REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

• BAADA YA KUPIGWA NA CHIDI BENZI..HUKU AKITUKANWA MATUSI MAKALI NA T.I.D, RAY C SASA ANA HILI LA KUSEMA:

6:34:00 AM Add Comment

SIKU chache zilizopita , TTM tulikupa Mtonyo kuwa Chid alimvamia Mwana mama Rehema Chalamila “Ray C” nyumbani kwake na kuanza kusambaza kifinyo, jambo ambalo lililaaniwa na wadau wengi wamuziki, likiwemo lile la T.I.D kumshushia maneno makali katika mtandao wa Instagram

Sasa kupitia Account yake hiyo hiyo ya Insta, Ray C amepost Picha ya Video Queen aliyehusika katika Video ya ICE CREAM, ya Noorah akiwa na Suma Lee, baada ya kuanza kurudi katika afya yake, kutokana na kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.
Katika kufafanua hisia zake juu ya jitihada za kuwakomboa baadhi ya watu ambao wameathirika na matumizi hayo ya Madawa ya Kulevya, Ray C amemiminika hivi kama tunavyomnukuu

MATUNDA YA RAY C FOUNDATION: tangu foundation yangu ianzishwe, tumeshawasaidia  vijana zaidi ya 40 kutoka kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya, na wote wamerudi katika hali zao za kawaida, wakiwa na afya njema, baada ya kutumia tiba ya METHADONE.
Ninaipenda sana hii kazi yangu, hasa ninapoona wenzangu nao wanaachana na utumiaji wa madawa, na wanabadilika kama huyo hapo (yaani Video Queen Huyo). Nikimuona huwa Mwili unasisimka. Kupitia mimi, wengi watapona. Ray C Foundation (uteja unazuilika na kutibika ! Vijana tuungane kuwatoa wenzetu kwenye janga hili. PAMOJA INAWEZEKANA)”

Alimaliza Ray C, huku Post hiyo ikipata Comments zadi ya 140

RAY C amekuwa na jitihada za dhati katika kuhakikisha Vijana walioathirika na dawa za kulevya wanarejea katika hali zao za kawaida, huku Juhudi zake zikigonga mwamba kwa Wasanii wawili, CHIDI BENZI na T.I.D ambao walimzingua ikiwemo kumtukana na kumpa kipigo

SAD NEWS: BUSTA RHYMES ATHIBITISHA KUTEMANA NA CASH MONEY RECORDS

6:25:00 AM Add Comment

MOJA kati ya vitu ambavyo vimewaacha watu hasa mashabiki wa Busta, ni kauli yake ya kuthibitisha kuwa hivi sasa yeye na CASH MONEY RECORDS, kila mtu kimpango wake.

Akizungumza katika Moja ya interview, Busta “Bussa Bus” himself, amethibitisha kuwa ni kweli ametemana na Record label hiyo, ikiwa ni baada ya kudumu nao kwa muda wa Miaka Minne ambayo hata hivyo haijakamilika.

Akitoa sababu ambayo wengi pia kuna Uwezo ikatushtua, ni kitendo cha kukosekana kwa Ubunifu, jambo ambalo lilikuwa kama Sehemu ya kikwazo hasa kimaelewano

Hata hivyo katika maelezo yake, Busta amedai amepoteza vitu vingi katika Mchakato wa Kurecord ALBAM moja, ambapo anasema amempoteza baba yake katika kurecord Albam, amepoteza Mwanga wa Kristo katika Kurecord Albam, na hata mambo Mengine.

Pia Busta aliongeza ya kuwa, baada ya kuona mambo hayaendi, na hakuna chochote cha maana alichookifanya akiwa na Record Label hiyo, aliamua kumfuata Big bos wa CASH MONEY RECORDS, Bird Man, na Kumwambia kuwa, ni Kweli wamefanya kazi vizuri na anajivunia kuhusu hilo, lakini hivi sasa anahitaji kufanya kazi vile anavyotaka na anavyohisi inakaa sawa kwake


BUSTA alitangazwa kuungana na CASH MONEY RECORDS mwanzoni mwa mwaka 2010, na amefanya nao kazi mpaka hivi sasa

T.I AKANUSHA TUHUMA HIZI ZINAZOMKABILI DHIDI YA RAPPER WA KIKE IGGY AZAELA….

6:20:00 AM Add Comment

Rapper kutoka ATL-Atlanta, Nchini marekani, T.I, amekanusha Vikali tuhuma ambazo watu wamekuwa wakizizusha dhidi yake kuhusu Kumwandikia Lyrics rapper wa kike IGGY AZAELA

Tuhuma hizo zilianza kuzagaa katika mwezi ambao tukio la BET lilifanyika, ikiwa ni baada ya NICKI MINAJ kurusha dongo kuwa, Iggy huenda akawa hana uwezo wa kuandika baadhi ya mistari ambayo tumekuwa tukiiskia kunako Mikwaju yake ikiwemo FANCY ambayo mpaka hivi leo iko katika nafasi ya kwanzo kunako BILLBOARDS 100 CHART.

Kwa mujibu wa maelezo ya T.I, amedai kuwa Bibie huyo kutoka AUSTRALIA na mwenye Miaka 24, ana uwezo mzuri sana hasa kiakili na kufikilia, kiasi kwamba hawezi kuhitaji T.I mwenyewe amchoree Mistari ya kuzungumzia kunako Mkwaju wowote…

Pia T.I ambaye amewahi kuhit na kwaju la TOP BACK na SWING YO RAGS, ameongeza kuwa Iggy ana mawazo yake na Fikra zake timamu, ambazo anajua ni namna gani atawasilisha kwa Ulimwengu ambao anautawala hasa katika Muziki anaoufanya. 

Hivyop asingeweza kila kitu ambacho amekizungumza katika Mikwaju yake.

Hata Hivyo T.I ameongeza kuwa, ingawa ni kweli Wanamuziki wengi hupata Msaada Mkubwa toka kwa Producers wao ikiwemo hata kubadilisha baadhi ya Mistari na kuiweka sawa, na ni jambo la kawaida, lakiniIGGY ni mtu mwingine kabisa, na yuko tofauti katika hilo, hasa uandishi na namna ya kuwasilisha.


MINONG’ONO ya Iggy kuandikiwa Verse imetawala sana katika akili za watu hivi sasa, jambo ambalo hata Boyfriend wake ambaye ni mcheza basket Ball, alisema kuwa, tatizo watu wengi wanamuogopa Bibie huyo, hasa Nicki Minaj, sababu anafanya mambo makubwa sana.

MNADA BANNER