REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA : MTUHUMIWA.........

8:20:00 AM Add Comment

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha CHANNEL TEN, David Mwangosi akitoka Mahakamani Mapema Leo hii

SPORTS COPE : TFF YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI DHIDI YA AKINA MANJI

8:11:00 AM Add Comment
 Mwenyekiti wa Yanga FC, YUSUPH MANJI

Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:

1.Waombaji uongozi wa TPL Board

(a)Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeidanayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na  Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:

(i)  Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii) Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi  hiyo.


(b) Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa  na  Ndg. Daniel T. Kamna na  Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :

(i) Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii) Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(iii) Hana elimu ya kidato cha nne
(iv) Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFFimezitupa pingamizi hizo.  

(c) Pingamizi dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg.  Hamad Yahya Juma,kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:

(i) Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii)  Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa  ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

2.                   Waombaji uongozi wa TFF

(a) Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.

Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi.


(b) Pingamizi dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg. Mvella:

(i) Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.
(j) Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.

(c)  Pingamizi dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:

(i)  Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA).
(ii)  Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.
(iii) Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA
(iv) Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.

(d)Pingamizi dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi  na Ndg. Paul Mhangwa kwamba  hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).

Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).


(e) Pingamizi dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:

(i)  Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi.
(ii) Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.
(iii) Amekuwa akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).
(iv) Mwaka 2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.
(v) Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.
(vi) Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.

Ndg. Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).

(f) Pingamizi dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:

(i) Alivunja Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia  maagizo ya FIFA na CAF
(ii) Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
(iii) Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.


Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.

(g)Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na  Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:

(i) Ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.
(ii) Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.
(iii) Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.
(iv) Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.

Ndg. Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.



Angetile Osiah
KATIBU
KAMATI YA UCHAGUZI


SHABIKI WA MAN U ALIVYOKOJOLEA GARI LA MARIO BALOTELLI

10:56:00 PM Add Comment
 Jamaa akiruka na kuimba juu ya Gari la Mario Balotelli alilokwa amelipaki pembeni

 Khaaaa....kudaadeki...si akaamua kulikojolea sasa

Mario Balotteli akipaki Gari lake

 SHABIKI NA MPENZI wa Clab ya Uingereza "Mashetani wekundu" Machester United (MAN U), ametoa kali ya Mwaka baada ya Kulikojolea Gari la Mchezaji wa MAN CITY, Mario Balotelli

 Jamaa huyo alifanya kituko hicho katika gari hilo aina ya Bentley Amid Rumours lenye thamani ya EURO 160,000 na kisha kushusha Suruali yake huku makalio yake yakiwa nje, na kupanda juu ya gari upande wa Kioo cha Nyuma, huku akipiga kelele za kutokumkumbuka Striker huyo hata kama ataondoka kwenda AC Milan.

Tukio hilo limetokea nje ya Mgahawa wa Indian, katika Mji wa Manchester, wakati Balotelli alipokuwa akipata chakula na Rafiki zake



CONFIRMED. RICK ROZAY APATA AJALI AKIJARIBU KUMKWEPA MPIGA RISASI

10:20:00 PM Add Comment
 Gari la Rick Ross "rozay likifanyiwa utaratibu wa kuondolewa katika eneo la Tukio, ambako Rozay alipata ajali kumkwepa mtu anayesadikika kuwa anataka kumpiga Risasi

 Rick Ross 



Eneo La Tukio Rick Ross amepata maswahibu hayo
 
Eneo la Tukio likiwa Limezungushiwa Mkanda wa Tahadhari

Kioo ca Jengo ambako Rick Ross amepata mswahibu hayo leo, likionesha Alama ya Risasi iliyokwa inamlenga Rick Ross

Jitihada za Kuliondoa Gari hilo


 Kwa Mujibu wa Jeshi la Polisi, Rapper The Big Baus Rick Ross "Rozay", amerparamia ukuta wa Jengo katika Mtaa wa Ft. Lauderdale maeneo ya Florida Nchini Marekani asubuhi ya leo, na gari lake aina ya Rolls-Royce, akijaribu kumkimbia mtu ambaye alikuwa akilirushia Risasi gari lake

