REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

INSTA COP: HATA BABA YAKO ANANIJUA...AU NIKUPE NAMBA YANGU? : CHIDDI BENZ

2:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
#WatuWaMungu kuna Jamaa mmoja alijitia kumkandia Chiddi Benz "Chuma kwa Madai kuwa ameisha na hana lolote kwa sababu ya Kubwia Miunga (Dawa za Kulevya)

Sasa, Jibu alilolitoa Chiddi kupitia Instagram, Insta Cop tuliliona tukasema sio mbaya kama na wewe Tukikuhusisha Kabisaaaaa



MONEY ! MONEY ! MONEY ! : ETI KEYSHIA COLE AMEKUWA "CHIZI" NA MAYWEATHER TENA?

2:27:00 AM Add Comment

Na Samuel Richard "Sam Rich"
#WatuWaMungu Hivi kweli kuna kitu ambacho huwa kinaweza kufunika Pesa linapokuja suala zima la Furaha ya Moyo au Roho?

WAUNGWANA wanadai kuwa, Baada ya Floyd Mayweather Jr kumtandika McGregor na kuchukua Mkwanja ule Wote, basi yule Ex wake wa Mwaka Jana, Keyshia Cole, ameanza kujisogeza Taratiiiibu

Kwa Mujibu wa Waungwana Pia ambao huwa hawapendi U-Makuzi, walidai kuwa, Siku ya Mtanange, Keyshia Cole ambaye pia ni Ex-wa Rapper Birdman, alikuwepo uwanjani. Na Baada ya Floyd kumchapa McGregor, alifanya kila awezalo, kujipenyeza huku na kule, mpaka akafanikiwa kumfikia Floyd Mayweather Jr na hata kutandika naye Picha

Kinachokuja kuduwaza Zaidi ni kwamba, tangu waachane, Keyshia hakuwa ni mtu wa kumsifia ama kujiweka Karibu sana na Floyd, lakini baada ya Kushinda kibunda kile cha Fwedha, ikawa ndo Njia.

BAADA YA KUDAI KUWA KAFANYA TRACK NA TUPAC !!!! : MSIAMINI KILE MDOMO UNACHOONGEA-CHIDI BEENZ

2:03:00 AM Add Comment

Na Baba Juti & Instacop        
#WatuWaMungu kama mtakuwa ni wafuatiliaji wazuri sana katika Muziki hapa Nchini Tanzania, kuanzia Jana nadhani, Chiddi Benzi alinukuliwa akisema kuwa "Tupac Yuko Hai, na amefanya naye Track kwa Mensen Selkekta, and Very Soon ataiachia"

Katika Kauli Nyingine, Chiddi Benzi aliopngeza kuwa Tupac (Ambaye Ni Marehemu ) yuko Hai na Yuko Cuba, hivyo alienda kule, wakakutana na kutengeneza Track Hiyo, lakini Mzigo bado anao Tupac, so soon atamuachia.

Lakini katika Hali isiyotarajiwa, Dakika chache zilizokata (Wakati Tunapata Update Hii) kupitia Instagram account yake, Chiddi Benz ametoa Tamko Rasmi kuwa, kuna wakati huwa anazungumza  "Masihala" ili kupima akili za watu ziko Vipi

Katika Kukazia Zaidi, Chiddi a.k.a KING KONG "Chuma" alisema kuwa, usisikilize kile unachoambiwa kwa Mdomo

Tunamnukuu

UBAGUZI UTAKWISHA KWELI? : CHANCE THE RAPPER ASHAMBULIWA KWA KUWA NA MAHUSIANO NA MWANAMKE MWENYE ASILI YA KIZUNGU

1:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu tunafahamu Vizuri kabisa Rapper Kutoka Nchini Marekani, CHANCE THE RAPPER, ni moja kati ya Rappers ambao wamefanikiwa katika masuala kadha wa kadha kiburudani, na kijamii Zaidi

