REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

CHRIS BROWN KUFUNGULIA MASHTAKA MREMBO HUYU

7:05:00 AM Add Comment



Baada ya Kutaka Kufungua mashtaka dhidi ya Adui yake Frank Ocean walipozichapa kunako Studio moja Nchini marekani, Breezy ameamua kuchukua Hatua nyingine kumshtaki Shabiki wake wa Kike..

Kama Utakuwa unakumbuka Vizuri, Breezy aliwahi kufunguliwa Mashtaka na Shabiki yake mmoja wa Kike,kwa madai kuwa alimsukuma katika UKUMBI wa HEAT ULTRA LOUNGE, alipokuwa akiondoka akiwa na watu wake wa karibu.

Lakini baada ya uchunguzi wa kina Kufanyika, ikabainika Mwanadada huyo anayefahamika kwa Jina la DEANNA GINES hakusukumwa na Chris katika Eneo la V.I.P alipokuwa amekaa, ila yeye Mwenyewe ndiye alikuwa Mkorofi.

Kwa mujibu wa Mmiliki wa CLUB hiyo, inasemekana kuwa DEANNA mwenye umri wa Miaka 24, alijaribu kupanda Mahali ambako Breezy alikuwa, lakini ilishindikana baada ya Kuzuiwa na Baunsaz waliokuwa wakihakikisha Suala Zima la Ulinzi kwa Breezy Linapatikana.
Lakini baada ya bibie huyo kutolewa mahali hapo na Walinzi hao, Inasemekana alivua “Michuchumio” na kuanza Kuwaponda, yaani kuwarushia.


Kwa mujibu wa mashtaka yaliyofunguliwa awali na Mrembo huyo, Chris Breezy alikuwa anatakiwa kumlipa  Mwanadada huyo Dolar za Kimarekani 25,000 sawa na takribani Shilingi za Kitanzania 37,500,000.

Lakini kwa hivi sasa, Chris Brown ameamua kufungua Kesi ya Kuzalilishwa na Mwanamke huyo, kwani hata hivyo anadai kuwa hawakupata hata nafasi ya kukaribiana kutokana na Ulinzi uliokuwepo, na pia alimuona akitembea  Vizuri Usiku wote ule, jambo ambalo lilimchanganya Breezy kuwa ni Mguu gani uliojeruhiwa

GIRL ON FIRE: CHEKI NYUNDO ZITAKAZOPATIKANA KATIKA ALBAM YA HOT BABE BRITNEY SPEARS

6:58:00 AM Add Comment



Up to This Moment , The Beautiful baby wa RnB na POP Nchini Marekani, BRITNEY SPEARS ameachia Rasmi Mikwaju itakayopatikana katika ALBAMU yake Mpya ya BRITNEY JEAN.

Baada ya kufanya Vema na Mikwaju kama Vile WORK BIT**H na PERFUME ambayo kamshirikisha dada ake JAMIE LYNN, Albam hiyo itaingia Sokoni Mnamo December 2/3, huku ikiwa na Nyundo 14 kama Ifuatavyo

Britney Jean tracklist:
1. Alien
2. Work B***ch
3. Perfume
4. It Should Be Easy (feat. will.i.am)
5. Tik Tik Boom (feat. T.I.)
6. Body Ache
7. Til It's Gone
8. Passenger
9. Chillin' With You (feat. Jamie Lynn)
10. Don't Cry

Deluxe Edition
11. Brightest Morning Star
12. Hold On Tight
13. Now That I Found You
14. Perfume (The Dreaming Mix)

Katika Albamu Hiyo, Britney ameshirikiana na WILL.I AM pamoja na T.I.

STYLE YA AUTO TUNE : T-PAIN ASEMA AMEUBADILISHA ULIMWENGU

6:08:00 AM Add Comment



Oshhhs ! Ula! La! Laaa!

Finaly Brother T Maumivu ameamua kufungua Ukweli kabisa na kusema kuwa hakika Style yake ya AUTOTUNE amini msiamini, imeleta Madailiko kunako Soko la Muziki

Nappy Boy T-Pain himself ameyasema hayo wakati akigonga interview na one of the Media nchini Marekani, na kuongeza kuwa aliweza kuisoma Vizuri Style anayoitumia na namna ya Kutoka nayo, huku akihakikisha anafahamu namna inavyofanya kazi, na Ilianzia wapi.

Pia T-Pain aliongeza kuwa , baada ya kuifahamu vema Teknolojia ya AUTO TUNE na kila kitu chake, alianza rasmi kuitumia na hivi sasa watu wengi wanaitumia kila Kona ya Ulimwengu huu

 Aidha baada ya Kuulizwa kuhusu Style hiyo kutumika kwa wingi Duniani na ukimya alioupiga kwa Muda Mrefu, nappy boy alifafanua kuwa, aliamua kubaki Kimya kwa Miaka kadhaa ili kujiweka sawa tayari kwa kurudi katika Muziki hasa baada ya ALBAM yake ya REVOLVER ya Mwaka 2011 Kutokufanya Vizuri katika Soko.

Tofauti na hapo, pain ameongeza kuwa hivi sasa Wadau wasubiri ujio wake Mpya  ambao utashusha Albamu Mpya kali balaa, hapo mwakani

MMLP2: HAKUNA CHA DRAKE..WALA JUSTINI TIMBERLAKE...NI EMINEM

6:01:00 AM Add Comment



Ladies and Gentlemen, Eminem yuko katika Level Balaa hasa ya Muziki, kiasi kwamba kaweza kuwachafua Vibaya wakali kama Vile Drake na hata Justin Timberlake.

ALBAM yake Mpya ya MARSHA MOTHER LP2-MMLP2, ambayo ilishushwa rasmi kunako Soko la Muziki ulimwenguni Kote Mnamo Novemba 05 Mwaka huu, imeweza kufanya Hili la kufanya na hatimaye kumfanya Eminemu kuonekana Moto wa kuotea Kilo mita 10.


Ikiwa ni Ndani ya Wiki Moja Tu tangia iingie Sokoni, Jumla ya nakala 779,577 zimenunuliwa, na hatimaye kumchapa Fimbo Mkali Drake, ambaye Albamu yake ya NOTHING WAS THE SAME iliweza kununuliwa kwa nakala 658,000 ndani ya Wiki ya Kwanza

Tofauti na hapo, Eminem ameweza kumcharaza gape Mkali mwenzake JUSTIN TIMBERLAKE, ambaye albam yake ya THE 20/20 EXPERIENCE iliuza nakala 968,000


MMLP2 ya Eminem imekuwa ni albamu ambayo imeonekana kuwa ngumu hasa katika mashairi yake na hata baadhi ya Tracks, wakati Mkwaju wa Rap God ukiingia kunako changamoto tofauti toka kwa wasanii ambao wanachipukia na hata Kutawala Music Industry Nchini marekani

Eminem pia aliweza kupata Tuzo za YOUTUBE ambako alipewa heshima yake ya MSANII BORA WA MWAKA.
EMINEM is on Fire Fellaz

MNADA BANNER