Katika Ajali hiyo ambayo ililkumba gari hilo kali la msanii, Big Baus huyo wa MMG ambaye alikuwa amempakia Msichana aliyetambulika kwa jina la Shateria L. Moragne ambaye ainasadikika kuwa hivi sasa ndo wako katika mahusiano, wote waw3ili hawakuweza kudhurika kwa Risasi pamoja na Ajali hiyo


FACEBOOK WALL YANGU LEO : Lizzle, The African Lady I will always appreciate

6:28:00 AM Add Comment

Nimesoma Naye Ordinaly Level "O- Level" Pale St Anne Marie Academy mpaka 2007 ambapo tulihitimu.

Though nilianza kumzoea hatua za Mwisho, But nilipata kufahamu mambo mengi kupitia yeye, na hatimaye kujifunza Mengi kupitia urafiki wetu. 

Though tumekuwa Marafiki kwa muda wote huo, we never had any conflict kias kwamba najivunia kuishi na watu vizuri, hasa marafiki zangu.

Since 2007, nimekuja kukutana tena na Lilian Lucian Kikoti "Lizzle" mwaka 2012, wakati nipo katika hatua za mwisho kuhitimu Taaluma yangu ya Habari.

I miss Her, and I love her coz she do the same to me too as Her Friend and Old School Mate.

HAPA HUNIDHURUMU KITU....

12:09:00 AM Add Comment
Kazi na Dawa Bhana...Eti nani alisema hata sisi wauza Samaki wa Uswazz hatuwezi kumiliki ma-Touch ya Kishua kama hayo?

Sasa kwa taarifa yenu, Mizigo hiyo inaweza kumilikiwa hata na "MAKABWELA" kama sisi bhana.

Nyie kama mnajipa ma-Flag kwa kuyamiliki au kuyatumia mkiwa kwenye magari yenu hasa mbele za Masista Duu, basi kimpango wenu

Sisi wengine tunazitumia "Ifektivule" hasa katika Biznes kama hivi. Hapa kama kawa, nawatonya wadau Mzigo Mpya nilioshusha, Nachat Facebook na Twitter kama kawa, pia kama ukija na 10,000/=, unataka Fish wa 470/=, napiga Kalikuleisheni kama kawa...Haina kumbwanda hapa...haumbuki mtu, wala hatoi boko Mtu hapa.

ISABELA DOS SANTOS : MTOTO WA RAIS WA ANGOLA< ANAYEONGOZA KWA UTAJIRI BARANI AFRIKA

11:56:00 PM Add Comment
IKO HIVI...
ISABELA DOS SANTOS kifungua Mimba wa Rais wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, ndiye Billionea wa Kwanza Barani Africa, yaani hakuna Tajiri mwingine katika Nchi yoyote ile Africa anamshusha bi Mdada huyu kwa kuwa na Mkwanja Mrefu




Hiyo inatokana na Jarida la Kiuchunguzi la Forbes, ambapo inasemekana kuwa, Mrembo huyo amekuwa akinunua hisa mbali mbali katika Mkampuni mbali mbali Nchini Portugal, ukijumuisha Hisa za BENKI na CABLE TV COMPANY. Kwa kujumisha hayo, inaonesha dhahiri kuwa , Mrimbwende huyo anaweza kumiliki Benki Moja Nchini Angola.





WABUNGE WAANGUA VILIO

11:24:00 PM Add Comment


WABUNGE waliochomewa nyumba na mali zao katika vurugu zilizotokea Mtwara juzi; Anna Abdallah na Mariam Kasembe, jana waliangulia vilio walipotakiwa  kuzungumzia tukio hilo.
Nyumba za wabunge hao wa Viti Maalumu na mali zingine kadhaa za taasisi mbalimbali, ni miongoni mwa vitu vilivyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo pia zilisababisha vifo vya watu wanne wilayani Masasi.
Akizungumza kwa huzuni,  Anna alisema hajui sababu za uharibifu huo, hasa ikizingatiwa mwenyewe amekuwa huko kwa karibu siku tatu na hakuona dalili za uhasama wowote dhidi yake.
Anna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho alisema: “Nina siku ya tatu hapa Masasi na nimeshiriki mkutano wa halmashauri kwa mwaliko na wakati wote, sikuhisi chochote hivyo siwezi kujua sababu ya chuki iliyofanya nyumba yangu ichomwe moto,” alisema.
Alipotakiwa aeleze hali ilivyokuwa, alisema, “Wavamizi hao walipora kila kitu nyumbani kwangu yakiwamo mapazia, kabla ya kumwaga petroli kila chumba na kuwasha moto.”

