REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HONGERA : MR & MRS NAHEKA (KHATIM NAHEKA & GENOVERA MWAKALEBE)

1:36:00 AM Add Comment

 ROYAL COLLEGE OF TANZANIA (RCT) Ndipo Mahali ambapo palinikutanisha Mie Pamoja na MR & MRS NAHEKA.

Khatim alikuwa ni Class mate Wangu (Swahiba na Best Friend kabisa) Huku Genovera akiwa ni Moja kati ya College Mate Wangu (Na Nilikuwa Program Manager wake)

Ninafarijika sana kuona Ndugu zangu ambao hata hakuna aliyetaraji kama wangefikia hatua Hii, wakitimiza Agano la Mungu , na kujenga familia pamoja.

Nisamehe Khatim, Ulinipatia Mwaliko na kunisihi Nihudhurie “Jembe Langu” katika Pilau lako, lakini Bahati mbaya Tulipoteza mawasiliano, na majukumu yalinibana.

Kupitia Black Touchez, nachukua nafasi Hii Kukupongezeni kwa hatua Hii maalum.

Ni Surprise Kiujumla, ila Ninajivunia kuona Chuo kinaweza kuunganisha Mpaka Ndoa.

Ninaamini Pia Classmates Wenzangu Wengi watakuwa Suprised Kukutana na Kitu Hiki maana umefanya jambo la Busara sana kumuona Genovera, ambaye alikuwa Ni Binti wa Pekee sana katika Chuo Kizima

Khatim, DIPLOMA MAY 2010, unaungana na SAFIA MOHAMED "Safmuu-Mtoto Wa Kocha" ambaye Pia ameingia katika Ndoa, na Nilipata Mualiko Pia, ila Nikashindwa Kuingia Zanzibar.

Ninajivunia kuwa na Ndugu ambao kila siku, tunakua, na kupiga hatua zenye Mafanikio na Heshima zaidi. Am Proud Of U Guys, and I Real Miss You all

NINAWATAKIA MAFANIKIO MEMA NA FAMILIA BORA. ALLAH (S.W) AWATANGULIE

Frank M. Joachim-Baba Juti
CONTENT MANAGER

BLACK TOUCHEZ & SASA BASI ENTERTAINMENT

#WasaniiNaSiasa: HUYU NDIYE MBABE WA WASTARA JUMA

1:04:00 AM Add Comment

Na BABA JUTI
KWA upande wake Mke wa Marehemu Juma Sajuki Kilowoko, WASTARA Juma, naye aliweza kumpongeza Mbabe wake katika Kinyang’anyiro Hicho cha VITI MAALUM kuwakilisha Mkoan Wa Morogoro.

WASTARA alithibitisha Kuangushwa na Bibi Mkanga katika Kinyang’anyiro hicho na Kupiga hatua ya kuchungulia kunakom Level za Taifa kwa safari ya Pili


 WASTARA ALIANDIKA HIVI


Mh mama mkanga nakupongeza kuludi tena ulingoni nakutakia mafanikio dodoma
Kikubwa umeteuliwa kwa ajili ya walemavu pigana kwa ajili yao sikiliza shida zao futa machozi yao na waombee wapate wanachokitaka kupitia uongozi wako kiongozi bora ni yule anaesikiliza wahitaji wake walikupigania uwe kiongozi wao
Tumia vizuri uongozi wako ili walemavu wasilalamike mungu akutangulie..

BAADA YA KUSHINDWA KATIKA VITI MAALUM: "NINAWASHUKURU WOTE MLIONIPINGA MAANA MMENIONGEZEA UJASIRI"-WEMA SEPETU

1:01:00 AM Add Comment

Na BABA JUTI
SAFARI Ya WEMA ISACK SEPETU Katika Kinyang’anyiro cha Ubunge wa Viti Maalum kwa ajili kuingia katika Crib la Mwaka Ujao, imefikia tamati siku ya Jana baada ya kushindwa kufua dafu mbele ya Baadhi ya wagombea wenzake

Wema Sepetu alikuwa anagombea kunako Mkoa wa Singida 

Kupitia account yake ya Instagram, Wema hakushindwa “Kudofyoa” yale ya Moyoni kuhusu Kushindwa Kwake. Wema alisema Hivi:


Nilivyo amua kugombea viti maalum, nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa, ila dunia bado inazunguka. Nawapongeza walioshinda. Nawashukuru mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo.

Nawashukuru pia wote mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu upya. 2015 ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa vijana Tanzania. Bigger things loading...

#UchaguziMkuu2015: KEISHA HUYOOOOOOO: HATIMAYE AMETOBOA

12:52:00 AM Add Comment

Na BABA JUTI 
MSANII ambaye Mpaka hivi sasa maethibitisha Kutoboa katika Yepi la Kinyang’anyiro cha Viti Maalum , Ni Mwanamama KEISHA, ambaye ataungana na wagombea Wengine kuelekea kunako NGAZI YA TAIFA.

KEISHA amewashukuru watanzania Kwa Dua zao, huku akiwasihi Kuzidi kumuunga Mkono ili aweze kuingia katika "Crib La Bunge na kuwakilisha kile ambacho anaamini kinastahili Kuwakilishwa.

“Mama wawili” aliandika Hivi Mapema leo katika Account yake ya Instagram


Hawa ni baadhi ya washindi wa leo namshukuru sana mwenyezimungu kwa hatua hii ahsanteni sana kwa dua zenu nimepita

MNADA BANNER