kwamba, Rameesha awali alikuwa  na kesi ya Kumdhuru mtu na silaha kali, na kupiga risasi kadhaa ndani ya jiji ikiwemo kumtishia mtu kwa Bastola


MNADA BANNER