REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ASLAY- FELLA NDIYE MSAADA MKUBWA KWETU KATIKA KUTUANDIKIA NYIMBO KWA ASILIMIA 90

5:57:00 AM Add Comment

Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.

KIONGOZI wa Bendi Hiyo, Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaada mkubwa katika nyimbo zao zote.

“Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies yeye anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno maoja baada ya moja.”  Amesema Asley.

“Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.



HII NDIYO SABABU YA KUTOKUMZINGUA MAMA YAKE NA SYLVESTER "RAMBO" STALONE, ANAYEITWA JACKLINE STALONE

5:51:00 AM Add Comment

















CHRISTINA AGUILERA APATA MTOTO MWINGINE..

5:43:00 AM Add Comment

CHRISTINA AGUIRELA ni Mama wa Mtoto wa Kike 

AGUILERA ambaye ni Mkali wa POP na ameweza kufanya Poa kupitia Mikwaju yake kadhaa ikiwemo 4 MINUTES ambayo amemshirikisha JUSTIN TIMBERLAKE, amefanikiwa kupata mtoto huyo wa Kike, katika Hospitali ya CEDARS-SINAI, huko LOS ANGELS

Ingawa bado hatujapata Jina La Mtoto huyo, lakini tutarajie Mengine mazuri kuhusu mtoto huyo zikiwemo Picha kadhaa, hasa kupitia mtandao wa Tweeter


Huyo anakuwa ni Mtoto wa Pili kwa AGUILERA ambaye amezaa  na Mchumba wake wa sasa, MATT RUTLER, huku mtoto wa kwanza ambaye ni wa Kiume, MAX, akimpata kipindi kile akiwa katika Ndoa yake ya kwanza na JORDAN BRATMAN

SIKU kadhaa zilizopita, CHRISTINA alionesha Ujauzito wake kupitia Picha aliyotweet katika account yake ya Twitter, huku akijivunia kuwa mama mtarajiwa kwa Mara Nyingine

KWA UFUPI: KUNA UWEZEKANO BEYONCE AKAPIGA COLLABORATION NA RIHANNA

5:21:00 AM Add Comment
INFO ambazo zimetufikia BLACK TOUCHEZ ju,apili ya leo, ni kwamba kuna uwezekano Mkubwa Mkali wa R&B , Beyonce, akapiga Track moja na Mkali wa Pop, RIHANNA.

Ingawa taarifa hazijatoka kamili, ila inasemekana kuwa, Beyonce yuko katika Mchakato wa kuhakikisha anakamilisha mazungumzo na Rihanna kuhusu mchakato mzima wa Kupiga “KOLABO” .

Aidha awali, kumekuwa na Tetesi kuwa, Beyonce hapatani na 

Rihanna kutokana na kuhisi kuwa, ameshakunjuka Kiutamu kunako uwanja wa Sita kwa Sita, na Mumewe JAY Z, ambaye hivi sasa wana mtoto mmoja, BLUE INVY

YALIYOJIRI KATIKA SHINDANO LA TMT..YAKO HIVI

5:14:00 AM Add Comment


Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limefikia hatua ya Mwisho kabisa mara baada ya washiriki kumi bora kupatikana katika Show ya Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Alhamisi.

Show hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda Mbili za Tanzania yaani Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika Kinyanganyiro hiko na Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao wameingia hatua ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.

Washiriki waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko ni Mwinshehe Mohamed ambae alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kati ambapo anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati kuondolewa na Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika Fainali hiyo. Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam.

Kanda ya Pwani walichukuliwa washindi watano huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya Washiriki wanne kuondolewa katika kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani, Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati ya washindi watano kutoka kanda ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani katika Fainali kubwa ya Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika Mashariki na Kati la Tanzania Movie Talents (TMT).

Mpaka Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake wote watatu ndio wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi wote kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja na Hatimaye kuanza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Hivi Karibu.

MNADA BANNER