REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WAVUTA SIGARA..WALA HILI LISIWAPITE..

11:25:00 PM Add Comment



Tunajua kabisa Kuwa kuna baadhi ya Watu hawawezi kupata Usingizi kabisa kama hawajachoma Chiga..yaani Sigara..lakini Msijali

Tunaamini kuna Sigara za aina mbali mbali na zenye Ladha Mbali mbali kutoka kwa makambpuni Mbali mbali, lakini hii pia inaweza Kukuhusu.

The man With Mkwanja kwa Kila Sekta, JAY Z hivi sasaanatarajia kuachia Bidhaa yake Mpya Sigara.


Kwa Ushirikiano Mkubwa na kampuni ya COHIBA, JAY Z ambaye ni Mfanya Biashara na Rapper Mkali na Mkongwe Nchini marekani, anatarajia Kuingiza Bidhaa hiyo Sokoni ambayo itatambulika kwa Jina la COMADOR

Kupitia Mitandao Mbali mbali ya Kijamii, JAY Z ameweza kuonesha Sigara Hizo za COMADO ambazo zitakuwa na Ladha Nzuri ya Tumbaku kama kawaida.

Wadau wa Sigara wamesema kuwa, Huenda Sigara hiyo ikaleta kitu Kipya Tofauti na Chenye Mvuto wa Aina yake kwa watumiaji wa Sigara Duniani Kote, na Kuna Uwezekano Biashara Hii ikaleta Ushirikiano Mzuri Wa Kuvuta Pesa Baina ya JAY Z na Mshirika Wake COHIBA RED DOT.

CHEKI PICHA ZA BIDHAA HIYO..





 

UKWELI KUHUSU JUSTIN BIEBER KUSTAAFU MUZIKI....

11:20:00 PM Add Comment



Mi Sidhani kama tulikosea kumuita Justin Bieber “The Majanga Boy”, sababu kila anachokifanya tunahisi na hata kubaini kuwa ni majanga matupu.

Sasa Bwana Mdogo huyu amekuja na Hili Lingine..

Justin Bieber, ambaye Hivi sasa ana Umri wa Miaka 19, na anajihusisha na Muziki wa Pop, alitoa kauli Moja tu ya Kuwa anastaafu Muziki wakati akigonga Interview na Kituo Cha Redio cha POWER 106 Kilichopo Nchini marekani, na hata Kuirudia Tena kauli hiyo wakati anafanya Interview na Kituo cha TV cha E News.

Lakini Kwa Mujibu wa Msemaji wake, Inaswemekana kuwa Sio Kweli, bwana Mdogo Bieber hatoacha Muziki, na Ni Kitu ambacho hakiwezi kutokea.


Pia Mitonyo Imezidi Kuvuja kuwa, huenda siku anatamka Hiyo kauli ya Kustaafu Muziki, alikuwa tayari ameshachoma Mmea Korofi, yaani BANGI, hivyo inawezekana kabisa Ile haikuwa akili yake Muda Ule.

Pia Mitonyo inadai Kuwa, Kabla hajaingia katika Studio za POWER 106 RADIO, Gari la Justin Bieber lilionekana likwasili hapo huku Likitoa Moshi Mkubwa kutoka ndani ya Gari, jambo ambalo linawafanya waamini kuwa, Mkali huyo Mdogo wa Pop, alikuwa anachoma Mmea Korofi.

Pia akiwa katika Studio Hizo, Bieber alitoa Taarifa kwa Media mbali mbali ambazo humuandama mara kadhaa kuwa, wamekuwa wakiamini yeye ni Mkorofi na Mwenye Kiburi, jambo ambalo anadai Si Kweli, kwani anawapenda, na Kuwajali Mashabiki zake.

TUNASHUKURU SANA

9:40:00 AM Add Comment

TUMEFARIJIKA SANA Kushinda nafasi Hii Kwa Mwaka Huu Kutoka kwa Waandaaji wa Shindano la UPCOMING AFRICAN INTERTAINMENT NEW MEDIA, ambao Ni CNMC (The Youth: Canada New Media Commitee).

Mwaka jana Tulikuwa washindi wa Pili katika kipengere hiki Hiki, lakini Tunawashukuru Wasomaji Wetu Nchini Canada kwa Support Mliyoonesha.

Tunawaahidi Kuvuta Tuzo zaidi ya Hii.

JULY JUTI
C.E.O BLACK TOUCHEZ

MKENYA AMFUNIKA OPRAH…NI YULE MKALI WA MUVI..

