REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KANYE WEST ANAKUKERA NA MANENO YAKE MABAYA?

6:39:00 AM Add Comment




Ohooo..Ushalalalaaaaa..kama ulikuwa unakereka sana na Mijimaneno ya Kanye West, BABA NORTH WEST Himself, amesema kuwa hatozungumza chochote kibaya dhidi Mtu yeyote Kwa angalau miezi Sita

Katika Moja Ya Tour zake katika Jiji la TORONTO Nchini marekani, amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuukaribisha Vema Mwaka Mpya wa 2014, na hata kujipanga kufanya yaliyo mazuri katika Mwaka Huo Mpya.

Pia kanye aliongeza kuwa, ili kudhihirisha hilo, katika Show Hiyo, ndio imekuwa mara yake ya Mwisho Kutamka maneno mabaya na machafu kwa Mtu yeyote na Juu ya Kitu chochote.

Hivi sasa kanye West bado yuko katika wakati Mgumu wa Kukopi Wimbo wa Bound kutoka PONDEROSA TWINS PLUS ONE, ambapo yeye kanye aliutumia na Kuuita BOUND 2, huku akiwa amemshirikisha Mchumba Wake Kim Kardashian

UNAMKUMBUKA LIL ROMEO?..SOMA HII

6:33:00 AM Add Comment



Kipindi Cha Nyuma sana alikuwa ni Hasimu Mkubwa wa LIL BOW WOW, ambaye hivi sasa anajiita BOW WOW ama Mr 106 BOW WEEZY…

Na kama bado Hujamkumbka, Ni Mtoto wa Mcheza Basket ball ambaye Pia Ni Mmiliki wa Studio ya NO LIMIT RECORDS…

Ili kukumbusha zaidi, Romeo Ninayemzungumzia, ni Yule aliyepiga Collable na AY katika kwaju la Speak With your body, ambalo lilifanya Byee Byee kinoma miaka Kadhaa iliyopita.


Sasa, basi Kwa Mujibu wa Mtonyo tuliotonywa na Mkuda Mkubwa Nchini marekani Kunako NYUMA YA PAZIA, eti inawezekana kabisa kuwa Romeo anataka Kutoka na SELENA GOMEZ, ambaye Ni EX wa The majanga Boy, JUSTIN BIEBER.

Ili kuthibitisha kuwa kuna uwezekano Mkubwa wa Romeo Mwenye Miaka 24, akamficha JUSTIN BIEBER katika Moyo Wa Mrimbwende huyo SELENA, kumekuwa na kupostiwa kwa Picha Mbali mbali katika Account ya Instagram ya SELENA, kuwa ROMEO amekuwa akimuomba sana watoke out jambo ambalo lilifanikiwa.

Sasa Mchakato Umekaaje?

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa chanzo kilichopo karibu na SELENA GOMEZ, inasemekana kuwa wawili hao wamekuwa wakitoka Wote mara Kadhaa na Kwenda Kutafuna Bata sehemu Tofauti, huku akikanusha kuwa wawili hao hawana mahusiano ya kimapenzi.


Lakini Chanzo cha Mitonyo Yote hii, ni baada ya ROMEO kupost Picha ya Selena kunako INSTAGRAM na Kusema kuwa ni Moja ya watu ambao hatowasahu hasa baada kumpatia kizuri katika Usiku mmoja..

NDIVYO WALIVYOSHREKEA SIKU KUU YA CHRISTMAS

6:24:00 AM Add Comment
 JAY Z akiwa na Tabasam katika vazi la SAINT CLAUSE, katika Siku ya Christmas

 NICK CANNON na Mke wake MARIAH CAREY wakiwa katika Poz la Christmas

 NICK CANNON, MARIAH CAREY na Watoto wao hawakuwa Nyuma

 RIRI: Rihanna Naye alikuwa na Mizigo Mikubwa

 RIRI: katika pauz...
 FUTURE na Mchumba wake CIARA nao hawakuwa Nyuma...