Kama mtakuwa Mnafahamu Vizuri, Chance The Rapper aliweza kujiachia na kufanya Kweli katika Track aliyoshirikishwa na Dj Khaled "IM THE ONE"

Lakini katika hali ambayo sio ya Kawaida, Chance The Rapper amejikuta katika "Kichambo" kizito baada ya kubainika kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanmke mwenye asili ya Kizungu, yaani Mwanamke Mweupe kama ambavyo wanasemaga wenyewe

Hii imekuja siku chache baada ya Rapper huyu ambaye ana Ngozi ya Kiafrika, kuonekana akifurahia kuwa Out na Mpenzi wake huyu, kitu ambacho kilishambuliwa sana na wengi

Aidha, Chance The Rapper amekuwa ni miongoni mwa wasanii ambao wanapinga sana Ubaguzi wa Rangi, na mara Zote amekuwa katika Kutetea Wamarekani Weusi, hivyo wanashangaa kwa nini anajihusisha na watu ambao wamarekani weusi wanawachukia kwa sababu huwabagua sana na huwatenga sana, ikiwemo kuwadhalilisha


NEW SONG !! : NAY WA MITEGO- MAKUzi

1:06:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Nimeisikiliza hii Track ambayo Rapper NAY TRUE BOY kaiachia Ghafla Bin Vuu !!, nimecheka Sana aisee

Track Inaitwa MAKUzi, na Producer ni AWESOME kutoka Free Nation. Unaweza kuiskiliza na wewe

INSTAC COP: OOH REALLY?... VANESSA MDEE KAGOMA KUANGALIA KALIO HILI, KISA?

2:39:00 AM Add Comment
 
Na Insta Cop  
Hapa Ndipo Unapokuja kuelewa kabisa kuwa alichokisema ZAIID kupitia Track yake Mpya Mpya Hivi ya ..."WOWOWO" kwa kweli kuna ka utamu fulani huwa kapo hata katika Kutizama wowowo

Bwana Bwana !!!, kumbe hata Wanawake wenyewe Huvutiwa kutizama "WOWOWO kama ambavyo Vanessa Mdee kathibistisha Hilo

INSTACOP imeweza kumnasa Binti huyu ambaye ni Hit Maker wa "kisela" na mikwaju mingineyo kama Vile "Cash Madame" na Nyinginezo Kibao tu, akitizama "Kalio" la Mtu aliyekuwa Mbele yake, na kisha akasema mwenyewe kuwa "Hakuna Kalio la Kutizama Pale"

ANAKUFURU? AU HAKUFURU? : ETI AMBER RUTT ANAMSHUKURU MUNGU KATIKA PICHA HIZI !!!!

2:08:00 AM Add Comment

Na Samuel Richard "Sam Rich" 
#WatuWaMungu Binafsi sijamuelewa Huyu Video Vixen ambaye wengi ni kama hawamuelewi na wanamuita "Mbaya kuliko Wote"

Kitu ambacho kimekuja kunistua asubuhi ya Leo, ni pale moja kati ya wadau wakubwa wa "Baba Juti Blog" kutuambia kuwa uzame kwenye account ya Video Vixen huyu kuona "Upuuzi" alioufanya.

Kinachoshangaza ni kwamba, Wakati Amber Lulu anatuhumiwa kuachia Picha ya Utupu akiwa na Young Dee, bado Amber Rutt anazidi kumimina Picha za kuabisha Zaidi huku akitoa kauli ambayo inaonekana kukufuru

Hebu tuongee vuzri kuhusu hili... Yeye kapost hivi, eti anamshukuru Mungu Kwa Yote (ikiwemo kuonesha hayo mauchafu yake... alistahili kumshukuru Mungu Kweli?)

Tunamnukuu
"Matusi ndo chakula 🍵🍞yangu so ukinitukana ndo unanifanya nizid kuwa mimi ,ahsante mungu kwa yote 🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏 #umechelewakunijua"

Ni Kweli Tumechelewa kumjua Binti huyu, lakini sio kwa Kufuru hizi halafu anatoa Shukrani kwa Mwenyezi Mungu. Kwann asimshukuru Shetani kwa kumpa akili za kipuuzi na kupost Mauchafu haya?

