REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MTOTO WA SHAKIRA NA PIQUE NDIO HUYU

6:18:00 AM Add Comment
 SMILING : Shakira akiwa na mumewe Pique katika Pouz

LIKE FATHER, LIKE SON : Pique akimbusu mtoto wake Milan

NIPE FAGIO PROJECT: Washiriki wa Miss Utalii Taifa Waungana na Meya Kufanya Usafi Jijini DSM

6:11:00 AM Add Comment
 TUKO BIZE: Walimbwende hao wakiwa katika zoezi la kuokota taka, huku wakiwa wameambatana na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (Mwenye Suruali ya Khaki)

 TUNAPENDEZA : Washiriki hao wakiendelea na zoezi lao

 DUH SIO KAZI RAHISI..NGOJA TUWEKE POZI KWANZA : Washiriki hao wakiwa katika Picha ya pamoja na Meya wa Ilala, Jerry Slaa

YEEEEEEES : Washiriki hao wakiwa wamenyoosha mikono kuashiria wanashangilia jambo

CONFIRMED: RADI YAUA WATANO MBEYA

6:02:00 AM Add Comment
WATU watano wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa kupigwa radi katika matukio matatu tofauti likiwemo lililoua ndugu watatu wa familia moja. 

Ndugu hao watatu wakazi wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi wamefikwa na mauti Februari 5 mwaka huu majira ya saa saba mchana wakati mvua kubwa iliyoambatana na radi za mara kwa mara ikiendelea kunyesha wakiwa nyumbani. 

Afisa mtendaji wa kata ya Nyimbili Lingtone Nzowa amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Jerumana Halinga(35),David Halinga(5) na Kumi Halinga(3) ambapo pia radi hiyo imemjeruhi mtoto wa miezi tisa ambaye jina lake halikufahamika mara moja. 

Tukio la pili limetokea katika kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu Wilayani Mbarali ambapo radi iliyotokana na mvua kubwa imempiga Kasim Sagutangu na kusababisha kifo chake ambapo diwani wa kata hiyo Juntwa Mwalyaje amesema mvua hiyo imenyesha Februari 3 majira ya saa nane za mchana. 

Tukio la tatu limetokea februari 3 katika kijiji cha Mbagala Kata ya Ilembo wilayani Mbeya ambapo mwanamke Kotanida Petro amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa shambani kwake. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo ya vifo vya watu watano vilivyotokana na radi.

MNADA BANNER