DRAKE na Mwanae nao Walikuwa Poa kabisa

 DIDDY na Familia yake hawakuwa Nyuma kabisaaaaaaaa

LIKE FATHER..LIKE SON: Wiz Khalifa naye alienjoy na Mtoto wake, SEBASTIAN THE BASH
 BOTTOMS UP..BOTTOMS UP: Trey Songz akiwa in Big Smile...

 TYGA na Mchumba Wake Chyna....Merry Christmas
 Mtoto wa Tyga CAIRO naye huyu hapa...

 Duh..Rozaaaaaaaay alipost Hii kitu
 EMINEM was Realy happy. kama ambavyo unamuona kwa Pic

 CHRIS BROWN "BREEZY" akiwa na Girlfriend wake KARRUECHE. Mwaaaaaaa

 SNOOP DOGG akiwa na Milley Cyrus..Braaaah

Big Man The GAME naye alikuwa So hot...like This

BAADA YA UKIMYA MREFU, FABULOUS KILA KITU TAYARI

6:00:00 AM Add Comment



In Fact kama Utakuwa ni Mfuatiliaji Mzuri sana wa JS (Jam Session) kwa Mwaka 2013, Kipindi cha awali kidogo tukliwahi kukupa Mtonyo Kuwa, The Swagg Boy FABULOUS, anakuja Town na New Mixtape ambayo ameipa Title la SOUL TAPE 3, ikiwa Ni Mfululizo wa Soul tape Mbili ambazo alizitoa Awali.

Sasa Mikwaju Iliyomo Ni kama Ifuatavyo

1. Everything Was The Same (feat. Stacy Barthe)
2. Sacrifices
3. Playa
4. The Get Back
5. Foreigners (feat. Meek Mill & Mike Davis)
6. The Hope (feat Jadakiss)
7. You know (feat. Young Jeezy)
8. Cuffin Season
9. Thim Slick (feat. Jeremih)
10. Lay Down (feat. Ryan Leslie)
11. Situationships (feat. Mack Wilds & Tiara Thomas) *Bonus Cut*
12. Young OG

HII NDIYO ZAWADI ALIYOITOA DIAMOND PLATNUMZ KWA WATOTO WALIOSHINDA KUCHEZA STYLE YA NGOLOLO….

5:56:00 AM Add Comment



KATIKA Moja ya Vitu ambavyo anakubali sana NASIB ABDUL “Diamond”, ni Pamoja na Kuwajali mashabiki wake, ambao pia Ni Watoto Wadogo.

Kabla ya Sikukuu ya Christmas, Mkali huyu wa Muziki wa Kizazi kipya Nchini Tanzania, aliitoa Siku yake kufurahia na Watoto wadogo ambao walinufaika na Kile alichokifanya Diamond.

Platnum awali aliweza kushiriki Chakula cha Mchana na watoto katika Kituo cha Kulelea watoto cha AL-MADINA Kilichopo TANDALE Jijini DSM, ambapo ilikuwa Ni kama Sehemu ya Thanx Giving Kwao.


Tofauti na Hilo, Diamond Aliweza Kushiriki Tamasha La Siku Kuu ya Christmas na watoto wadogo katika Viwanja Vya LEADERS CLUB huko huko DSM, ambapo Kulikuwa na Kivumbi cha Kuwasaka washindi watatu watakaofanya Vema katika Mchakato wa Kucheza NGOLOLO.

Katika Shindano Hilo, Finaly walipatikana watoto watatu ambao walionekana kufanya Vizuri Balaa, jambo ambalo lilimfanya PLATNUM Kuwapatia zawadi ambayo ni Msaada mkubwa Sana Kwa maisha Yao.


Tofauti na Kuwapa Zawadi ya Fedha, Pipi, Chocklate, au Nguo, Platnum alisema Kuwa, Management Nzima ya WASAFI CLASSIC, itawasomesha watoto hao walioshinda, Miaka Yote waliyobakiza Shuleni, huku akiongeza Kuwa atawahamisha na kuwapeleka katika Shule Bora zaid.

Unasemajekuhusu Hilo?

MNADA BANNER