REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA: PUMZIKA KWA AMANI PADRE EVARIST

4:54:00 AM 1 Comment
PUMZIKA KWA AMANI PADRI EVARIST MUSHI. BWANA AMETOA...NA BWANA AMETWAA. UWASAMEHE WALE WOTE WALIOKUTENDEA UNYAMA HUO, MAANA KAMWE HAWAJUI WALITENDALO

ZA FASTA: AMBER ROSE YUKO LABOUR

4:49:00 AM Add Comment
Mamito Amber Rose ambaye ni Mchumba wa Wiz Kharifa, inasemekana kuwa Yuko Labour, na Muda wowote tunaweza kupata taarifa Njema za Kujifungua kwake.
Mungu Amsaidie, na tutaendelea kuwajuza kitakachojiri hapa hapa BLACK TOUCHEZ

PICHA : NAZINDUA KIWANDA CHA KUSINDIKA MBEGU ZA PAMBA

1:13:00 AM Add Comment

MBEGU NZURI SANA HIZI: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mbegu za pamba wakati alipofungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti.



NAKATA UTEPE: Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa  cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti  na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho, Morgan Nzwele. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUNATAKA ADHABU YA KIFO KWA WANAOTUUA- ALBINO RUKWA

1:09:00 AM Add Comment




NA HAMZA TEMBA – OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
Mwenyekiti wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania “Tanzania Albino Society” (TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.

Aliyasema hayo jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.

Amesema kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. “Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino” alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika Mkoani kwake.

Kumekuwepo na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao zinaendelea.

Vilevile katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.
Matukio yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri

KUTOKA FACEBOOK: KWELI KAKA?

1:06:00 AM Add Comment



Billy G. Shechambo posted to ROYAL COLLEGE OF TANZANIA - Learn to serve the Community

Joyce Ndalichako adai Clouds FM imechangia yaliyotokea Kidato cha Nne!
 Adai walimpa 'Promo' kijana aliendika matusi na "Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.

AKILI YANGU ILIVYO FINYU : KAMA HAJUI ANGEJAZA NINI JAMANI?

12:53:00 AM Add Comment
Na Frank M. Joachim.
Vitu vingine huwa tunalaumu tu jamani....hapa Kingetafutwa Chanzo cha yeye kujaza hivi, halafu ndio tutoe taarifa kamili. Pengine ana matatizo ya akili, Hajawahi kufundishwa, yaani sababu zipo Nyingi tu!

MKURUGENZI MPYA WA TTCL HUYU HAPA...

12:50:00 AM Add Comment



Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL jana imemteua Dkt. Kamugisha Kazaura kuwa Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo.

Dkt. Kazaura amechukua nafasi ya aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Said Amir Said ambaye amestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kazaura alikuwa ni Afisa mkuu wa ufundi (CTO)wa TTCLBodi ya wakurugenzi ya TTCL imewaomba wafanyakazi na menejimenti kumpa afisa Mtendaji mkuu mpya ushirikiano wa kutosha ili kuwa na mshikamamo wa pamoja ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi.

Kwa kusisitiza Bodi imesema “Tufanye kazi na tusonge mbele pamoja, kama timu ililyoshikamana pamoja na iliyodhamiria kuinua utawala bora.”

Dkt. Kamugisha Kazaura alitunukiwa shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (PhD)katika fani ya Habari na mawasiliano ya simu katika chuo kikuu cha Waseda kilichopo Tokyo, Japani.

MNADA BANNER