REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WALLE: ANAPOPULIZIWA MOSHI WA SIGARA NA MTOTO WA KIKE.

1:40:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KAMA ni Hapa 255, ukamfanyia Kala Pina, Kitendo ambacho Rapper Walle amefanyiwa, hakika ingekuwa ni another Story !!!

Rapper Walle amejikuta katika Jazba kali baada ya kupuliziwa Moshi wa Sigara na Mtoto wa Kike Mmoja, Nje ya Club ya BOOTS BELLOW usiku wa Kuamkia Jana.

Lakini Licha Ya Kufanyiwa Yote hayo, Walle hakumfanya Chochote ingawa alidhararulika sana, zaidi ya kumwagia chakula alichokuwa amekishika mkononi.

Ingawa Wasamaria Wema walikuja kusaidia, na kuamua Ugomvi huo, bado Walle alionekana kupandwa na Makali ya Ndimu mpaka kuanza kumjibu tofauti kwa lugha isiyo Poa
Katika Kufafanua Msala Uliotokea, Walle anadai Kuwa Yeye alikuwa akifanya Masihala na Rafiki zake aliokuwa nao, na Ndipo alipopita Mdada aliyetamka sentensi "You People Are So Disrespectful" akimaanisa "Nyie Watu Hamna Heshima"

Rapper Huyo wa MMG anaongeza , baada ya kusikie Neno "Nyie Watu" alitafsiri kama ni neno la Kibaguzi ukizingatia aliyetamka ni Raia wa Urusi

Lakini baada ya kumfuata na kumuuliza vizuri kuwa alimaanisha nini baada ya kutamka neno "Ninyi Watu" na ndipo yule Bibie akampulizia Moshi.

lakini Baada ya Walle kuanza kuja juu, basi yule bibie alianza kumuuliza kama anataka kumfanya nini, lakini Rapper huyo akamwambia kuwa yeye huwa hapigi wanawake, ila kwa sababu kaonesha utovu wa heshima na nidhamu , ikabidi apige chini chakula chake

SNURA: VIDEO YANGU MPYA YA CHURA, INAMZUNGUMZIA MWANAMKE ANAYERUKA RUKA KATIKA MAPENZI

1:35:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
TUNAAMINI mashabiki wengi sana wa Snura Watakuwa Wamefurahi Kurudi kwa Chura, na hakika imekuwa hivyo baada ya kummiss kwa muda mrefu sasa.

Kupitia Mkutano wa Waandishi wa habari ambao ulifanyika siku ya jana, Snura amemshukuru sana Mheshimwa Waziri wa Michezo Utamaduni na Wasanii, NNAPE NNAUYE, kwa Kuruhuisu Video ya Chura ambayo ni Mpya, kupigwa katika Vituo Mbali mbali vya TV Nchini tanzania, sambamba na Audio ambayo itachezwa katika Radio Station Mbali mbali.


Tofauti na Hilo, Snura amefafanua kuwa, Maana halisi ya Chura, na Wimbo Mzima na kile alichokifafanua katika Video Hiyo, ni Mwanamke anayeruka ruka katika Mapenzi, na siyo Maana ambayo Wengi wamekuwa wakiitafsiri.

MNADA BANNER