8:18:00 AM Add Comment



Unaweza kujiuliza maswali Mengi saaana kuwa inakuwajeWakenya wanakua kiuchumi, lakini hata katika Tasnia ya Burudani, jamaa hawalazi damu kama Tanzania?..Lakini ukweli utabaki pale pale, wakenya wanajua umuhimu wa Sanaa kwao

LUPITA NYONG'O, Mwanadada Mkenya anayejishughulisha na Filamu katika Nchi za Wengine, finaly mezidi Kung’ara na kuipatia Heshima Nchi ya Kenya, baada ya Kupata Tuzo nyingine, na kumfanya awe Msanii Bora wa kike Mwenye mafanikio makubwa katika Filamu hasa za Hollywood, akiwa anatokea Afrika Mashariki.


BAADA ya Kuchaguliwa katika Moja ya Kipengere kwenye Tuzo za THE HAUSTON FILM CRITICS SOCIETY (HFCS), hatimaye ameweza kuibuka Mshindi katika Kipengere Hicho cha MHUSIKA MSAIDIZI BORA (Best Supporting Character), katika Filamu ya  12 YEARS A SLAVE


Katika kuandika Sehemu ya Historia, Mkenya huyu ameweza kuwapiga Chini Malkia wa Vipindi Vya TV Duniani, OPRAH WINFREY, Jeniffer Lawrence, Octavia Spencer, na June Squibb

WIMBO MAALUM WA KWA MAREHEMU NELSON MANDELA…UMEFANYA MAKUBWA

8:08:00 AM Add Comment



R.I.P Kwako Mzee wetu NELSON MANDELA “Madiba”. Umetuachia Historia ya Kila aina kila kukicha, linazuka jipya.
Iko Hivi Mazee…

TRACK ya Bure kabisa ambayo ilikuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya Kumbu kumbu ya Mzee Madiba, umetangazwa kuwa Wimbo Uliokuwa Downloaded sana katika matumizi ya Muito wa Simu kwa Mpigiwaji, ikiwa Ni ndani ya siku Moja tu tangia Uachiwe rasmi.

Wimbo Huo ambao Ulipewa Jina la MANDELA (Tribute To Mandela), Uliachiwa rasmi Mnamo December 11,ikiwa ni siku sita tu baada ya Mzee madiba, mpiganiaji wa Uhuru aliyetumikia Miaka 27 Gerezani, kutangazwa kuwa amefariki Dunia.

Msanii ambaye alihusika kutengeneza Track Hiyo, ni Mshkaji anayetoka Nchini Nigeria, HARRY SONG, ambaye Pia aliweza kuzipiku Track nyinginezo Nyingi zilizotolewa Maalum kwa Jili ya Shujaa Huyo, baada ya Kupata zaidi ya DOWNLOADS MILLIONI kwa Siku Moja Tu.

Kwa Mujibu wa Takwimu Zilizotolewa, Mpaka Kufikia Siku ya jana, Track hiyo imeweza Kupata Downloads zaidi ya Milioni Mbili nab ado takwimu zinazidi kumiminika.

WAKENYA NOMA…WAMEMUUMBUA RASMI SENATOR MTATA SONKO

8:06:00 AM Add Comment



Wiki Mbili Zilizopita, Senator Mwenye Majanga Jijini Nairobi,MIKE SONKO,aliweza kupost Picha ambayo ilikuwa Photoshoped,yaani ilitengenezwa, akiwa ameachia Pozi na Marehemu Nelson Madiba Mandela.

Lakini baada ya Kufanya Hivyo, watu walishtushwa na Kitendo ambacho Senator Huyo, na hata kushika Vichwa Vingi vya habari katika Mitandao Mingi na hata media mbali mbali.

Lakini sasa, Wakenya walivyo Nomaa, waliweza kuisaka Orijino ya Picha ya mtu aliyekuwa na Nelson Mandela, na hatimaye Kuipata.

Mtu Ambaye alipiga picha na marehemu Nelson Mandela, alikuwa ni Mwana masumbwi Nguli na hatari Ulimwenguni, Mohammed Ali, alipokwenda kumtembelea Nchini afrika Ya Kusini Miaka Mingi iliyopita, Kabla Umauti haujamkumba Mzee madiba.

Alichokifanya Sonko, ni Kuondoa Kichwa Cha Mohamed Ali aliyekuwa amekumbatiana na Mzee Mandela, na Kuweka Cha Kwake Mwenyewe, jambo ambalo Wengi walidai kuwa alitaka Kujipa Ujiko lakini Finaly Amegonga Mwamba.

ONA WALICHOKIFANYA










 

MNADA BANNER