REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

Sintah Abanwa...akutanishwa Tena na Nature...akana Kuwa na Mtoto. Jini Kabula naye atoa Kali.

4:41:00 PM Add Comment





Sintah "J.Lo"




Sexy Lady Wa Bongo Movie mwenye Vituko kila Kukicha, Sintah Maarufu kama "J.Lo wa Bongo", Ijumaa alikuwa ni Talk of The Town baada ya kufanya yake katika Kipindi Cha Friday Night Live kinachorushwa na Tinga namba Moja kwa Vijana EATV (Channel 5), kinachorushwa na Sam Misago "The Presenters Prezdaa".

Katika hali ambayo ilitufanya wengi tushindwe Kumuelewa Sintah, ni pale tu alipokuwa akionesha dalili za Kuwa alikuwa ameshakung'uta Kilevi cha aina yeyote ile, ambacho kilimfanya aweze kuchangamka kupita maelezo huku akishow swagga za Akina dada waliolewa. Sintah alikuwa katika list ya Wageni ambao walihudhuria katika Club hiyo ya TV.

USO KWA USO NA JUMA KASSIM "NATURE".

Hatimaye baada ya kutupiana Vijembe katika kipindi hichooooo cha Nyuma, Sintah na Juma Nature ambao walikuwa ni wapenzi na wakaachana kwa Bo...bo...Boooonge la Bifu, walikutana tena huku Umma tukiwa tunashuhudia. Tukio hilo wengi tulidhani lingetuonesha Picha Tofauti hasa ukilinganisha na Vile ambavyo tunafahamu yaliyotokea baina ya wawili hao waliokuwa katika "Mahab ya Dhati" na Kuachana ghafla, ambapo Nature alitoa baadhi ya ngoma kama Vile "SITAKI DEMU" na "INANIUMA SANA".

SINTAH AMSHANGILIA NATURE...

Hapo ndipo wengi tulivutiwa na hali halisis iliyotokea. Sintah aliungana na Sam Misago kumkalibisha Juma Nature Studi huku akiimba "Nature..Nature...Nature !!!". 
Juma Nature


Wengi tulidhani Labda Sintah ataondoka, au atakuwa ni mtu aliyenuna mpaka Nature anamaliza Interview, lakini iilikuwa Ni shangwe Matata sana..... Obviously ilikuwa ni Tamu sana kama ulikosa.

NATURE AINGIA NA "MALAPA" (KANDAMBILI) STUDI KUFANYA INTERVIEW.

Jambo lililmuacha kila Mtu Hoi, Ni Kitendo cha Juma Kasim Nature "Kiroboto" kuingia katika Studio za EATV kwenye Kipindi hicho hicho cha FNL kwa ajili ya Interview akiwa amevaa Malapa, yaani kanda mbili......
Swali lilikuwa ni Je, kwani kuvaa Kandambili kunaharibu nini?'

SINTAH AJIKANYAGA KUHUSU KUWA NA MTOTO.
Katika hali isiyotarajiwa, Sinta alishindwa kueleweka baada ya Kujikanyaga kwingi kuhusiana na yeye kuwa na Mtoto. Mmoja kati ya Mashabiki na Watazamaji wa EATV kutoka Nchini Uganda, alimtumia Sam SMS kumuuliza Sintah kama ana Mtoto Uganda au Lah, lakini Sintah alijikanyaga haswa huku akishindwa kwenda Direct kama ana Mtoto au Lah, na kuishia kusema "Kwanini wanafuatilia Maisha Yangu?"...Mimi naamini anaye.

SINTAH- "OKWI NI BOYFRIEND WANGU TU"

Katika Hali nyingine ya Kushangaza, ni Sintah ambaye ni Mmmiliki wa www.sintah.com kujikanyaga kuhusu uhusiano wake na Emmanuel Okwi, Mchezaji wa Timu ya Taifa Ya Uganda. Nuru, Jini Kabula, na Sam walimuhoji sana Sintah kuhusu hilo, ila aliishia kusema.."Okwi ni Boyfriend wangu tu jamani...kwani Boyfriend si Rafiki wa Kiume?'   Bhaaaaaaaaaas.

KABULA NA UJAUZITO WA BUSHOKE.
Jini Kabula















Hiyo ilieta mengine huku wengi Tukimchora Kabula  kwa kushindwa kuheshimu mahusiano yake. Yes, alimsifia Bushoke kuwa ni Mrefu, ana Macho Mazuri, na ndo maana kabeba Kibendi chake. Pia alipoulizwa kuhusu Mr. Chuz, alisema na yeye ni Mwanaume Safi ndo maana alimzalia mwana....then akaulizwa akitkea mwenye Sifa kama za Bushoke, akasema "Labda na Yeye naweza Kumzalia"



MAUNDA ZORRO....Huyoooo..Kwenye MOVIE !!!

