REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

AJALI KAZINI,AU?: JAMAA AMNG'ATA ASKARI POLISI NA KUMUAMBUKIZA UKIMWI

3:03:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KUNA wakati unaweza ukatamani ujute kufanya kazi fulani hata kama ilikuwa ndiyo ndoto yako, hasa kutokana na hili ambalo limetokea na linakatisha tamaa kwa asililimia kubwa

Kutoka Eneo la KERICHO Nchini Kenya, Katika Mahakama ya Kericho, mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la MUTAI, mwenye miaka 30 anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kumng'ata Askari Polisi katika Kidole Gumba na kumuambukiza VIRUSI vya UKIMWI

Kwa Mujibu wa mashtaka yalisyosomwa katika mahakama hiyo Mutai alifanya Tukio hilo alip[okuwa amekamatwa na Askari Polisi huyo mnamo February 27 Mwaka 2018 katika Eneo la kibiashara la KEBENETI majira ya Usiku

Taarifa zinaongeza kuwa Katika hali ya kujitetea kutoka katika Maumivu ya kukamatwa na Askari huyo, aliamua kuzamisha meno yake katika Dore Gumba la Polisi , hali iliyompa majeraha sanjari na kuambukizwa Virusi vya UKIMWI

Hata Hivyo, Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo, Na askari Polisi yuko anaendelea na matumizi ya Dawa za kupunguza Makali ya Virusi hilo, na Kesi imepangwa kusikilizwa Tena MARCH 15,2018



HONGERA SANA !!!: NICK CANNON KAPOKEA PONGEZI NYINGI KWA HILI

2:38:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
NICK CANNON ameanza kuonesha namna gani anamthamini mwanamke na hasa Uzuri wake kupitia Projects mbali mbali ambazo huwa anazifanya na Very Soon tutarajie Album yake Mpya

Rapper huyu ambaye pia ni Mchekeshaji ambaye ni Mzazi mwenzake na Mariah Carey huku ndoa yao ikishindwa kudumu, ameandaa album Maalum aliyoipa jina la MODEL MUSIC ambayo itasheheni nyimbo kibao za kuhamasisha wanawake wajikubali hasa kimuonekano kuanzia nje Mpaka Ndani

Awali Nick Cannon ambaye mpaka hivi sasa anausherekea Mwezi wa Wanawake, alkuwa na mpango wa kuandaa kazi ambayo itamuhamasisha Binti yake huko mbeleni hasa kuhusu muonekano wake na uzuri ambao yuko nao

Lakini ukiachilia mbali Idea hiyo ambayo inaonekana kufanikiwa, Katika Video yake ya MOTIVATION, aliona ni Bora awashirikishe wanawake ambao ni Wazee akiwemo Bibi Yake mwenye alipokuwa amefikisha Miaka 99, ili kujenga tafsiri ya kile ambacho kinaitwa Uzuri na Urembo

Wengi wamepongeza sana Idea Hiyo ya Nick Cannon ahasa kuwatumia Wanawake Wazee tupu badala ya kuweka Mademu wakali wenye Figure Kali na kadhalika

JACQUELINE WOLPER: "NILIANZA MASUALA YA FASHION KABLA HATA SIJAINGIA BONGO MOVIE"

2:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WENGI tumeanza kumfahamu Jacqueline Wolper kupitia kiwanda cha Filamu hapa Nchini Tanzania, maarufu kama Bongo Movie, lakini yeye mwenyewe anathibitisha kuwa kuna jambo lingine ambalo amekuwa akilifanya hata kabla hajaingia Katika ulimwengu wa Filamu hapa Nchini tanzania

Akizungumza weekend hii katika Ukumbi wa King Solomon alipokuwa ameenda kwa ajili ya Shughuli ya Usiku wa The Vikings, Wolper alisema kuwa haonekani sana katika Bongo Movie kutokana na shughuli zake za Ujasiliamali ambazo ndo hizo tunazoita Fashion

Wolper ambaye hivi sasa anaitwa WOLPER STYLISH, amedai kuwa alianza kuonesha dalili za kuwa mtu wa Fashion wakati yupo Shule na aliwahi kubuni vazi lake mwenye ambalo lilikuwa na Material ya Mifuko Ya Rambo

