REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WAHAMIAJI TOKA ETHIOPIA WAKAMATWA MKOANI RUVUMA

2:57:00 AM Add Comment
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Koku Lwebandiza akielezea jinsi walivyo fanikisha kuwa kamata wahamiaji haramu kutoka Ethiopia amesma wahamiaji wote 22 wata fikishwa mahakamani ili hukumu itolewe warudishwe kwao Ethiopia







PICHA NA EDDY MO BLAZE

MWANAHABARI MWINGINE APIGWA RISASI NA JESHI LA POLISI..

2:49:00 AM Add Comment



 Na Francis Godwin
Mwanahabari mwingine  mkoani Dar es Salaam apigwa  risasi na askari  polisi ambao  wanadaiwa  kuwa  walikuwa  wakimsaka mtuhumiwa  wa ujambazi  mwanamke na kuishia kumpiga mwanahabari  huyo mwanaume  Bw  Shaban Matutu wa gazeti la Tanzania  Daima.


Tukio  hilo limetokea jana majira  ya saa 2 usiku  jijini  Dar es Salaam ambapo askari  hao walipofika  nyumbani  kwa  mwanahabari  huyo na  kumgongea mlango na  wakati akifungua mlango ndipo

 Matutu amepigwa risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu ambapo katika zoezi hilo, walienda na kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo, kabla ya kutwanga kwa risasi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mara baada ya tukio hilo, mwandishi huyo amekimbizwa hospitali ya Mwananyamala ambako anaendelea kupatiwa huduma ya haraka na inaelezwa kuwa, amejeruhiwa lakini hali yake si mbaya sana
Habari zaidi zitakujieni

Taarifa za uhakika na ambazo zimethibitishwa­ zinaeleza kuwa jana usiku polisi mwenye silaha, aina ya bastola alimjeruhi begani kwa risasi, mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu.

Risasi bado imenasa kwenye bega lake hadi sasa Matutu alipigwa risasi nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam wakati askari walipovamia nyumba yake kwa madai kwamba kuna kibaka aliingia kujificha nyumbani hapo. Hivi sasa Matutu anatibiwa Mwananyamala hospitali, lakini amepewa rufaa kwenda Muhimbili.

Mwenyekiti  wa  jukwaa la wahariri Tanzania Bw Absalom Kibanda, ambaye amefanya jitihada za kumuhamishia Matutu Muhimbili, anasema hali ya Matutu siyo nzuri na kwamba wanajipanga kwenda Muhimbili kuona iwapo risasi hiyo itaondolewa mwilini.

Hata  hivyo  Kibanda ameeleza  kusikitishwa kwake ni  vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi ya  wanahabari nchini Tanzania ambavyo  vimeendelea kufanywa na jeshi la  Polisi nchini na kutaka polisi  waliofanya  hivyo  kuchukuliwa hatua  kali.

Alisema wakati Taifa likiwa bado katika majonzi ya  mauwaji ya  kinyama ya Mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi leo  tunashudia tena unyama mwingine dhidi ya  mwanahabari  huyo.

Hivyo  iwapo jeshi la  polisi litakosa majibu juu ya sababu ya  kumpiga risasi mwanahabari  huyo ambaye hata  hivyo hakuwa mlengwa katika msako wao  wa kumsaka mtuhumiwa wa ujambazi ambae ni mwanamke basi itafika  sehemu  wanahabari nchini  watalichukulia jeshi la polisi ni maeneo ya hatari kwao

LEO NI BIRTH DAY YA PRESENTER MATATA WA KITULO FM RADIO , TATU YASIN SIJAONA "TATY"

2:27:00 AM Add Comment





TAARIFA KWA UMMA

1:24:00 AM Add Comment

TANGAZO KWA UMMA.
Mkuu wa Chuo cha ROYAL (Royal College Of Tanzania-RCT) anapenda kuwataarifu kuwa Mahafali ya 11 yatafanyika  Disemba 22, 2012 Katika VIWANJA VYA CHUO Hicho.
Watakaohitimu ni :
  • Stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Diploma in Journalism)
  • Stashahada ya Ustawi wa Jamii (Diploma in Social Work With Community Development)
  • Astashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Certificate in Journalism)
  • Astashahada ya Ustawi wa Jamii (Certificate in Social Works with Community Development)      
Kama wewe Ni Muhitimu katika Ngazi hizo, unaombwa Kuthibitisha Ushiriki wako katika Mahafali hayo, kabla ya Disemba 07, 2012.
 Uthibitisho huo Ufanyike Kupitia namba Zifuatazo : +255756 672 684 au +255713 390 903