3:54:00 PM Add Comment




Maunda Zahir Zorro (Picha Kwa Hisani Ya Global Publishers)


Baada ya Maunda Zorro kuwa nje ya game yake kwa muda wa takribani miaka minne now she’s back but round hii kwenye movie scene.

Kwa mujibu wa Maunda Zorro ni kwamba ukimya wake ulitokana na kuwa bussy location akiigiza movie inayotarajiwa kutoka hivi sasa kwa jina la “Room Number 13” chini ya kampuni ya ZG iliyopo Zanzibar ambayo ndani yake amecheza kama ghost.

Does that means anaacha mziki, “No siwezi kuacha mziki. Pamoja na kuwa kwangu kimya nilikuwa na-record ngoma ambazo management yake ilikuwa ikizizuia kuzitoa na hadi leo sijui inakuweje“- Maunda Zorro.

NGWEA AINGIA MITINI......TID Njia Panda !!

3:36:00 PM Add Comment
 



Mangwea, Cow Obama, Cow Wizzy
 Radder Entertainment Mates, T.I.D & Mangwea

Na Frank Joachim & Baab Kubwa

Zilisikika Kinoma sana kuhusu Tour ya T.I.D na Mnyama mwenzake wa Radder Entertainment, Albet Mangwea “Ngwair, Cow Boy, Cow Obama, Cow Wizzy” watashuka Madiba land “South Africa” katika Kipindi hiki hiki cha Eid.

Sasa unajua kilichijiri sasa?...Mhhhhhhh…Eti Mangwea si amekula Chocho, simu yake haipatikani na kumuacha T.I D Njia Panda?
Kwa Mujibu wa Baab kubwa zimedondoka kuwa mwanzoni Mangwair alidai hana passport akapewa mkawanja wa kwenda kutatua suala hilo but baada ya kukamata mkwanja tu…akasepa kusikojulikana.

Baada ya kutafutwa bila mafanikio TID ameamua kuondoka mweneywe  kwenda South of A kukata kiu.
What will Happen, Stay here Here !!!!!

MAANDALIZI YA SENSA MAKETE YAENDELEA VIZURI.

3:14:00 PM Add Comment



Na Edwin Moshi.

Makete, NJOMBE.

Zikiwa Zimesalia siku Saba tu ,Imebainika kuwa maandalizi ya sensa ya watu na makazi wilayani Makete yanaendelea vizuri hasa wakati huu ambapo mafunzo kwa watekelezaji wa zoezi hilo yakiendelea kutolewa ngazi ya wilaya katika vituo vinne tofauti
 
Hayo yamebainika leo wakati kamati ya sensa mkoa wa Njombe ilipofanya ziara wilayani makete yenye lengo la kuangalia namna mafunzo kwenye vituo hivyo yanavyoendelea ikiwa ni pamoja na kuelewa changamoto zinazowakabili

Mmoja wa wakufunzi katika kituo cha Bulongwa kinachojumuisha tarafa mbili za Bulongwa na Magoma Bw. Fadhili Nkenza ameiambia kamati hiyo ya mkoa kuwa mafunzo yanaenelea kutolewa na kwa wale wanapoatiwa mafunzo ya dodoso refu kwa hivi sasa wanaendelea na mafunzo ya vitend ikiwemo kwenye kaya husika

Amesema katika kituo cha Bulongwa wanaopatiwa mafunzo kwa dodoso refu ni 58 na wanapatiwa mafunzo ya dodoso fupi ni 53 na wote ni kutoka kwenye tarafa mbili za Bulongwa na Magoma

 Amesema kuwa kwa sasa wanandelea na mafunzo na wamefikia kwenye hatua nzuri na ni lazima wayamalize kwa wakati kama ilivyopangwa kwenye muongozo

Akizungumzia changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wa mafunzo hayo, Bw. Fadhili amezitaja kuwa ni pamoja na upungufu wa vifaa (vifutio na penseli aina ya 2HB), mabegi kwa ajili ya kutunzia vifaa walivyokabidhiwa makarani hao wa sensa, pamoja na majina ya watu maarufu yaliyoandikwa kwenye ramani kukosewa hivyo kuwa ngumu kuwatambua ama kuwapata watu hao

 “kuna ramani tulizopewa zenye kuonesha maeneo mbalimbali lakini katika ramani hiyo kumeandikwa majina ya watu maarufu hivyo majina mengine yamekosewa kwa mafano unakuta mtu huyo maarufu amaitwa Fadhili Sanga lakini kwenye ramani pameandikwa Fadhili Chaula, sasa huo ni mkanganyiko pindi unapomtafuta humpati” alisema Fadhili

Ameongeza changamoto nyingine kuwa ni pamoja na malipo ya darasa la dodoso refu kuchelewa, hamasa kwa jamii kuwa ndogo, baadhi ya viongozi kutofahamu maeneo mengi wanayoyaongoza, ukubwa wa kazi lakini malipo ni kidogo, E.A kuvuka mipaka ya kata (kwa kata ya Kipagalo na Bulongwa) pamoja na changamoto ya wengi kusafiri kwa usafiri wa pikipiki na magari binafsi, hali inayopelekea usumbufu wakati wa kurejshewa nauli zao kwani hawana risiti kutokana na maeneo wanayotoka kukosa usafiri wa basi