KUDAAADEKI !!!!! : "HALAFU NYIE MNAOSEMA SINA SHEPU.....!"- NISHA BEBE

1:56:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
GOOD MORNING TANZANIAAAAAAAA !!! And Off Course Kumekucha Upande wa Bongo Movie, maana sio kwa "ndimu" aliyamua kukamua Muigizaji wa Bongo Movie kwa upande wa Mabinti, tunamzungumzia Nisha Bebe

Kama Mtakuwa ni Mashabiki wazuri na wafuatiliaji wazuri kabisa wa Msanii huyu, Week hii mnajua kuwa amesherekea Kutimiza Miaka yake Kadhaa tangu aanze "Kuinusa" Dunia hii

Lakini Katika Hali Nyingine, Binti huyu ambaye pia ni Mjasiliamali Mzuri tu ambaye pia ni mkali zaidi katika "Comedy" aliamua kulimimina la kwake kwa wale wote ambao humchamba kwamba Makalio yake yamepigwa PASI kitu ambacho kinaonekanaga kumkwaza sana bibi huyu

Kupitia Instagram account Take, Nisha aliandika Hivi

  • "Halafu nyie mnaosema nimepigwa pasi sijui sina shepu #MUNIKOME TUKIVAA VIGODORO MANENO,MTU AKIWA ALIVYO MANENO,hemu chunguzeni wanawake wazuri wote duniani na wenye mashepu na status zao,ndo wale wanaoishia kupiga picture za uchi,kujiuza,kuishi kwa kutegemea mabwana n.k.

    Then tazama status za waliofanikiwa wote.

    OMBA MUNGU AKUPE AKILI,AFYA NJEMA,IMANI,HESHIMA,UPENDO,MAARIFA NA KIPATO,SOTE TUMEUMBWA KWA MFANO WAKE.

    KUTENGENEZA SHEPU NI DOLAR 6000 TU (ML.10 NA KADHAA)NI SAWA NA NISTOPISHE KUSAFIRI SAFARI MBILI ZA NJE NINAZOENDA KILA NDANI YA MIEZI MIWILI,NIJIBADILI KWA KUJITENGENEZA HIZO SHEPU ZENU INDIA AU THAILAND.

    NAPENDA MUNGU ALICHONIPA NA NAJIVUNIA,SIISHI KIFEKI FEKI KAMA WEWE BORODOZWA,WE UNAYEKOSOA WATU WKT HUNA MBELE WALA NYUMA SURA KAMA ULOTAPIKWA NAKOBRA.

    MUDA HUO UNAOKOSOA UNGEJIINGIZIA KIPATO USINGEKUWA UNAKOPA BANDO #ISHIMAISHAYAKO B*TCH NAJIKUBALI NA HALI YANGU."


MAJIBU: ALICHOKISEMA MASTER P BAADA YA KUDAIWA KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MKE WA T.I-Tinny

1:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu kuliibuka Taarifa za kushtua kidogo kuhusu Mke Wa T.I kuwa Moyo wake na mahaba yake yako kwa Mkongwe wa Hip Hop Ulimwenguni, MASTER P, na sio kwa Mumewe wa Ndoa, T.I

Kwa Mujibu wa SANDRA ROSE, taarifa ambazo zimemenika ni kwamba Licha ya kwamba Tinny ni Mke wa Ndoa wa T.I, hiyo ni kwa sababu ya familia yao ambayo inahusisha watoto watano ndani yake, lakini ukweli ni kwamba, Master P ndiye kila Kitu

Pia Mtandao huo ukatoa Taarifa Nyingine kuwa, Master P humpatia kila kitu Tinny, hasa kile ambacho hupewa na T.I, ndio maana hawezi kuacha kumpenda