Aliendelea kueleza,” Kila kitu kiliteketea. Inatia uchungu kwani nyumba hiyo niliijenga kwa kudunduliza fedha kidogo kidogo nikiwa mkuu wa mkoa.”
Anna alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.


“Hali si nzuri. Kila kitu kimeibwa na nyumba imechomwa moto, hakuna kilichobaki. Walichukua kila kitu na itanichukua muda mwingi kujua thamani halisi ya hasara iliyopatikana,” alisema.
Kauli ya Kasembe
Naye Kasembe alipokea simu ya mwandishi wa habari hii kwa kilio na kuikata huku akisema, “Jamani niacheni… Mwenzenu naumia…!”
Alipopigiwa tena baadaye, alisema anashangazwa na tukio hilo ambalo limemfika bila kutarajia na kumtia hasara kubwa.
“Wamepora kila kitu katika nyumba na kuichoma moto, sijui atakuwa nani huyu, kwani sina tatizo na wapiga kura wangu na sina mgogoro na mtu yeyote. Nashindwa hata kuhisi nani kafanya uchochezi,” alisema Kasembe.

Alisema wakati wa vurugu hizo, ndugu zake akiwamo mama yake, walikimbia na kwenda kujihifadhi hotelini, lakini mpaka sasa hawajui wataishi vipi baada ya nyumba hiyo kuteketezwa kwa moto.
“Jana wanafamilia walilala hotelini na leo tupo nje ya gofu la nyumba yangu ambayo imeteketea kabisa kwa moto, tunasubiri majaaliwa mengine, lakini nimechanganyikiwa kwa kweli na sijui ni kitu gani hiki, siamini,”alisema.
Polisi waeleza uharibifu
Watu 44 wanashikiliwa na polisi wilayani Masasi kufuatia vurugu hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Mtwara, Maria Mzuki alisema watu hao wamekamatwa kwa wakituhumiwa kujihusisha na vurugu hizo zilizosababisha uhalibifu mkubwa mali.
CHANZO : MWANANCHI

MAANDAMANO NCHINI MISRI JANA YALIKUWA KATIKA STAILI HII

11:07:00 PM Add Comment
 Mmoja wa wa Vijana walioandamana jan Nchini Misri akiwa katika Style kai ya Kuandamana, huku akionekana kurusha Jiwe, na Suruali ikiwa chini...

Waandamanaji wakipambana na Jeshi la Polisi

KUTOKA KENYA

11:02:00 PM Add Comment

Tume huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka IEBC Jumapili imetoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa vyeti bandia ambavyo inadai vimekuwa vikisambazwa jijini Nairobi na vinadaiwa kutolewa na tume hiyo.

Kulingana na IEBC vyeti vitatolewa na IEBC baada ya vyama kuwasilisha vyeti vya uteuzi, na wagombezi wa viti mbalimbali. IEBC inatarajiwa kutoa vyeti kwa wagombezi wa urais tarehe 29 na 30. 

Watakaowania nyadhfa za ugavana, useneta na wawakilishi wa wanawake katika kaunti na wengine watawasilisha karatasi zao za uteuzi tarehe 31. IEBC imebaini kwamba vyeti hivyo bandia ambvyo vinasambazwa vina maelezo bandia ikiwemo sahihi ya mwenyekiti wa IEBC Isaac Hassan na baadhi ya wakuu wengine.

Tayari IEBC imewaarifu maafisa husika wa usalama na mshukiwa mmoja ametiwa mbaroni.