Na alipofika uraiani, akagundua kuwa watu wanapenda kile anachokifanya katika Mavazi, akaona ni Bora aendelee tu

MSIKILIZE HAPA

SIRI IMEFICHUKA !!! : KUFULIA KWA KRI HILSON, BEYONCE NA CIARA WANAHUSIKA

1:48:00 AM Add Comment

Na HEZRON MUNISI
#WatuWaMungu Siri taratibu zinaanza kufichuka hasa kuhusu kile ambacho kilimfanya Keri Hilson apotee kwenye muziki na vitu vyake kutokusonga vizuri

Kipindi cha awali kidogo tulikupa taarifa kuwa Keri Hilson aliamua kuweka wazi kuhusu yeye kukutana na anguko kubwa sana lenye kishindo kizito kimuziki, huku akifafanua kuwa Kuvunjika kwa mahusiano yake yaliyodumu kwa miaka 11 lakini pia kukutana na vidole vingi vya watu na hata kupewa pressure kubwa na watu wanaomzunguka vilikuwa ni chachu kubwa ya kuanguka kwake

Lakini bwana, kumbe kuna jambo lingine ambalo kama tulikuwa hatulifahamu, basi na tulifahamu lkeo kupitia hapa hapa Ndugu zangu.

Bifu zito lililokuwepo baina ya Keri Hilson na Mwanamama Beyonce pamoja na CIARA, ndivyo pia vilichangia bibie huyu kuamua kukaa kimya maana lilimuathiri kwa namna kubwa sana

Ishu Iko Vipi sasa wakubwa wa kazi, Kunako Kipindi cha Mwaka 2007 mpaka 2011, Keri Hilson alikuwa anatarajiwa huku akitengenezewa mazingira ya kuwa Msanii Bora na Malkia wa muziki wa RnB kutokana na uwezo ambao aliouonesha katika Vitu mbali mbali

1. KUWA BACKGROUND ARTIST WA WASANII MBALI MBALI
Uwezo mkubwa wa kuimba wa Keri Hilson, ulimfanya akawa Background wa wasanii wengi sana akiwemo CIARA, KELLY ROWLAND, USHER, LUDACRIS, BRITNEY SPEARS, TONI BRAXTON na wengineo Wengi sana. hii ilimtengenezea mazingira makubwa ya kuitwa Malkia Mtarajiwa wa RnB

2. KUANDIKA NYIMBO KADHAA ZILIZOHIT
Keri Hilson aliandika mikwaju kadha wa kadha ya wasanii ambayo ilihit kwa asilimia kubwa. Mfano RUN AWAY LOVE ya LUDACRIS Feat. MARY J BLIDGE, TAKE ME AS I AM ya MARY J BLIDGE, LIKE A BOY ya CIARA, ICE BOX ya OMARION, GIMME MORE ya BRITNEY SPEARS, WAIT A MINUTE ya PUSSY CAT DOLLS na nyinginezo kibao

3. KUANDAA SOUND TOFAUTI
Keri Hilson akifanya kazi na Timberland, walifanikiwa kutengeneza sound mpya kabisa na ya kipekee ya muziki wa RnB huku bibie huyo akiwa ni mmoja wa wasanii ambao waliandaa melody nyingi tamu na nzuri zaidi. Uzuri huo ulimfanya apewe kolabo nyingi sana na hata kutengeneza jina kubwa

Lakini sasa, Kuna kitu kilikuja kutokea ambapo inasemekana Tabia ya Keri Hilson ilianza kubadilika huku akionesha dhaihiri kuwachukia baadhi ya Wasanii na hata kuleta Pozi za hapa na pale.

Katika hilo, Keri alianza kutajwa kuwana Beef na Wasanii BEYONCE, RIHANNA na CIARA. Katika hilo, Keri aliwadiss Ciara na Beyonce katika Track ya TURN ME ON Remix, huku Beyonce naye akirusha Dongo zito kwa Keri Hilson kupitia TRACK ya DIVA....

Baada ya hilo kufahamika, madongo yalianza kurushwa huku na kule, na mpaka hivi sasa, weekend hii, Keri Hilson aligusia hilo hilo pia kuwa katika sehemu ya kuwa na Msongo wa Mawazo

MNADA BANNER