Katika Kukazia zaidi, Mtandao huo ukamimina kuwa, MASTER P alimpatia Nyumba Tinny, pamoja na Timu ya Mpira wa kikapu inayoitwa NEW ORLEANS GATORS kitu ambacho eti kinaashiria kuwa wawili wapo katika Mahaba Mazito

Umri pia ukahusishwa kuwa, Master P ana miaka 47 na Tinny ana miaka 42, hivyo ni watu ambao wamekuwa karibu ili kuendeleza mahusiano yao kwa Umakini zaidi

MAJIBU YA MASTER P:  
Baada ya Kukutana na Sereka hilo, Master P akiwa mwenye mshangao Mkubwa, alikanusha Taarifa hizo na kusema kuwa hawezi kufanya hivyo na wala hakuna kitu kama Hicho maana anamuheshimu sana T.I

Tunamnukuu
"Mitandao ya Kijamii ni Zawadi na pia ni chachu ya maumivu na udhalilishaji. Hebu tufutilie mbali hizi fununu za Lugha ya Mwili. Mimi sina mahusiano ya kimapenzi na Tinny. Nilikutana nae katika Mkutano wa waandishi wa habari kuhusu GMGB na ndipo tukapiga Picha. Kwa taarifa yenu ni kwamba sie tunafanya Biashara. Ninamiliki Timu na yeye anamiliki Timu. Watu lazima wawe wamekwazika na kuchukia, pia hawana muda wa kuendekeza hizi tuhuma za Uwongo. Huyo Binti aliyetengeneza hizi Fununu, tafadhari acha. Ukweli utakuweka Huru. Unatakiwa umuombe kila mmoja Msamaha. Ninaheshima kubwa sana kwa T.I. Ninachowaombea yeye na Familia yake sio zaidi ya Mema "


HALELUYA : CANNIBAL KUTOKA NCHINI KENYA KAAMUA KUOKOKA

3:17:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu kuna tarrifa kuwa Rapper CANNIBAL kutoka Nchini Kenya Hivi sasa ameamua kuokoka kabisaaaaaaaa

Kupitia kenyan-post.com, Cannibal alidai kuwa wengi walibaini ukimya wake katika Soko la Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Humo, lakini hivi karibuni watamsikia katika Ulimwengu wa Muziki wa Injili, maana anahisi huko ndiko anakostahili kuwa

Tunamnukuu
"Sababu kubwa ya Mie kuwa Kimya, ni kwa sababu nimekuwa nikifikiria sana Kuokoka. Nimekuwa nikigombana sana na nafsi yangu kwa muda Mrefu.  Nafsi yangu imekuwa ikitaka kumjua Mugu, wakati huo, inataka Mambo ya Kidunia"


WALLAH WAKENYA MKO VIZURI- HII NI COVER NYINGINE YA DESPACITO

3:04:00 AM Add Comment

Na Sambuli Joseph 
#WatuWaMungu tunafahamu vizuri kabisa kuwa Mkwaju wa DESPACITO kutoka kwa LOUIS FONSI umekutana na Covers Nyingi Sana

Sasa, kutoka Nchini Kenya , huyu hapa ni Binti ambaye Pia ametukuna. Anaitwa VIOLA KARURI

JAMANI" BINTI ALIYEMUUA MDOGO WAKE KWA AJALI YA GARI, KISHA AKAMREKODI KUPITIA INSTAGRAM, AMESEMA ALIFANYA HIVYO KWA SABABU ALIHITAJI FEDHA (VIDEO)

2:44:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu sijui hii hatua tuitafsiri kama ni kitu kizuri ama kama ni kitu kibaya, maana inachanganya kwa kweli

OBDULIA SANCHEZ , Binti mwenye Miaka 14, aliingia Hatiani baada ya Kusababisha Ajali ambayo ilichukua Maisha ya Mdogo wake mwenye Miaka 14 na kumjeruhi binti Mwingine

Jeshi la Polisi lilitoa Taarifa kuwa, Obdulia alikuwa akiendesha gari hilo akiwa amelewa, huku akiwa amefungulia Muziki kwa Sauti kubwa sana, na akiwa Live Kupitia Instagram, hali iliyosababisha apate ajali katika Eneo la LOS BANOS huko Califonia, Marekani