Pia ameitaka kamati hiyo ya sensa wilaya kuangalia namna ya kuwasaidia wakufunzi hao kutolipwa sawa na wanaopatiwa mafunzo kutokana na kazi wanayoifanya wakufunzi hao ni kubwa lakini wanalipwa sawa

“Sisi wakufunzi tunatoa mitihani, bado tunabaki usiku tukiisahihisha na pia muda wote tunatoa mafunzo tukiwa tumesimama, kwa kweli tuoneeni huruma, lipelekeni hili mkoani muone namna ya kufanya kwa kweli” alisema Fadhili

 Hata hivyo kamati hiyo imesema itazifikisha mara moja changamoto hizo mkoani na kuona namna ya kuzitatua kwani lengo ni kufanikisha zoezi la sensa kama ilivyopangwa na serikali, huku ikiwataka wakufunzi hao kutekeleza majukumu yao kwa kadri ya uwezo wao kwa sasa licha ya changamoto zinazowakabili

Kamati hiyo kwa hii leo imetembelea vituo viwili vya Iwawa na Bulongwa

COUPLE TALK 8 Inakuhusu !!!

3:05:00 PM Add Comment




WACKAVVU BLACKAZ INC & BLACK TOUCHEZ ENT. Bado tunazidi kukuthamini kama mmoja wa watu ambao kiujumla ni muhimu sana Kwetu. Kwa dondo za Mapenzi, Love Stories (Za Ukweli zilizowahi kuwakuta Watu), My Bedroom, Fashion, Food, na Mazaga zaga Kibao ya Kimapenzi, yanapatikana COUPLE TALK 8.

Ingia www.coupletalk8.blogspot.com ushuhudie Mwenyewe.
Ahsante.

Imetolewa na :
Frank Magnus Joachim, 
C.E.O - WACKAVVU BLACKAZ INC & BLACK TOUCHEZ ENT

HATUA MEDIA COMPANY LTD...Ndo kwanza inamalizia Mikakati. Chekishia Vitu vilivyoko Njiani mazee

2:52:00 PM Add Comment






 HAYA NI BAADHI YA MAJARIDA YATAKAYODONDOSHWA NA HATUA MEDIA COMPANY LTD






Jarida La MULE MULE litakalokuwa Linatoka Kila Jumatatu Tu katika muonekano huu, tofauti na Muonekano wa Mule Mule Ijumaa. Majarida haya Yatakuwa Yakitoa Taarifa Mbali mbali za Udaku na Ukweli kuhusu Mishe za Watu Maarufu Nchini kwa Katika Weekend Nzima (Ijumaa, Jumamosi, Na Jumapili)


Jarida Hili la Mule Mule, Litakuwa linatoka Kila Ijumaa Tu, likikuletea Habari Mbali mbali za Udaku na kadharika kuhusu Watu maarufu Duniani kwa Muda wa Juma Zima (Jumatatu hadi Alhamisi). Pia katika Jarida hili utapata fursa yua kufahamu viwanja vya Bata, watu kutangaza Biashara yao katika Weekend kwa Bei nafuu kabisa

Jarida Hili la "Ndimu, Litakuwa linatoka Kila Jumatano Tu. Ni jarida ambalo linalenga hasa kukosoa Uchafu, Uppuzi, Unafiki, Uwongo, na Majigambo ya Watu Maarufu Nchin Tanzania tu, ili kuwekana Sawa. Pia Jarida litakuwa nlinatoa Matangazo mbali mbali, na kukaribisha Matangazo mbali mbali kwa Gharama nafuu Kabisa.

HAYA HAYA WADAU WANGU....

2:05:00 PM Add Comment






Frank M. Joachim, Mmiliki wa joachimjunior.blogspot.com & coupletalk8.blogspot.com. Pia ni C.E.O wa Black Touchez Inc & Wackavvu Blackaz Entertainments


Baada   ya Muda kama wa Wiki Mbili hivi, nimekuwa nikjaribu kuboresha zaidi Michkato itakayokuwa ikifanyika ndani ya Hii Blog. Moja wapo ni kufanyia kazi maoni ya Kuboresha Zaidi blog hii, pamoja na kuandaa itakayokuwa ikizungumzia suala zima la Mahusiano mbali mbali ambayo iko tayari hivi sasa (www.coupletalk8.blogspot.com)

Baada ya kukosa radha Kibaao kutoka katika Blog hii, now natangaza Rasmi kuwa NIMEREJEA TENA, yaani I'M BAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAACK

News kibao zitakuwa Zinatiririka Humu ndani asikuambie Raia aisee....Kote kote ntakuwa nagusa kama kawaida.

Nashukuru sana kwa Ushirikiano wenu, na ninawapenda sana aisee
Lets Roll...                                    

MNADA BANNER