REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BET AWARDS 2013: DRAKE AFUNIKA KWA NOMINATIONS, RADIO NA WEASEL KUIBEBA BENDERA YA AFRIKA MASHARIKI

2:38:00 AM Add Comment






BET Awards ’13 Nominations

Best Female R&B/Pop Artist
Beyoncé
Tamar Braxton
Alicia Keys
Rihanna
Elle Varner


Best Male R&B/Pop Artist
Chris Brown
Bruno Mars
Miguel
Justin Timberlake
Usher


Best Group
Macklemore & Ryan Lewis
Mary Mary
Mindless Behavior
Slaughterhouse
The Throne (Kanye West & Jay-Z)


Best Collaboration 2 Chainz f/ Drake – “No Lie”
A$AP Rocky f/ Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “Problems”
French Montana f/ Rick Ross, Drake and Lil Wayne – “Pop That”
Kendrick Lamar f/ Drake – “Poetic Justice”
Justin Timberlake f/ Jay-Z – “Suit & Tie”
Kanye West f/ Big Sean, Pusha T and 2 Chainz – “Mercy”


Best Male Hip Hop Artist
2 Chainz
A$AP Rocky
Drake
Future
Kendrick Lamar


Best Female Hip Hop Artist
Azealia Banks
Eve
Nicki Minaj
Rasheeda
Rye Rye


Video of the Year 2 Chainz f/ Drake – “No Lie”
A$AP Rocky f/ Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “Problems”
Drake – “Started From The Bottom”
Drake f/ Lil Wayne – “HYFR
Kendrick Lamar f/ Drake – “Poetic Justice”
Macklemore & Ryan Lewis f/ Wanz – “Thrift Shop”
Miguel – “Adorn”
Rihanna – “Diamonds”
Justin Timberlake f/ Jay-Z – “Suit & Tie”
Kanye West f/ Big Sean, Pusha T and 2 Chainz – “Mercy”


Video Director of the Year
A$AP Rocky & Sam Lecca
Benny Boom
Director X
Dre Films
Hype Williams


Best New Artist
Azealia Banks
Joey Bada$$
Kendrick Lamar
Trinidad Jame$
The Weeknd


Best Gospel Artist
Deitrick Haddon
Lecrae
Tamela Mann
Mary Mary
Marvin Sapp


Best Actress
Angela Bassett
Halle Berry
Taraji P. Henson
Gabrielle Union
Kerry Washington


Best Actor
Don Cheadle
Common
Jamie Foxx
Samuel L. Jackson
Denzel Washington


YoungStars Award
Gabrielle Douglas
Jacob Latimore
Keke Palmer
Jaden Smith
Quvenzhané Wallis


Best Movie
Beasts of the Southern Wild
Django Unchained
Something from Nothing: The Art of Rap
Sparkle
Think Like a Man


Subway Sportswoman of the Year
Gabrielle Douglas
Brittney Griner
Candace Parker
Serena Williams
Venus Williams


Subway Sportsman of the Year
Victor Cruz
Kevin Durant
Robert Griffin III
LeBron James
Ray Lewis


Coca-Cola Viewers Choice Award
A$AP Rocky f/ Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “Problems”
Drake – “Started From The Bottom”

Kendrick Lamar – “Swimming Pools (Drank)”
Miguel – “Adorn”
Rihanna – “Diamonds”
Justin Timberlake f/ Jay-Z – “Suit & Tie”


Centric Award
Tamar Braxton – “Love and War”
Fantasia – “Lose To Win”
Miguel – “Adorn”
Nas – “Daughters”
Charlie Wilson – “My Love Is All I Have”


Best International Act: Africa
2Face Idibia (Nigeria)
Toya Delazy (South Africa)
Donald (South Africa)
Ice Prince (Nigeria)
R2Bees (Ghana)
Radio and Weasel (Uganda)

Best International Act: U.K.
Marsha Ambrosius
Estelle
Labrinth
Rita Ora
Emeli Sandé
Wiley