Pia Taarifa za Kiuchunguzi zilidai kuwa, Gari ilikosa Mwelekeo na kugonga Uzio kisha Kupinduka, na Mdogo Wake JACQUELINE kupitia Dirishani (Maana hakuwa amefunga Mkanda) na kisha Kufariki alipotua Chini

Jambo la ajabu ni kwamba, Obdulia aliendelea kuwa Live Instagram huku akionesha watu zaidi 5000 waliomfollow katika Account yake, namna ambavyo mdogo wake akifariki, huku akisema "NIMEMUUA MDOGO WANGU, LAKINI SIJALI"

Wakati akijitetea katika Maelezo yake, Obdulia anadai kuwa, alifanya hivyo na hata kuruhusu watu washuhudie akifa, kwa ajili ya kuchangisha Fedha za Mazishi ya Mdogo wake huyo, maana familia yake isingeweza

Pia anaongeza kuwa, asingefanya hivyo kwa mdogo wake kwa nia mbaya, ila alijua kabisa kuwa amemuua mdogo wake, na familia yake isingeweza kuhimili gharama za mazishi

"Nilifanya Hivyo kwa sababu ninafahamu nina followers zaidi ya 5000. Ilikuwa ni njia pekee ya kumsaidia Mdogo wangu apate Mazishi Mazuri. Nisingeweza kumuanika Mdogo wangu kiasi hicho. Samahani kwa kuachia Video hiyo. Ninaonekana katili wa ajabu. Lakini nilifanikisha Nia yangu. Nilishawishi Umma unichangie Fedha maana familia yangu sio Tajiri"
R.I.P : JACQUELINE SANCHEZ Mdogo wake Obdulia, ndiye alifariki katika Ajali hiyo maana hakuwa amfunga Mkanda wa Gari

Familia hiyo ilifanikiwa kupata USD 12,630

OH MY GOD JAMANI !!! : PINK ASIMULIA NAMNA BINTI YAKE ALIVYOJIHISI NI MBAYA WA SURA !!!!!

2:16:00 AM Add Comment

Na Samuel Richard "Rich Sam" 
#WatuWaMungu kwa Wale ambao Mna watoto, tunaamini kabisa huwa mnakutana na Maswali Mengi kutoka kwa Watoto wenu.

Katika Maswali hayo, kuna yale ambayo huwa yanavutia, yanafurahisha, yanachekesha, yanashangaza, yanaduwaza, na hata mengine huiwa yanaumiza sana

PINK ni moja kati ya Wazazi ambao wamekutana na kitu kama Hicho kutoka kwa Binti yake ambaye anaitwa WILLOW ambaye ana umri wa Miaka 6 kwa Hivi sasa

Kupitia Tuzo za MTV VIDEO MUSIC AWARDS 2017, Hitmaker Huyo wa "Family Potrait" aliweka wazi kuwa, kuna siku alikuwa akimpeleka Binti yake huyo shule, na wakiwa kwenye Gari, Binti yake alimuuliza kuwa ni kweli yeye ni Binti mbaya Duniani?, maana amekuwa akikutana na Ukosoaji mwingi kuwa anafanana na Mvulana.

Pink anadai kuwa, aliumia sana kukutana na kitu hicho, na ndipo alimuambia kuwa, licha ya yeye kutokuonesha mabadiliko yoyote katika Mwili wake kuanzia Nywele, mwili na mengineyo, lakini Bado anavutia na ana mafanikio makubwa sana

Huyu Hapa

DUDE: WENGI WANADHANI NILIFARAKANA NA MRISHO MPOTO KUHUSU BONGO DAR ES SALAAM (VIDEO)

1:47:00 AM Add Comment

SOURCE: SASA TV  
#WatuWaMungu tunafahamu Vizuri kabisa kuwa Igizo la BONGO DAR ES SALAAM lilikuwa likisababishwa na DUDE pamoja na Mrisho Mpoto, lilikuwa kivutio na Elimu kubwa sana kwa Wageni na wakazi wa Jiji La Dar Es Salaam

Watanzania Wengi waliokuwa wakilifuatilia kwa ukaribu sana kupitia kituo cha Televisheni TBC 1, walikuja kushtushwa na hata kuumia baada ya Igizo hilo kusitishwa Ghafla, wakati bado watu wanalihitaji.

