REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HII NDIO NYABEHU, JINA TULILOLIGEUZA KINYWAJI

2:59:00 AM Add Comment

NYABEHU ni Moja kati ya Maeneo Madogo yanayopatikana katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Musoma, Kanda ya Ziwa Victoria.

Eneo Hili lipo Kilomita Chache sana Kutoka BUNDA MJINI
Nilipata Bahati ya Kufika hapa na Timu Nzima ya Metro Fm 99.4 Mhz-Mwanza, wakati tunasafirisha Mwili wa Kaka Yetu Mpendwa, MAREHEMU ALEX MASATU “DJ ALEX DA WOLF” (R.I.P)

Katika Eneo La Nyabehu, tulivutiwa na Madhari ambayo imetawaliwa na Mashamba kadhaa ya Mahindi, na Hata Mpunga, Huku Rangi ya Kijani, ikipamba Ardhi na kuonekana kama ardhi Yenye Rutuba haswa.


Nilimuuliza Sefroza Joseph, maana ya Neno Nyabehu, na aliniambia kuwa, NYABEHU inamaanisha UWOGA/HOFU, Ingawa Mie na Wenzangu Tulitumia Jina hilo kama Kilevi



NYOTA NDOGO YUKO NJIANI NA MAPANYA.

2:31:00 AM Add Comment

BAADAA kuingia katika Mbwadidi na Msanii Mwenzake Nchini Kenya, COLONEL MUSTAPHA kuhusu Picha za Utupu, Mamii ambaye SAUTI yake kitambo sana Haijasikika, hatimaye anakuja na Brand New Swaggalinyuz ambazo ni Video na Audio , vikipewa Jina la MAPANYA, TTM tumezinasa.

Kwa Mujibu wa Info za Uhakika, Ni kwamba Nyota Ndogo ambaye Miaka ya Nyuma alisumbua sana Vichwa vya Watu na Track yake ya WATU NA VIATU, mchakato wa Awali ambao ataufanya, ni Kuachia Video ya Track Hiyo Mpya inayofahamika kwa Jina la MAPANYA, ambayo imemshirikisha jaama mmoja anayefanya Po asana Kunako HIPHOP Nchini Kenya, KAA LA MOTO.

Aidha Nyota Ndogo ameendelea Kufafanua kuwa, Kwaju hilo ambalo limepikwa kuna studio za A MILLION RECORDS-Kenya, linazungumzia Marafiki FEKI ambao wanakuwa Happy na Wewe hasa katika Kampani yako, wakati mambo ni mazuri, ila yakiwa Mabaya, kila Mtu anachukua Time yake na kukuacha uki-hang.


Pia Nyota Ndogo ameongeza kuwa, Kwaju hilo lipo katika Mahdahi ya Kiafrika, huku kukiwa na Combination ya Style ya TAARAB na LINGALA, huku rap Ikichukua nafasi yake kutoka kwa Rappa KAA LA MOTO..

DAVIDO NI MUBAYA…PLATNUMZ ATASUBIRI TU…..

2:24:00 AM Add Comment

Kibongo Bongo ukiambiwa kutaja moja kati ya Wasanii ambao wanalipwa Mkwanja Mrefu sana katika Shows, tunaamini DIAMOND ndiye atakuwa wa kwanza kutajwa , na TTM tunaamini Hivyo

Lakini Baada ya Weekend Nzito kumalizika, Finally KITENGO CHIMBUA CHIMBUA imeshusha Ripoti kuwa Msanii Davido Kutoka Nchini NIGERIA, ni habari Nyingine katika Gharama za Kupiga Show sehemu yoyote Ile, hata Tukiizungumzia Tanzania.

Baada ya Kudaka Mtonyo kuwa, Davido alidai kuwa gharama za kupiga Show katika Jiji la Nairobi ni Zaidi ya Shilingi Milioni 4 za Kenya, TTM tulizama kunako Calculator zetu na Kubaini kuwa, kama Mkali huyo wa Skelewu ataamua kushusha Show Nchini Tanzania katika Ukumbi wowote, Basi Promota atatakiwa Kusalimisha Zaidi ya MILIONI 72 za Kibongo.

Kwa Mujibu wa Takwimu Hizo, TTM tulikaa na Kutathmin  Msanii ambaye ni Talk of The Country kwa Kupiga Show kwa Gharama Kubwa, DIAMOND, na kubaini kuwa anafunikwa Mbaaaaaaaaaaaaaaaali na Jombaa Huyu.

PLATNUMZ akama atahitajika Mfano Nairoi Kupiga Show, basi Promota wa Huko atatakiwa Kushusha Shilingi MILLION 1.6 Za Kenya, sawa na zaidi ya shilingi MILION 18 za Kitanzania.


Baada ya Kupata takwimu Hizo, TTM na Dawati Zima la Nyuma ya Pazia , tulikuja kudiscover kuwa, Kwa System hiyo, Diamond atasubiri sana kwa davido katika Kupiga Show Kwa Gharama Kubwa , pamoja na Mbwadidi la Utajiri…

MNADA BANNER