NIPO MWANZA, NYUMBANI NILIKOZALIWA. HII NDIYO LADHA YA JIJI LETU

2:15:00 AM Add Comment
 BISMACK ROCK: Moja kati ya Vivutio Vizuri sana katikati ya JIJI la Mwanza. Mawe haya yabo katika Maji ya Ziwa Victoria

 FISH KEEP LEFT: Usione Umati huo wa Watu umejaa hapo ukadhani kwenye hilo eneo kuna tukio la Hatari. Hapo kuna sanamu ya SAMAKI,ambaye Wakazi wengi wa Mwanza na Hata Wageni, hupenda kupiga Picha mbele ama Pembeni ya Sanamu hiyo ya Samaki

 KAMANGA GARDEN: Hii ni Bustani katika Bara bara ya Kutoka Kamanga kuelekea CAPRIPOINT. Inavutia sana na Inang'aa Muda Wote. Karibu Mwanza

 HALIDONDOKI HILO: Moja kati ya Mawe ya Ajabu yanayopatikana ROCK CITY Mwanza. Unaweza dhania linadondoka lakini hulidondoshi hata kwa Greda

 RAILWAY STATION: Kwa wale tunaotumia Usafiri wa GOGO (Treni) Kutoka, Dar, Dodoma, Shinyanga, na Hata Kwingineko, Hapa ndo Mwisho wa Reli yetu kwa Jiji la Mwanza

 LIKO IMARA HILO: Jiwe ambalo liko karibu na Reli ndani ya Jiji la Mwanza. Mwenyewe unawesza dhania pia kuwa litaidondokea Treni, lakini miaka na Miaka, jiwe hilo halijawahi hata Tikisika

 MAGOROFANI: Hii ndio Magorofani ya Mitaa yetu ya Uswahilini. Nyumba zimejengwa juu kwajuu, na Hasa juu ya Jiwe hili na Lingine kama Unavyoona Mwenyewe

 KIVUKO: Hiki ni Kivuko kilichopo Kamanga Ferry: PANTONZ haziko Da'slaam Peke ake, hadi huku zipo aisee

 MVUTO WA AINA YAKE: Bismarck Rock katika Muonekano wa Karibu.

 KARIBU SATO: Utambulisho wa Kitoweo kikuu cha Jiji la Mwanza na Kanda Ya Ziwa


KISIWA: Hiki Ni Kisiwa cha SAA NANE,ambacho pia Ni Hifadhi ya Wanyama Mbali mbali na Kituo cha Utalii hasa kwa Jiji la Mwanza

KUMBUKUMBU: Hii Ni Kumbu Kumbu ya Kihistoria kwa Jiji la Mwanza.

KARIBU MWANZA: Mandhari Yetu Ni Nzuri Sana.

MBEYA YETU:PICHA ZA AJALI TENA WILAYANI RUGWE MKOANI MBEYA JIONI YA JANA MMOJA AHOFIWA KUFA MAJERUHI MWINGINE APELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

1:18:00 AM Add Comment




AFYA: MATUMIZI YA SIMU KWA WAUGUZI WAKATI WA KAZI

12:50:00 AM Add Comment



Gordon Kalulunga, Mbeya  
              
WAUGUZI nchini wameshauriwa kuacha simu zao katika vyumba maalumu au kuzizima wakati wanapotoa huduma kwa wagonjwa.

Wito huo ulitolewa juzi na muuguzi mstaafu Andulile Mwansyange (68) alipokuwa akitoa tofauti ya utumishi wake na uuguzi wa sasa katika maadhimisho ya Siku ya Uuguzi Tanzania iliyofanyika Mbalizi-Ifisi, Mbeya.

Mwansyange alisema mjadala unahitajika kuhusu umuhimu wa wauguzi kutotumia simu za viganjani wakiwa kazini.

“Kuwe na mjadala wa wauguzi kutotumia simu wanapokuwa kwenye vyumba vya kutolea huduma muhimu pia wagonjwa wafunge simu wanapoingia kwenye matibabu.
…Unaweza kupigiwa simu ya msiba au kupokea ujumbe wa mtu anayekuhusu hali inayoweza kusababisha kuacha kutoa huduma kwa mgonjwa,’’ alisema muuguzi huyo mstaafu.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Upendo Sanga, alisema angekuwa mkufunzi wa wauguzi angewafundisha maadili na watakaoshindwa angewafukuza uuguzi.

