REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SANAIPEI : SITUMII TENA POMBE KALI AINA YA TEQUILA TAFDHARI !! INATOSHA"

8:18:00 AM Add Comment
 
Na Joe Mwangi-KENYA 
SIJUI kama wengine huwa wanachukua uamuzi kama ambao ameuchukua huyu bibie ambaye ana ukongwe wake kutoka Nchini Kenya, SANAIPEI TANDE (Zamani alikuwa anajiita Sana)

Kama hukuwa unajua kuhusu hili, Jana SANAIPE alitimiza Umri wa miaka 33, tukimaanisha kuwa ilikuwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa, na hakuwa nyuma kushare ujumbe mzuri kwa waungwana ambao wanamzunguka na hasa mashabiki wake

Kupitia Instagram account yake, Sanaipei aliomshukuru mwenyezi mungu kwa kufikia hatua Nzuri ya kutimiza miaka hiyo 33 akiwa hai, huku akiahidi kuachana na matumizi ya vitu ambavyo kwa asilimia kubwa vinaweza kumrudisha nyuma

Bibi huyu ambaye aliuvuna umaarufu mkubwa kupitia Kolabo yake na JUA CALI-"Kwa Heri", ametangaza rasmi kuwa hivi sasa hatumii tena pombe kali (Tequila)

Tunamnukuu
 "Ninamshukuru Mungu kwa Miaka yangu 33 Leo. Amekuwa na atazidi kuwa MWAMBA wangu!. sasa, hakuna tena Tequila tafadhari. Nimemaliza"
 

KI-BEN TEN CHA BLAC CHYNA KIMESEMA KUWA HUWA HAWAVAI KONDOM WAKATI WA TENDO LA NDOA..NI MWENDO WA KAVU KAVU !!!

7:47:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
WATU WA MUNGU nina imani tunafahamu kuwa Ex-wa Rapper Tyga, Blac Chynna hivi sasa ana mahusiano Mapya na "ki-ben Ten" chake ikiwa ni baada ya kukumbana na kashfa ya kuvuja kwa Video yake ya Ngono hivi karibuni.


Sasa kama ulikuwa hujafahamu Vizuri, Boyfriend wake huyo anaitwa YBN ALMIGHTY JAY na ana umri wa Miaka 18 ilihali Blac Chyna ana miaka 29 na kwa hali ambavyo inaonesha, bwana mdogo anamiliki mpunga mzuri tu kama sio kutuoneshea kupitia social networks tu.


WIKI hii Bwana Mdogo huyu kaibua siri nyingine kuwa yeye na Blac Chyna Hawatumii Kondom piindi wanapokuwa wanafanya tendo la Ndoa, yaani maana yake ni kwamba huwa wanaenda "Kavu Kavu"

Tunamnukuu
" Huwa ninaenda kavu kavu. Huwa sivai mipira mie rafiki yangu. Nani afanye huo upuuzi?. Nisengefanya mapenzi na mwanamke kama ningekuwa naogopa yeye kupata Mimba"

KILICHOSIKIKA LEO KATIKA INTERVIEW YA MO MUSIC KUHUSU NAMNA AMBAVYO WASANII CHIPUKIZI KUTOKA MWANZA WANAVYORUDISHA TAARIFA TOFAUTI KUTOKA KWAO WANAPOKUTANA NAO, MUZIKI WAKE, MANAGEMENT YAKE MPYA, KUUMIZWA NA MCHUMBA WAKE

7:12:00 AM Add Comment

Na Rich Sam-Mwanza  
Msanii MO MUSIC ambaye hivi sasa anakiri kuwa na Bajaji katika Mikoa karibu yote ya Tanzania (yaani Nyimbo yake ya Bajaji iko Kila mkoa wa Tanzania) Siku ya Leo alipita Unyamwezini katika Studio za JEMBE FM 93.7 MHz-Mwanza, na kukutana na Interview katika kipindi "korofi" cha HIT ZONE

Katika Interview akiwa na Baba Juti pamoja na Natty E, Mo Music alizungumza Mengi hasa akitutambulisha kwenye Management yake Mpya ikiwa ni baada ya ile ya awali kumalizika katika Hali ya Mtafaruku kidogo.


Mo Music awali ameweka wazi kuwa Mwaka huu wa 2018, anatarajia kuachia Audio na Video takribani 8, hivyo mashabiki wake wanatakiwa kukaa tayari kwa ajili ya "mikwaju" heavy itakayofuatia.

Upande Mwingine, Mo Music ameweka wazi kuhusu namna ambavyop wasanii wenzake kutoka jijini Mwanza hasa namna ambavyo huwa wanafikisha taarifa tofauti na kile ambacho wanakikuta kwa wenzao walioko Dar Es Salaamu, kitu ambacho kinaonekana kuwakatisha tamaa kuwasaidia pindi wanapowahitaji

INTERVIEW FULL IKO HAPA

MNADA BANNER