Igizo hilo liliwapatia Umaarufu Sana Dude, Flora Mvungi, na wengineo kadha wa Kadha, lakini nini kilikuwa Nyuma ya kusitishwa Kwake?

Wengi walikuwa wakiamini kuwa, Mrisho Mpoto na Dude wameshindwa Kuelewana na mpaka kufarakana na Bongo Dar Es Salaam kuvunjika, lakini Dude huyu hapa anasimulia


MUNGU OKOA JAHAZI !!!: YULE MSANII WA R&B AMBAYE ANADAIWA KUTOA HARUFU, SASA YAMEMSHINDA

1:38:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu mnamkumbuka yule Msanii wa R&B Nchini Marekani ambaye tuliwahi kukuambia kuwa Wengi wanalalamika kuwa "anatoa Harufu mbaya?"...sasa kuna hili jipya kuhusu yeye

Yes, anaitwa  KEHLAN ambaye safari hii kaamua kuachana kabisa na masuala ya Kutinduana na Wanaume kutokana na lawama za kutoa Harufu Nzito, na ameamua kujikita katika Mapenzi ya Jinsia Moja

Kwa Mujibu wa Taarifa ambazo tumezipata mpaka hivi sasa, ni kwamba Kehlan amekuwa akikutana na changamoto ya wanaume kudumu naye katika Mahusiano, huku sababu kubwa ikiwa ni kutoa Harufu Nzito, hasa katika Sehemu kadha wa kadha za Mwili wake
MAHABA: Kehlan (Kulia) akiwa na Mpenzi wake Mpya (Jina halijapatikana)

Hivyo Kutokana na hilo, Kehlan ameamua kujitosa katika Mahusiano ya Jinsia moja, maarufu kama Usagaji

MANI FONGO : SIJAMSHAWISHI MKALI WENU AACHANE NA TIMAMU MEDIA

2:42:00 AM Add Comment


Na Shaibu Ali & SASA TV (Dar Es Salaam)
#WatuWaMungu tunaamini kuna watanzania wengi sana wamekuwa wakivutiwa mno na Vichekesho vya Mchekeshaji MKALI WENU ambaye wengi tulikuwa tunafahamu kabisa kuwa alikuwa chini ya Timamu Media.

lakini Hivi karibuni, kumekuwa na Taarifa kuwa Mkali Wenu aliamua kupiga Chini Makubaliano ambayo yalikuwa yameundwa na Timamu Media na yeye, na kuamua kuchukua Zake.

KISA HIKI HAPA
Lakini kwa Taarifa za Chini Chini ambazo pia tulizinyaka, ni kwamba , Mani Fongo ambaye ni msanii wa Muziki wa Singeli kutoka hapa hapa Nchini Tanzania, ndiye alikuwa chachu ya kumshawishi apige Chini Timamu Media, na kuchukua maisha Yake Mengine.

Katika Ufafanuzi wake, Manifongo alidai kuwa, Mkali wenu ni zaidi ya rafiki yake, kuna kipindi alilalamika kuwa, anajisikia Vibaya kuwaona wenzake (akina Manifongo) wakiwa na maisha Mazuri, wakiendesha Magari, ilihali yeye ni Msanii Mzuri na anakubalika na hana Kitu

KAPIGA HATUA !!!!: HATIMAYE AZEALEA BANKS KAFUNGUA RECORDS LABEL YAKE?

2:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWa Mungu kama mtakuwa ni wafuatiliaji wazuri wa Muziki wa Hip Hop Ulimwenguni kote basi mtakuwa mnafahamu Vizuri kuwa kuna Bibie ambaye ana majanga kupita maelezo aisee

Mamito huyu anaitwa AZEALEA BANKS ambaye ni Rapper wa Kike ambaye kimuziki amekuwa Chini sana kupita maelezo, yaani mpaka inaboa.

Lakini baada ya kukutana na anguko kubwa, alianza kutamani kubakisha jina lake katika akili za watu, hali iliyomtu akutane na majanga Mengi ikiwemo kupigwa, kujichubua na hata kuachia Picha za Utupu Hivi karibuni, kitu ambacho kiliwashtua wengi sana sana sana

Lakini kitu ambacho kimewashangaza wengi, ni baada ya Bibie Huyu kudai kuwa hivi, Hivi sasa amefungua Records Label yake na ilikuwa ni Ndoto yake ya Muda Mrefu sana

Records Label hiyo inafahamika kwa jina la CHAOS & GLORY RECORDS.

AISEE !!!! : AVRIL AMEKIRI KUWA AMESHAWAHI KUWA NA MAHUSIANO NA.............

2:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Katika Maisha ya kawaida, Mwanaume yoyote akipewa Gape la kukutana na Msanii AVRIL kutoka Nchini Kenya, basi lazima atapata kigugumizi hasa pale atakapoona lile tabasamu lake.

Lakini ukiachilia mbali hayo, wengi tunafahamu kuwa Hivi sasa Avril yuko Single ingawa hatuna uhakika kama she is Ready To Mingle.

Hivi Sasa Hit Maker Huyu wa CHOKOZA, anafanya Vizuri sana na Mkwaju wake wa BABBIEE akiwa amemshirikisha Msanii wa Reggae & Dance hall kutoka Uganda, A PASS.

Ukiachilia Mbali masuala yote Kiujumla, kama ulikuwa hujui, ndani ya hii wiki, Avril ameweka wazi kuwa katika Mahusiano yote ambayo amewahi kuwa nayo, amewahi kukunjuka na Kijana ambaye ana Umri Mdogo kuliko yeye.

Ingawa Hakumuweka wazi Mtu huyo, ila Bibie huyo hakuona aibu wala haya kukiri mbele ya wanaafrika mashariki kuwa tayari ameshawahi kufanya hivyo na ni sehemu ya historia ya maisha yake.

BAADA YA KUDHALILISHWA !!: BOBY VALENTINO KAAMUA KUFANYA HILI WATU WA MUNGU

1:36:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.   
#WatuWaMungu Hatimaye Bobby Valentino ameamua kuamka na kufungua Makucha yake baada ya Wiki Kadhaa zilizopita kudhalilika vibaya  sana kupitia Mitandao ya Kijamii

Hatimaye Msanii Bobby Valentino na Yule Mwanamke aliyejibadili Jinsia kutoka uanaume (Transgender) anayefahamika kwa jina la Reima Houston, wanatarajia kuvaana uso kwa uso Kizimbani, ikiwa ni baada ya Reima kumrekodi Boby Valentino na kumpost Mitandaoni

Kama hukufahamu, ni kwamba, Reima ambaye ndiye Mwanamke, alichukizwa na Kitendo cha Boby Valentino, cha kugoma kumlipa Hela yake baada ya kumpa huduma ya Ngono, kitendo ambacho kilimlazimu amrekodi Mkali huyo wa TELL ME akikimbia Peku peku kutoka katika Chumba alichokuwa akipewa Huduma

Bobby V ndiye aleyefungua Mashtaka na kutoa taarifa ya kutaka Reima akamatwe kwa kosa la kumdhalilisha kwa sababu ya USD 2000, na alifungua mashtaka hayo kupitia Mwanasheria wake GERALD GRIGGS

Hata Hivyo, Reima alikuwa akitoa taarifa kupitia Interview Kadha wa kadha kuwa Alifanya hivyo kwa sababu alidhurumiwa

Madai makubwa ya Bobby ni kwamba mwanamke yule ni Kahaba, hivyo alitumia kila njia, ili amlipe USD 2000, kitu ambacho hakustahili kukipata, bali ilikuwa ni kumtishia.