PICHA : MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA CHUO CHA ST. JOHNS (ST. JOHNS UNIVERSITY) DODOMA HAPO JANA

12:14:00 AM Add Comment
 Wanafunzi wa Chuo cha ST.JOHNS Kampasi ya Dodoma, wakiwa katika Maandamano kupinga matukio ya uharifu yanayofanywa na baadhi ya vijana Mkoani humo, na kusababisha kifo cha mwanafunzi mwenzao baada ya kubakwa na kuliwa na Fisi....






PICHA ZOTE NA MJENGWA

TUMESEMA HIVI ...TUTAIHAMISHA DAR LIVE TOKA MBAGALA, KUJA BONGO MUVI

12:05:00 AM Add Comment
 Rais wa Shirikisho la Filamu Nchin, TAFF, SIMON MWAKIFAMBA akizungumza na Waandishi wa habari (Hawapo katika Picha), kuhusu tamasha lao litakalofanyika DAR LIVE Jumamosi hii

 Msanii wa Filamu Nchini, Kulwa "Dude" akichangia Jambo


Baadhi ya Wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria katika kikao chao na Wanahabari (hawapo Pichani)
katika viwanja vya Leadres Club, jijin DSM

PICHA ZOTE KWA HISAN YA MUSA MATEJA

MBUNGE W#A SINGIDA ATOA ZAWADI KATIKA JIMBO LAKE

11:40:00 PM Add Comment
 
 


Na Nathaniel Limu.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa pea za vitenge 7,500 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.

Mh. Dewji ametoa msaada huo mkubwa na wa aina yake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na Katibu wa CCM manispaa ya Singida.

Msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi, amesema jumla ya vikundi vya uhamasihaji 112, vimenufaika na msaada huo wa vitenge.

Amesema  pamoja na vikundi hivyo, pia wajumbe wa halmashauri kuu ya matawi, wafanyabiashara wa kuku za kienyeji soko kuu, boda boda na taasisi mbali mbali, watanufaika na msaada huo.
Msaidizi huyo wa mbunge, amesema kwa hali hiyo, sherehe hii muhimu, ni lazima nayo ipewe heshima ya aina yake ikiwemo wana- CCM na wapenzi wake, waonekane tofauti siku hiyo ya sherehe.

Katika hatua nyingine, Katibu tawi la Ughaugha (CCM), Hamisi Ramadhani, amesema msaada huo wa vitenge, ni mwendelezo wa misaada mingi ya kimaendeleo anayotoa mbunge Dewji, jimboni kwake.
“Kwa kweli mimi binafsi nakiri tu kwamba Dewji anafanya mambo makubwa sana jimboni kwake.  Hivi karibuni ametoa majembe mengi ya kukokotwa na ng’ombe pamoja na tani nyingi za mbegu ya mbaazi, dengu na choroko”,amesema.

Ramadhani amesema msaada huo ambao utamgharimu Dewji zaidi ya shilingi 250 milioni, unalenga kuwanufaisha wakulima watakaojiunga kwenye vikundi kujikomboa kiuchumi.
“Kwa sasa baadhi ya wakazi wa jimbo la Singida mjini wanakabiliwa na upungufu wa chakula.  Hivyo naomba nitumie nafasi hii kumwomba mbunge wetu Dewji asichoke, atusaidie chakula ili tuweze kunusurika na atharii za njaa”,amesema.

Kuhusu msaada wa vitenge, Hamisi amesema msaada huo hauna kabisa harufu ya rushwa, kwa madai kwamba hauna mambo ya kona kona wala kificho.
Naye mhasibu wa kikundi cha kijiji cha Misake, Mwajabu Haji, amesema msaada wa sare hizo, utachochea ari ya kikundi kuongeza bidii katika jukumu lao la uhamasishaji.

GOOD MORNING...

11:25:00 PM Add Comment
Nilikuwa nadhani Mishe kama hizi zipo Bongo tu....kumbe hata Mbele?...Habari za Asubuhi Wapendwa. Ingawa ni siku ya Siku kuu ya MAULID, ndo kwanza kijana wenu nipo ofisini, si unajua tena kazi zetu?

MNADA BANNER