Akisoma risala kwa niaba ya mkurugenzi huyo aliyekuwa mgeni rasmi, mwanasheria wa wilaya hiyo, Prosper Msivala, alisema suala la matumizi ya simu kwenye maeneo ya kutolea huduma limekatazwa na lipo kisheria hivyo halihitaji mjadala.

Naye Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Mbalizi Ifisi inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, Sikitu Mbilinyi, alisema upendo kwa wagonjwa ni tiba, hivyo umefika wakati kwa kila muuguzi kubadilika.
               

RUSHWA: POLISI 16 MBARONI

12:40:00 AM Add Comment



HATIMAYE Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewatia mbaroni askari 16 wanaohusishwa na tuhuma za uhalifu.

Kutangazwa kwa taarifa hiyo kunakuja siku chache baada ya Tanzania Daima kuandika habari juu ya polisi hao kwa kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuunda mtandao wa kihalifu.

Taarifa ya kukamatwa kwa askari hao zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kova alisema askari hao wanatuhumiwa kuunda mtandao wa kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru wa serikali.

Licha ya kuweka wazi idadi hiyo kamanda Kova aligoma kuyataja majina ya wahusika bila kuweka wazi kwa nini ameamua kufanya hivyo.

Kova pia alitumia muda huo kuilaumu Tanzania Daima, kwa kuandika habari za uhalifu huo juzi ikiwa ni baada ya uchunguzi wa zaidi ya wiki moja tangu kukamatwa kwa askari hao.

Alisema kabla ya gazeti hili kuandika habari hizo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, jeshi hilo lilikuwa limeshawakamata askari wake wanane kutokana na tukio hilo.


“Si kwa kuwa gazeti moja liliandika na ndiyo tumesukumwa kuwakamata wahalifu hawa; tulianza taratibu hizi mapema na tukawa tunasubiri muda muafaka wa kuweka mambo yote hadharani,” alisema Kova.

Hata hivyo Kova jana alishindwa kuweka wazi yalikopelekwa magari yaliyokamatwa kwenye uhalifu husika.

Wakati akishindwa kutaja kama kuna magari yaliyokamatwa, baadhi ya askri waliozungumza na gazeti hili wameshangazwa na hatua hiyo na kumtaka DCP Kova awe mkweli juu ya sakata hilo.

Askari hao wamehoji hatua ya Kova kuwakamata wenzao walioonekana katika picha za video za mnato na kushindwa kuyakamata magari yaliyokubali kushiriki katika uhalifu huo.

“Mnapaswa kujiuliza kama askari wameshafika 16 halafu hakuna gari hata moja lililokamatwa, hao watakuwa wanapelekwa mahakamani kwa ushahidi wa namna gani na kwa nini hayo magari hayakuweza kuchukuliwa katika hizo picha au ni siasa za mzee wetu zimewafanya mkashindwa kuhoji hilo?” alisema mmoja wa askari.


Mtandao huo unadaiwa kufanya kazi kwa takriban miezi sita kabla ya kujulikana na kuchukuliwa kwa hatua dhidi yao.

Kwa mujibu wa Chanzo cha habari, mbinu inayodaiwa kutumiwa ni kwa askari hao kuwasaidia wafanyabiashara kuingiza bidhaa kupitia bandari bubu ya Mbweni, kisha kuzipakia kwenye magari makubwa kwa ajili ya kutawanya bidhaa hizo katika masoko ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kuingizwa kwa wingi ni runinga, redio, pasi za umeme na kompyuta mpakato.

MIUNDO MBINU : BARA BARA SITA HIZOOOO, DAR- CHALINZE

12:32:00 AM Add Comment



SERIKALI imeanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam – Chalinze inayojengwa kwa njia sita, na katika mwaka wa fedha 2013/2014, imetenga Sh bilioni 100 kwa ajili ya kazi hiyo. Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014 juzi, alisema barabara hiyo itajengwa kwa ubia kati ya Serikali na kampuni binafsi.