MUNGU LINDA WATOTO WETU ; DEREVA WA GARI LA SHULE AKUTWA AMELEWA HUKU AKIENDESHA GARI LA WANAFUNZI 31

1:22:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WAZAZI sanjari na Walezi, naamini tunatakiwa kuwa na tahadhari kubwa sana hasa linapokuja suala la Watoto Wetu ambao wanachukuliwa na kurudishwa Nyumbani kwa Gari la Shule

Na Hii Pia sio kwa Wazazi na Walezi tu, bali hata kwa Walimu na Wamiliki wa Shule ambazo hutoa huduma ya Usafiri kwa Wanafunzi wao.

Dereva Mmoja Nchini Marekani katika Jiji la Georgia, ameangukia katika Mikono Ya Sheria baada ya kubainika kuwa anaendesha Gari ambalo limebeba Wanafunzi 31, huku akiwa yuko "Mtungi" kichwani mwake

Kwa Mujibu wa Taarifa Rasmi kutoka Jeshi la Polisi huko Huko GEORGIA, Bi Carole Eutheridge, amefikishwa mahakamani Jumatatu ya Wiki hii baada ya kubainika katika Hatia

Katika Gari hilo la Wanafunzi, Carole alikutwa akiwa ameficha Chupa kubwa ya TEQUILA, chupa Ndogo za Vodka pamoja na Chupa Ndogo Nyingine za Vidonge ambavyo havijaainishwa Mpaka Hivi sasa

Wanafunzi ndio waliofichua Uovu huo baada ya kutoa Taarifa kwa Wazazi wao kuwa Dereva wa Gari la Shule yao, huwa ni mtu ambaye anapiga "Makali" kwanza, kisha anawaendesha.

Hata Hivyo, mmoja wa Waajiri wa Zamani wa Dereva huyo, alidai kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya Bi. Carole, na wao walimtimua Kazi January Mwaka Huu


HEBU TUAMBIE !!! : ET HUYU NDIYE VIDEO VIXEN MBAYA KULIKO WOTE BONGO? (PICHA 12)

7:48:00 AM Add Comment

Na Hamis Ally   
#WatuWaMungu Tunajua Vizuri kabisa kuwa Soko la "Video Vixens" ama "Video Queens" limetufichulia Mambo Mengi sana katika Soko la Muziki na hata katika Maisha ya Dada Zetu ambao wanapenda Lifestyle ya aina Fulani

Wengi sana wanafahamika na kazi zao zinaonekana kabisa mfano Mzuri ni akina Hamisa Mobeto (Mama Dully), Giggy Money, Amber Lulu, Nai Huddah, Na Wengineo Wengi sana ambao tunawaona wanatokea Mara kadhaa kwenye Video mbali mbali

Sasa, Hivi Majuzi lilikuja kutopkea la Kutokea baada ya Kutokea Video Vixen Mwingine, anayefahamika kwa jina la AMBER RUTT.

Wengi tulikuwa hatumfahamu, lakini tulikuja kuanza kumsaka baada ya kuona "Kichambo" alichokipokea toka kwa watu mbali mbali akiwemo JACQUELINE WOLPER na wengineo, baada ya kusambaza Picha za Takriban Nusu Utupu.

Sasa Kama mlikuwa hamumfahamu, inasadikika kuwa Ndiye Video Vixen "Mbaya" kuliko Mavideo Vixen wote Bongo (Sio Maneno Yetu Lakini)

Comments Nyingi katika Instagram account Yake, zinamtukana haswa na hata kumuita majina ya Wanyama kama Vile Paka, n.k

Sasa, Tumeona Tumlete Kwenu, ili na nyie Mseme, kama Kweli ni Hivyo anavyotuhumiwa, ama Vipiu?

Picha zake Hizi hapa  











MNADA BANNER