REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MTOTO WA LIL WAYNE: KUWA NA BABA MAARUFU SIO KAZI RAHISI

3:07:00 AM Add Comment

   Na Baba Juti  
WENGI Tunafahamu Vizuri kabisa kuwa Binti wa Lil Wayne hivi sasa ni Mkubwa na ameshaanza harakati za kutafuta Mkwanja wake ili aweze kufanya kile ambacho anadhani kipo sahihi katika ndoto zake

REGINAE CARTER amedai kuwa, Haikuwa na Wala Sio Kazi rahisi kuwa na Baba ambaye Ni Maarufu, tofauti na wengi ambao hudhani ama kutamani

REGINAE ambaye hivi sasa ana Umri wa Miaka 18, amedai kuwa, wengi wanahisi kuwa ukiwa na Mzazi Maarufu, basi ndo umemaliza kila kitu na kila mtu atakuchukulia Sahihi, la hasha, kuna wengine wartakuenjoy Tu.

     Namnukuu      
“Niliwahi kuwa na Rafiki ambay nilimuamini kwa kila kitu, lakini mwisho wa siku alinigeuka. Awali, hakuwahi kunionesha Dalili zozote za kuwa FAKE, au kama alikuwa anataka kuvuna kitu kupitia Jina langu na Baba Yangu (Lil Wayne). Hivyo katika hali hii , maishani mwangu hivi sasa, nahitaji kufahamu ni nani ambaye yupo kwa ajili yangu, na ni kitu ambacho sio Rahisi”

Katika Kujifunza hayo yote, Reginae anahitaji kufanya kazi kwa juhudi ili nayeye atengeneze Jina lake tofauti na Umaarufu wa Baba Yake


Binti huyu hivi sasa anahusika katika Kipindi cha TV kinachofahamika kwa jina la GROWING UP HIP HOP ATLANTA akiwa pamoja na watu wengine hasa Rapper BOW WOW

ETI NINI !!!?. NICKI MINAJ HUKOSA AMANI AKIMUONA MEEK MILL?

2:55:00 AM Add Comment

  Na Baba Juti 
#WatuWaMungu Hata kama haijawahi kukutokea, lakini siku ikifika basi lazima ka hali haka hata kwa Uchache katakukuta Tu automatically

Taarifa za Uhakika zinadai kuwa, NICKI MINAJ huwa anakosa amani kabisa anaposikia kuwa Rapper Meek Mill yupo karibu ama katika mazingira ambayo yeye yupo

Hiyo imetolewa na moja kati ya Wapambe ambao huongozana na Hit Maker huyo wa HIGH SCHOOL wakidai kuwa, hii siyo Mara ya Kwanza Nicki anaonesha dalili ya kutokuwa na amani hasa pale ambapo Meek Mill anakuwa katika mazingira ya karibu naye.


Mpambe huyo aliongeza kuwa, Kitendo cha Meek Mill kuingia katika Club ambayo Nick Minaj alikuwemo kwa ajili ya  Party yake, kilimkosesha Raha sana na kumuacha akiwa mwingi wa wasi wasi katika eneo alilokuwa ameketi.

Tofauti na Umbali ambao wawili hao walikuwa, Inasemekana NICKI alisisitiza Ulinzi wa Kutosha na wenye Nguvu katika eneo lake, ili kuepukana na Majanga ambayo yangeweza kutokea Muda wowote

Pia Inasemekana kuwa, Ilifikia Muda Nicki Minaj alizuia Watu waliokuwa katika Eneo la Meek Mill, kusogea katika Eneo lake, na hata kama kulikuwa na watu ambao wanapiga Picha, basi alikuwa akijitahidi kuwaminya

#WatuWaMungu : HAYA NDIYO MARADHI YANAYOMSUMBUA AUGUST ALSINA.. TUMUOMBEE KWA MUNGU

2:51:00 AM Add Comment

 Na Baba Juti  
HATIMAYE AUGUST ALSINA ameamua kuuweka wazi Ulimwengu kuwa ana tatizo ama Ugonjwa ambao umekuwa ukiitafuna hata Familia yake Kiujumla

Akizungumza na Mke Wa Will Smith , JADA PINKET, August Alsina ambaye aliusumbua Ulimwengu na Mkwaju wa NO LOVE aliomshirikisha Nicki Minaj , amedai kuwa amekuwa na tatizo la Msongo wa Mawazo ambalo mpaka hivi sasa linaonekana kumtafuna kwa asilimia kubwa sana

Katika Video Clip aliyopost kunako Instagram account yake, AGUST anadai kuwa ukiachilia mbali tatizo la Msongo wa Mawazo, Pia amekuwa akikabiliana na Tatizo la INI, ambalo limekuwa likimfanya augue Mara kwa mara


Na katika Maelezo yake, amesema kuwa, ameshakuwa na taarifa kuwa kuna baadhi ya wanafamilia wake ambao tayari wameshapoteza Maisha kutokana na Tatizo la Msongo wa Mawazo, ingawa walipambana sana ili kuwa Sawa

KWAN' KITU GAN' !!!!? : ASHANTI NAYE ETI KAONGEZA UKUBWA WA MATI***

2:47:00 AM Add Comment


   Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Kuna habari Mpoya kuhusu Bibie Ashanti ambaye hivi sasa ameamua kuchukua Uamuzi mpya ili kuboresha Vitu ambavyo anahisi vinahitaji Great Modification

Kwa Mujibu wa Muonekano Mpya aliokuwa nao katika Perfomance yake ya MEMORIAL WEEKEND, Ashanti alikuwa na Kifua tofauti na kile ambacho tumezoea kukiaona Niezi Kadhaa iliyopita kitu ambacho kilizua Mjadala Mzito sana

Aidha, waungwana wanadai kuwa, Ni Kweli, Ashanti alikuwa na kifua cha Kawaida sana kipindi cha Nyuma Kidogo, lakini kwa Hivi sasa kimekuwa Tofauti kidogo , kitu ambacho kinaashioria kabisa kuwa, Ashanti alifanya maboresho Muda Mfupi tu uliopita


Hata Hivyo, Ashant Mwenyewe hajaweka Bayana kama ni kweli kafanya Modification ama Lah, lakini kipindi cha Nyuma iliwahi kuenea kuwa anahitaji kuweka Utamu Mwingine katika Kifua Chake….

MNADA BANNER