REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TUMEMMIS KANYE WEST WA ZAMANI?

5:25:00 AM Add Comment
Na Baba Juti

WANGAPI wanakubali kuwa Rapper Kanye West Wa Zamani alikuwa ni Bora kuliko Kanye West Wa Hivi Sasa?... Lakini Pia, ni wangapi wanakubali kuwa Kanye West wa sasa ni Bora kuliko yule wa Zamani?

Swali hilo pia imebidi team tujiulize kama yanayosemwa na Business patner wa Jay Z yana ukweli wowote, ikiwa ni baada ya kuwepo na Mgogoro wa majibizano baina ya Jay Z na Kanye West


KAREEM BIGG BURKE ambaye ni Patner wa Jay Z katika Studio ya ROCA FELLA RECORDS amedai kuwa, mara ya kwanza wakati anamsikia Kanye West akimzungumza vibaya Jay Z na kudai kuwa hata watoto wao hawajawahi kucheza pamoja, iliweza kumshtua kila Mtu.


BURKER ANASEMA...
"Nilishtuka sana kasikia kile ambacho Kanye aliksema kwenye Jukwaa. hakukuwahi kuwa na tatizo baina yao.. kwa hiyo ukisikia kitu kama hicho tena hadharani , lazima ushtuke kidogo. Mara ya Mwisho namuona Kanye , alizungumza vizuri na Jay Z. Sina uhakika sana kama mahusiano yao yamefikia hatua hii. Na nilipozungumza na Jay Z kuhusu Ishu aliyoisema Kanye West, kila mtu alibaki akisema TUMEMMISS KANYE WEST WA ZAMANI. Kwa kile ambacho ninafahamu kutoka kwa Kanye, ni kwamba huwa ni mkweli sana. hivyo inaonekana kabisa kuwa kuna kitu ambacho kinaendelea baina yao kwa hivi sasa. Anaweza kuzungumza kitu kama hicho, lakini baada ya Wiki kama tatu, utamsikia tena akisema "Jay Z ni Kaka Yangu kabisa. "

Tofauti na Hilo, Nicki Minaj pia aliwahi kutamka kauli ambayo kila mtu ilimshtua kuhusu Kanye West, ambapo alidai kuwa Kanye West wa Zamani sio wa hivi sasa, maana kupitia kwa mkwaju wa GOLD DIGGER, alikuwa akiwapondea wanawake tegemezi sana na wanaotafuta pesa kwa njia za kijanjanja kijanjanja, huku akihamasisha Wanaume Weusi, kutwaacha wanawake Weusi kisa wanawake weupe. Lakini hivi sasa, imekuwa tofauti, na Kanye West ana Mke Mweupe na Gold Digger ambaye ni Kim Kardashian.

SUGE KNIGHT: NAMSHTAKI DR DRE KWA KUNITUMIA WATU WA KUUA.

5:19:00 AM Add Comment


Na Baba Juti
MENGINE yameibuka na kuzidi kumuweka Dr Dre katika Wakati Mgumu ambapo hivi sasa amefunguliwa Mashtaka ya Kutaka kuua.

SUGE KNIGHT ambaye alikuwa Mkuu wa DEATH LAW ambaye hivi sasa yuko anatumikia Kifungo chake Jela, amedai kuwa anafungua mashtaka dhidi ya aliyekuwa Swahiba Wake, DR DRE kwa madai kuwa amekuwa akijaribu kumuua kwa kumchora kwenye michongo ya kuuawa mara kadhaa na watu ama na mazingira tatanishi.


Kwa Mujibu wa File la Mashtaka ya SUGE KNIGHT ambaye pia anatuhumiwa kuhusika kwa asilimia fulani katika kifo cha Marehemu Tupac, inasemekana kuwa, sababu ya DR Dre kutaka kumuua, ni baada ya kutaka kumdhurumu asilimia zake za mapato katika BEATS BY DRE ambazo zilinunuliwa kwa mkwanja mnono na Kampuni ya APPLE

Kwa mujibu wa Mkataba ambao upo mpaka hivi sasa, ni kwamba Dre alitakiwa kumlipa 30 ya mavuno katika masuala ya burudani, lakini ikaja kusemekana kuwa, Dr Dre alihitaji kusitisha makubaliano hayo baada ya Apple kutokuhitaji kufanya kazi na SUGE KNIGHT


Pia Maelezo ya kesi yanaongeza kuwa,  SUGE anaamini kitendo cha yeye kupigwa Risasi mara 7 nje ya Ukumbi wa 1 OAK katika Week ya BET Awards mwaka 2014, ilikuwa ni Njama na maagizo ya Dr Dre.

JAGUAR: BADO SIJAOA MPAKA HIVI SASA

5:13:00 AM Add Comment


Na Mwamba-Kenya
AKINA dada mnaweza kuchangamkia Hii Tenda aisee !!!!

LICHA ya kufanikiwa Kimuziki na hata kumiliki mkwanja mzuri ambao unaweza kumfanya yeye na maisha yake  yakawa katika mstari ulionyoka.


Kama ulikuwa hufahamu, licha ya kuwa na hayo yote , kumbe mpaka hivi sasa Jaguar hajaoa, na hiyo ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe
Kupitia Facebook fan page yake mwenyewe, JKaguar alijibu swali akidai kuwa, mpaka hivi sasa hajaoa, hivyo hawezi kuonesha au kumzungumzia mwamke ambaye hayuko naye au ambaye hajamuoa.

BANNA ZORRO : AMEWAKUMBUKA HARD BLASTERS NA ALBAM YAO

5:10:00 AM Add Comment



Na Baba Juti
SIO kitu rahis kumuona msanii mwingine hapa Nchini Tanzania, anayefanya Style flani ya Muziki, na bado anasupport Style Nyingine ya Muziki.

Lakini Hii Imedhihirishwa na Banana Zorro ambaye ameshindwa kuzuia Mahaba yake, na kuamua kuwakumbuka HARD BLASTERS, kundi ambali liliwahi kuchukua akili za watu katika Miaka ya 90 mpaka kufikia 2000


Kupitia Instagram yake, Banana Zorro alipost ULBUM COVER ya Tape, kutoka Kwa Hard Blasters, iliyopewa jina la FUNGA KAZI, ambayo pia iliachiwa Mwaka 2000.

Katika Maneno yake, Banana amenyoosha mikono na kudai Ilikuwa ni kazi kubwa sana, na bado itaendelea kuwa Kubwa zaidi

NUKUU
Hard blaster hii album ilikuwa hatari na itaendelea kuwa kubwa zaidi katika Historia ya muziki WA kizazi kipya....#HBC

MNADA BANNER