Nyote Mnakaribishwa katika Maendeleo ya Tasnia ya Habari Nchini

Imetolewa na 
Nsajigwa Mwalugaja,
Mkuu Wa Chuo cha Royal (Royal College Of Tanzania- RCT)   

WANANCHI WA ZANZIBAR WATAKIWA KUTEMBELEA UTALII WAO

12:54:00 AM Add Comment
Na Safiya Mohammed "Safmuu", ZANZIBAR


Wananchi wameshauriwa kutekeleza agizo la Utalii kwa wote kwa kuyatembelea maeneo mbali mbali ya utalii Zanzibar ili kufahamu historia ya nchi ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi.

 Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdallah Ali wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliyojumuisha wanahabari na maafisa wa Makumbusho.
 

 Pia ameongeza kuwa katika kutekeleza agizo la Utalii kwa wote wananchi wanapaswa kushajihishwa kutembelea maeneo ya kihistoria badala ya kuwaachia watalii peke yao kufanya ziara katika maeneo hayo. Bw. Abdala amesisitiza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wenyeji hawana hamu ya kujua historia ya nchi yao na kuwafanya wageni kujua historia ya Zanzibar. 


 Aidha Mkuu huyo wa makumbusho amemaliza kwa kusema kuwa Idara ya Makumbusho imeweka kiwango kidogo cha Shilingi 1000 ili kumrahisishia mwenyeji pale anapohitaji kwenda kutembelea maeneo ya makumbusho kwa ajili ya kujua historia ya nchi yao

HAWA NDIO VODACOM.....KAZI NI KWAKO SASA.

12:29:00 AM Add Comment


Taarifa kwa vyombo vya Habari
*       Vodacom na Nokia yaja na ofa ya funga mwaka
*       Maelfu ya zawadi kushindaniwa kwa wanunuzi wa simu za Nokia
*       Pia kufaidika na SMS, muda wa maongezi na internet za  bure

Dar es Salaam, Disemba 4, 2012 ... Wakati shamrashamra za maandalizi ya msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka yakiwa yanaendelea, Kampuni ya  Vodacom Tanzania na Nokia zimetambulisha ofa kabambe kukamlisha furaha ya kuelekea kufunga mwaka wa 2012.

 Kampuni hizo kwa pamoja zimezindua rasmi shindano litakalomuwezesha mteja yeyote atakayenunua simu ya mkononi aina ya  Nokia, kujishindia zawadi mbalimbali papo kwa hapo, pamoja na kupata fursa ya kuingia kwenye droo kuu.
Mteja atakayenunua simu ya Nokia na kisha kuweka muda wa maongezi wa aidha Tsh 1,000 au Tsh 1,500  atapata kifurushi cha BURE chenye muda wa maongezi  wa dakika 10, SMS 50  na internet ya MB10 kila siku kwa muda wa wiki moja. Kila simu ya Nokia itakayonunuliwa itakua na namba maalumu/kuponi ambayo mteja atatakiwa kutuma namba hiyo kwa SMS kwenda 15544 ili kuingizwa kwenye droo. Kila SMS itakayotumwa kwenda kwenye namba 15544 itatozwa gharama ya kawaida ya SMS.

Washimdi wa droo hizo zitakazokuwa zikichezeshwa kila siku watakuwa wakijishindia zawadi za simu, chargers, t-shirts na headphones zitakazotolewa kwa wateja kama zawadi za papo hapo.

"Ushiriki wa kubahatika kujishindia zawadi za papo hapo humuwezesha mteja kuingia moja kwa moja katika Droo kubwa ya mwisho itakayofanyika Januari 11, 2013 ambapo washindi watapata simu za kisasa za Nokia Lumia."Alisema Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa

Washindi wa zawadi za kila siku watachukua zawadi zao katika maduka ya Vodacom yaliyochaguliwa, ambapo watapatiwa huduma stahiki

Shindano hilo litafikia tamati ifikapo Januari 10, 2013, majira ya usiku, na Januari 11, 2012 ndiyo siku ambayo Vodacom na Nokia zitachezesha droo itakayoshirikisha washiriki wote wa shindano hili toka mwanzo, na kati yao mshindi atatangazwa

MNADA BANNER