REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KIMENUKA !!! : BABA MZAZI WA BEYONCE AKUTANA NA HILI BAADA YA KUTANGAZA KUZLIWA KWA MAPACHA , KABLA YA BEYONCE !!!

3:24:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Kuna fununu kuwa Mzee Mathew Knowles, ambaye ni Baba Mzazi wa Beyonce, alikutana na Kichambo cha Hali ya Juu baada ya kutangaza Kuwa "Mapacha Wa Beyonce" wameshazaliwa, kabla Hata Mlengwa Mwenyewe hajafanya Hivyo

Kwa Mujibu wa Info ambazo tuko nazo mpaka Hivi sasa, Ni kwamba kumetokea na Mgogoro Mkubwa baina ya Baba Huyo wa Beyonce na Mashabiki wa Beyonce ama "TEAM BOYONCE" kwa Madai kuwa Kwanini amefanya hivyo kabla Beyonce hajatangaza

"Mbwadidi" hilo lilianzia Twitter ambapo Wengi walianza Kumchamba Mzee huyo huku wakimuita kuwa ni "Baba Kihele hele" na ana Kisebengo cha kutoa taarifa wakati wengine bado hawajatoa wakati ndio walengwa husika

MAJIBU: "SIKUONA TATIZO KATIKA PICHA, ILA NIMEJIFUNZA KITU KATIKA PICHA HIYO YENYE RANGI NYEUSI"- KIM KARDASHIAN

2:01:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
#WatuWaMungu Hatimaye KIM KARDASHIAN ameamua kujibu Tuhuma ambazo zilikuwa zikimuandama kuhusu Vipodozi vyake kuibadilisha Ngozi yake Nyeupe kuwa Nyeusi katika Tangazo la Promotion ya Bidhaa Hizo

Kama Utakuwa ni Mfuatiliaji Mzuri sana wa Kitu Hii, Weekend iliyokata , Kim Kardashian alikutana na "Ndimu" za kutosha toka kwa Mashabiki wake, baada ya kuachia Tangazo la Vipondozi vyake vya KKW BEAUTY LINE ambalo lilionekana kumbadilisha Ngozi, yaani kutoka kwenye Weupe na kuwa na LIGHT BLACK
Wengi wao walikuwa ni wale ambao wana Ngozi Nyeupe huku wakimtuhumu kuwa ameanza kuutukuza Uafrika na kuuacha Uzungu wake, kitu ambacho kilimfanya Mke huyo wa Kanye West afanye mabadiliko ya Fasta sana katika Tangazo hilo

Katika Kufafanua Zaidi, Kim Kardashian alijibu Hivi

"Sipendi Kumkwaza Mtu yeyote. Nilimtumia Mpiga Picha Mzuri sana na Timu kubwa ya Watu katika zoezi hili. Nilikuwa na Ngozi ya Manjano mchanganyiko na Brown wakati napiga Picha, ila nahisi Mwanga haukuwa wa kutosha wakati tunapiga Picha. Lakini, niliwaonesha Picha watu wengi tu katika Biashara. hakuna aliyekosoa na hata kulizungumzia Tatizo hilo. Hata Hivyo, nina Heshima kubwa sana kwa watu wangu ingawa najua kuna wengine watajihisi vibaya. Tulifanya Mabadiliko yanayowezekana kuibadili hiyo picha na Nyinginezo. Tuliona Tatizo liko wapi, na tukafanya Mabadiliko haraka  iwezekanavyo. Kiukweli, nimejifunza kupitia Hili "


DJ KHALED: WAMENIFANYIA UJINGA HUU STEJINI

1:36:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu DJ KHALED alijikuta akikutana na "BOOOOOOO" za kumimina katika Tamasha la ELECTRIC DAISY (Electric Daisy Carnival) ambalo lilifanyika Jumapili ya Weekend Iliyopita

tukio hilo lilitokea kwa Muda kadhaa baada ya Kubainika kuwa Sound haikuwa imekaa sawa na ilikuwa kama Inasumbua kwa Upande wake, kitu ambacho kilionekana kuwaboa sana Nyomi la Mashabiki ambao walikuwa wametia Timu kuja Kumsupport

Lakini Baada ya kutokea Balaa Hilo, DJ Khaled alijitokeza na kuweka wazi kuwa kulikuwa na Matatizo ya Sound , ambayo inaonekana kufanywa na Waandaaji wa Tamasha Hilo

Katika hatua Nyingine, Khaled anadai kuwa, walimfanyia "Kitu Mbaya" kwenye Sound yake
Kupitia Instagram account yake, DJ Khaled aliandika hivi

" Walijaribu kuvuruga Sound Yangu Mara Nyingi. hawakuweza kuiweka Sound ikae sawa kwa Upande wangu, lakini bado nilisimama jukwaani bila sound yoyote. Lakini walipoiweka sawa, bado walijitahidi kuminya baadhi ya Vitu vyangu ila bado niliwakilisha watu wangu. Mtu yeyote angeondoka Stejini. Nilifahamu kuwa mashabiki wangu wa Califonia na Vegas walikuwepo. HAWATAKI SIE TUSHINDE, ila Tunashinda zaidi."

Tofauti na hilo, Khaleed alifichua Jambo lingine kwa Kuandika Hivi
" Walikula Muda Wangu na kuufupisha Kabisa wakati wakiniweka Nyuma ya Jukwaa kwa kama Saa moja na Nusu. Sound bado ilikuwa inazingua... lakini ghaf;la nikawasikia mashabiki wangu  wakilalamika, nikawaambia, niotaenda jukwaani hata kama mmeminya muda wangu... Niko hapa kwa ajili ya Mashabiki wangu hata kama Mtu wa Sound na Promoter hawajaweka vitu sawa. Ninawasamehe.. MASHABIKI WANGU WAKITOKEA, NA MIE NINATOKEA, HATA IWE NINI"

MNADA BANNER