REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MILIONI SITA TU, NDIZO ZITAKAZOOKOA MAISHA YA MTOTO HUYU..

8:54:00 AM Add Comment



MILIONI SITA zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani Said (1), ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa nje ya tumbo lake imeleezwa.

Akizungumza na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent ambaye ni Mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya kutolea haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.

Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia operesheni mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa.

Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.

“Mimi ni nachoomba ni msaada wa fedha ili niweze kumpeleka kwenye matibabu kwani sina msaada wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na hivi sasa naishi kwenye nyumba ya  mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani Kinondoni jijini baada ya kushindwa kupangisha chumba kwani sina kazi yeyote”alisema.

Aidha, alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya kufanyiwa operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo hata alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa madaktari na wahudumu wengine.

Alisema kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza wasiliana naye kwa kupiga simu namba 0715 83 77 00, na namba ya mwenyekiti huyo wa mtaa 0656780236.

Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Kijiji cha Uru,Moshi ambye alimzaa mtoto huyo na mwanamme aliyemtaja kwa jina la Abdalah Said, kabilake makonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.

JUSTIN BIEBER NA SERENA GOMES WAMEYAMALIZA?

8:49:00 AM Add Comment
Mtandao wa Kidaku kule Mbele, Umewahi kuripoti kuwa SERENA GOMEZ ambaye ni Mpenzi wa Justini BIEBER, amemblock Bieber kwenye Simu yake ili asiwe anampigia Simu.

Hali hiyo ilizua utata Mkubwa saaana  ikiwa ni huenda wameachana au Wana matatizo...

Lakini hii Ni Picha mabayo inawaonesha Bieber na Serena Gomez wakiingia katika Moja ya Hoteli kubwa huko OBAMA aland, ikiwa ni baada ya Jana yake, Bieber kumpeleka Serena Nyumbani Kwao na kusemekana kuwa alilala Huko huko

MIKWAJU MIPYA LEO.

8:29:00 AM Add Comment

OMMY DIMPOZ Ft. VANESSA MDEE in "ME & YOU"


Kwa Mujibu wa Ommy Dimpoz "Pouz kwa Pouz", Mwanadada Halima Mdee amekamua Vilivyo kabisa yani katika Track hiyo.
Hebu Fanya Mchakato uweze Kuisaka.

MIKWAJU MINGINE YA OMMY DIMPOZ
1. NAI NAI- Ft Ali Kiba
2. BAADAYE- Ft. Dayna 

******************************************************************
LINEX Ft. SUMA LEE in "BODA BODA" 

 Hivi Sasa Video Ipo Tayari, na Unaweza kuipata kirahisi zaidi katika YOU TUBE.
Ni Bonge Moja la Video, ambalo ninahuakika utafurahia Mwenyewe.

MIKWAJU MINGINE YA LINEX.
1. AIFOLA-Ft. Fundi Samweli

SABABU YA KUKATIKA OVYO KWA UMEME NCHINI, HII HAPA

8:10:00 AM Add Comment





Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza sababu zinazosabisha kukosekana kwa umeme katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine nchini.

Akiongea na Radio One asubuhi ya leo Mheshimiwa Muhongo alisema lilikuwepo tatizo katika mfumo wa gesi ambao umerekebishwa zaidi ya mara tatu na kusabasha gesi kukata.

“Tumeomba wataalamu wetu waangalie na ikiwezekana isitoke, sasa ikishatokea namna hiyo inamaanisha kwamba watumiaji wa gesi wanaendelea kutumia gesi iliyo kwenye hilo bomba, kama nyingine haiji inamaanisha pressure inapungua kwahiyo wanahitaji muda wa masaa ili pressure irudi kuwa sawasawa, “ alisema.

“Tatizo la pili ilikuwa ni kwamba mitambo yetu ile ambayo ilikuwa inatumia mafuta kama unavyojua kwa zaidi ya wiki mbili palitokea mtafaruku mafuta yalikuwa hayapo na kama unavyofahamu mafuta ndo yameanza kufika hata huko mikoani sehemu nyingi mafuta ndo yameanza kuwafikia watumiaji kwahiyo haya matatizo mawili yote tumeyaangalia kwa makini sana nadhani kwasababu ni vitu vinatokea mara kwamara tuna jitaidi visitusumbue tena.”

“Lakini umeme wetu mwingi hautokani na maji sasa hivi hilo ndilo Watanzania wana paswa kufahamu, umeme wetu mwingi unatokana na gesi kati ya asilimia 40 na 60 inategemea na uzalishaji wa siku hiyo ukoje alafu unafuata umeme wa mafuta na mwisho kabisa unafuata umeme wa maji.”

Alieleza kuwa tatizo jingine ni la miundombinu ya kusambaza umeme imechoka na hivyo kuhitaji marekebisho ya mara kwa mara.

“Miundombinu ni kwamba kweli imeshoka inahitaji muda kuweka miundombinu mizuri ambayo ni ya kisasa kwamfano kuna sehemu ambazo sehemu moja ikipata hitilafu karibu wilaya mzima inakosa umeme , saa zingine mkoa mzima kwahiyo hiyo ni miundombinu ya kizamani na hilo tatizo mafundi wa Tanesco wanajitaidi na Tanesco tumewaeleza kwamba wajitahidi sana kuwa wanakagua miundombinu yao na kutengeneza.”

Aliongeza kwa kudai kuwa sababu nyingine kubwa ni wizi wa miundo mbinu ya Tanesco ikiwa pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma na nyaya za umeme.

HONGERA AUNT EZEKIEL KWA KUOLEWA...LAKINI....MHHHHH!

2:39:00 AM Add Comment





 HAYA HAYA HAYAWI HAYAWI........................

Queen na Kichwa cha Bongo Movies kwa Upande wa Wanadada, AUNT EZEKIEL ambaye kwa sasa ni RAHMA, finaly amefunga Ndoa Rasmi huko kunako maraha Tele, DUBAI.
Picha ndo Hizi hapa, ambapo aunt kaolewa na Kijana nayekwenda kwa jina la DEMONTE
Hebu tuambiane jamani, Kuna uwiano kweli hapo?

MNADA BANNER