“Kutokana na tangazo lililotolewa na Wizara kupitia Tanroads, kampuni 19 zimewasilisha mapendekezo ya jinsi ya kujenga barabara hii kwa njia sita kuanzia Dar es Salaam – Mlandizi na njia nne kuanzia Mlandizi – Chalinze.

Akizungumzia barabara kwa ujumla, alisema katika mwaka 2012/2013, Wizara kupitia Wakala wa Barabara (Tanroads), ilipanga kukamilisha ujenzi wa barabara kuu zenye urefu wa kilometa 414 kwa kiwango cha lami, kukarabati kilometa 135 kwa kiwango cha lami pamoja na kujenga na kukarabati madaraja 11.

“Hadi kufikia Aprili 2013, ujenzi wa kilometa 374.65 za barabara kuu kwa kiwango cha lami na ukarabati wa kilometa 140.63 kwa kiwango cha lami ulikamilika,” alisema Dk Magufuli. Kuhusu matengenezo ya barabara kuu, alisema lengo lilikuwa ni kuzifanyia matengenezo kilometa 10,534.3 na madaraja 1,154.

“Hadi kufikia Aprili, 2013, kilometa 6,052.8 za barabara kuu na madaraja 652 yalifanyiwa matengenezo,” alisema.

Waziri Wa Ujenzi, JOHN POMBE MAGUFULI
Wakati huo huo, wabunge wameipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kote nchini kwa ufanisi mkubwa. Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), aliitaka wizara hiyo kusonga mbele na kukaza buti kwa kuwa kazi yao nzuri inaonekana.

Naye Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Buyogera (NCCR-Mageuzi), alisema, “Kwa mara ya kwanza leo nawashukuru sana. Naipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kazi nzuri, ila naomba wanisaidie kuweka lami barabara za Kasulu.”

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), aliitaka CCM itembee kifua mbele kwa sababu imefanya kazi kubwa katika ujenzi wa barabara nchini. Kwa upande wake, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alisema kwa mara ya kwanza anaunga mkono kwa asilimia 100 bajeti, na kuwa watu wa Ludewa wataendelea kumuombea afya njema Dk Magufuli.

Mbunge wa Kwela, Ignas Malocha (CCM), alisema Tanzania sasa ina mtandao mkubwa wa barabara za lami, lakini akaomba wananchi walipwe fidia wanapobomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi. Naye Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (Chadema), alimpongeza Dk Magufuli kwa kutenga fedha kwa barabara za jimboni kwake, huku Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (CCM), akitaka fidia mapema kwa wanaobomolewa nyumba zao.

Wabunge wengine waliochangia na kuipongeza bajeti hiyo ya Wizara ya Ujenzi ni Joshua Nassari (Arumeru Mashariki – Chadema), Ramo Makani (Tunduru Kaskazini - CCM), Ezekiel Maige (Msalala- CCM), Kaika Telele (Ngorongoro – CCM), Cynthia Ngoye (Viti Maalumu- CCM) na Jerome Bwanausi (Lulindi – CCM).

Kwa upande wao, wabunge kutoka mkoani Tabora, licha ya kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri, wameitaka ikamilishe ujenzi wa barabara za mkoa huo kwa wakati kama zilivyoelezwa katika mikataba kwani kumekuwa na uzorotaji katika miradi mingi mkoani humo. Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) alisema,

“Sina hofu na Kamanda Magufuli, nafahamu wewe unachapa kazi. Kwa watu wa Tabora, tunakuomba usimamie ili kuhakikisha barabara zetu zinakamilika kwa wakati.

Nyingi mikataba imeisha na tunadaiwa fidia kubwa.” Mbunge wa Nzega, Suleiman Zedi (CCM) na Magdalena Sakaya (Viti Maalumu – CCM), waliungana na Rage kutaka barabara hizo za Tabora zikamilishwe mapema kwa sababu mkoa wao ‘umefungwa’ na mikoa mingine.

Katika hotuba yake, Dk Magufuli alieleza kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara za lami nchini kote, ujenzi wa madaraja na vivuko, na kuliomba Bunge limuidhinishe Sh trilioni 1.226, akachape kazi mwaka 2013/14.

MNADA BANNER