REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SHIKILIA HAPO HAPOOO !!!!! : LICHA YA KUCHEPUKA KWA RAPPER T.I, MKE WAKE HATOMUACHA NG'O !!!!

2:34:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu tunaomba "Mshikilie Hapo Hapooooo "
Kama wewe umeamua kukata tamaa juu ya yule uliye naye kisa amekusaliti, basi unaweza kujikuta unakata tamaa katika kila kitu ambacho kitakuzingua hapo Mbeleni

Wiki Kadhaa zilizopita, Ilikuja kuvuja kuwa Rapper T.I ameonekana akimshika "Tamnye" mmoja kati ya mabinti ambaye anasadikiwa "kutinduana naye kiwizi wizi" walipokuwa Back Stage, hali iliyozua utata katika Ndoa yake na Mke wake wa Muda Mrefu sana, Tameka a.k.a TINY.

Pia baada ya hilo "Ngenje (Noma)" kuchukua nafasi kubwa sana na kuzagaa kunako Mitaa ya Social Networks, ilikuja kubainika kuwa Tiny amechukia haswa na hata kushea kunako Account yake ya Instagram Clip ya Snoop Dog Doggy akizungumzia namna ambavyo mwanaume anatakiwa kumheshimu mkewe, dongo ambalo lilielekezwa moja kwa moja kwa T.I.

Sasa, baada ya mengi kuzungumzwa, haya na yale kusemwa, hiki na kile kutabiliwa, hili na lile kuchambuliwa, hatimaye Mke wa ndoa kasema kuwa, HABANDUKI, HALEGEZI , HACHOMOI na wala HAACHII kwa Rapper Huyo.

Kupitia Instagram Story yake, Tinny amedai kuwa ataendelea "kushikilia" kama kote katika ndoa yake licha ya kwamba mumewe ni mchepukaji kimtindo

Nanukuu
"Unapotaka kukata tamaa (Katika Ndoto zako, kipaji chako, Ndoa yako, watoto, familia, Kazi, Mungu, Ukristo, katika dhamira yako ama kila kitu unachotaka kukatia tamaa) kumbuka na kwanini ulikianza"

NGOJA KWANZA !!!!! : KUMBE EX MANAGER WA CARD B NDIYE ALIYEMTAFUTIA MENO MAPYA NA KUMFUNGULIA ACCOUNT YA KWANZA YA BANK?..SHABAAAAASH !!!!

2:21:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi 
KABLA ya Yote, "Mzinga Wa Heshima" kwa the baddest Female Rapper Card B kwa Kupata mtoto wa Kike mwenye afya ya kutosha.

Lakini Waungwana bwana, Hata kama Umepata Furaha ya kupongezwa na Mamilioni ya watu, bado kama tunakudai chetu, tutaendelea kukudai tu Mtu wa Mungu.

Kama utakuwa unakumbuka Vizuri, Tuliwahi kuwahabarisha kabisa kuwa Rapper huyo wa kike na Manager wake wa awali walifikishana mahakamani kwa madai kuwa Card B anatakiwa kumlipa kiasi fulani cha fedha kutokana na kuwa yeye ndiye alimpatia Umaarufu na kumsaidia katika mambo mengi kama yote

Sasa Ex- Manager huyo , Klenord “Shaft” Raphael ambaye amefungua mashtaka ya kulipwa USD Milioni 10 na Rapper huyo , amedai kuwa yeye ndiye aliyemtengenezea Card B Meno na kuwa na muonekano mzuri tofauti na yale ya awali yaliyokuwa yakimpa tabu kuongea fresh na hata kuwa na muonekano Mzuri.

Ukiachilia mbali Madai hayo, Pia Manager huyo wa zamani, amedai kuwa, yeye ndiye aliyemfungulia account ya kwanza kabisa ya Bank hit Maker huyo wa BE CAREFUL na hata kumtafutia mjengo wa kwanza kwa yeye kuishi


KIMENUKA !!!!! : KILICHOTOKEA KATIKA UGOMVI WA RIHANNA NA BOYFRIEND WAKE BILIONEA....

2:08:00 AM Add Comment

Na Rich Sam....     
#WatuWaMungu Shabaaaaaaaaaaaaaaash
Kila Kitu huwa kinaenda Vizuri lakini kama ikitokea Dosari katika safari yake, lazima mambo yawe Magumu kidogo, na hii ndiyo tafsiri ya kile kilichotokea Hivi Karibuni

Taarifa za Umbea ambazo wengi hatukuzitilia maanani, zilikuwa ni zile ambazo zilifumuka kuwa hatimaye Mahaba yaliyotishia Dunia, kati ya mamito Robbin Fenty-RIHANNA na Boyfriend wake mwenye Mkwanja Mrefu sana, Hassan Jameel, yamefikia mwisho !!

lakini baadae taarifa Nyingine zikaibuka kuwa wawili hao hawajapigana Chini hata kidogo na mahaba still yapo, lakini kuna jambo ambalo si sawa baina yao kiasi kwamba kichambo kikamuhusu bwana Jameel

Picha ambazo zinaendelea kusambaa kunako kimtaa ya Social Networks, ni kwamba kulikuwa na "Msuguano Heavy" baina ya Wawili hao kutokana na kile kilichoonekana Rihanna kufoka na kumsonta kwa hasira Boyfriend Wake, huku Boyfriend wake akionekana kufafanua jambo, na kisha kuondoka eneo la tukio akiwa ni mwingi wa hasira
A post shared by badgalriri (@badgalriri) on
Sasa, Baada ya kutapakaa kwa Picha Hizo, Rihanna aliamua kuingia kunako Instagram account Yake na kupost picha inayomuonesha SIMBA JIKE akimuungurumia Simba Dume ambaye alionekana kutia Uwoga na kuandika

"Pale unapodhani unajua sana kuhusu Soccer"

Ukiachilia mbali suala hilo, Pia Rihanna alionekana kukwazwa sana na Comments za baadhi ya watu kudai kuwa Rihanna huwachoka mapema ma-ex wake na kuwasumbua na tabia zake kisha huachana nao huku wao wakiishia kuwa na furaha na wanawake wengine

Alipost kitu kilichosomeka hivi:

"Hakuna hata mmoja wa Ma-ex wangu waliooa au kuwa na mahusiano yenye furaha. Hivyo ni salama kusema kuwa SIKUWA TATIZO"

Ukiachilia mbali hayo yote, inasemekana kuwa Ugomvi wa Rihanna na Hassan Jameel ulitokana na baadhi ya vitendo vya Rihanna kuendekeza kukubaliwa katika kila jambo ambalo analifanya, kitu ambacho Hassan Jameel hakufurahishwa nacho

MNADA BANNER