REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

FLAVIANA MATATA NA AY, WAMEUNGANA NA WATANZANIA WOTE WALIOPOTEZA NDUGU ZAO KATIKA AJALI YA MV BUKOBA

7:56:00 AM Add Comment

Jana Ilikuwa ni kumbu kumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba iliyotokea May 21 Mwaka 1996 Mkoani Mwanza ikitokea Bukoba Mkoani Kagera.

Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uingereza na Marekani Mwanaidi Majaar jana ameongoza zoezi la Kuweka Mashada katika Makaburi ya Kumbukumbu ya Watu waliopoteza Maisha katika ajali hiyo.

Flavian Matata ambae katika ajali hiyo alimpoteza mama yake mzazi sanjari na binamu yake, amewashukuru watu wote waliohudhuria katika kumbukumbu hiyo ya Ajali ya Mv.Bukoba ambapo amesisitiza kwamba jambo kubwa zaidi ni kuwaombea wale wote waliopoteza maisha wapumzike kwa amani.


Ambwene Yessaya (AY) alikuwepo siku ya jana katika maeneo hayo, na Hiki Ndicho Walichokizungumza

WILL SMITH NA MKEWE JADA PINKETI, WANACHUNGUZWA KUHUSU PICHA YA MTOTO WAO, WILLOW.

7:52:00 AM Add Comment

LOS ANGELS,Marekani
KITENGO cha Huduma kwa Watoto na Familia kutoka jijini Los Angels, kimesadikika kuanzisha Uchunguzi dhidi ya wazazi wawili, Will Smith na Jada Pinket, hasa kuhusu Picha ya Mtoto wao wa Kike Willow Smith, iliyomuonesha akiwa kitandani na Muigizaji MOISES ARIAS.

Kwa mujibu wa Mishe za Chimbua Chimbua, inasemekana Kitengo Hicho kimeamua kufanya Uchunguzi huo haraka Iwezekanavyo , ikiwa ni baada ya Picha ya Willow mwenye Miaka 13 akiwa kitandani na MOISES mwenye Miaka 20, huku kukiwa na mazingira tatanishi , Baada ya jamaa huyo kuonekana akiwa kifua wazi.

Kwa Mujibu wa Chanzo kimoja ambacho kipo karibu na familia Hiyo, kilifunguka kama Sio kumiminika kuwa, Upelelezi ama Uchunguzi Huo, Ulianza Juma lililopta, yaani wiki iliyopita Kuhusu Ishu Hiyo.

Hata Hivyo bado Chanzo hicho kimezidi kumiminika kuwa, Will Smith pamoja na Mke wake Jada Pinket, wameonekana kutoa ushirikiano Mzuri kuhusu Uchunguzi huo, ambao Kiujumla unadhamira ya kufahamu kilichokuwa kikiendelea baina ya watoto hao wawili.


Kama Utarudisha kumbu kumbu zako, TTM tuliwahi kukupa Mtonyo kuwa, mama Mzazi wa Willow, Jada, alisema kuwa Picha hiyo haikumaanisha Kile ambacho Wengi wanakidhania.

JAMAA AJITOKEZA KUMSHTAKI DR.DRE KUHUSU BEATS ELECTRONIC

7:50:00 AM Add Comment

Ukiskia Good Things Gone Baad, mchakato Ndo unaanzia Hapa, Zima TTM tukukatie Mtonyo fasta.

Jamaa Mmoja anayefahamika kwa jina la STEVEN LAMAR ambaye ni Meneja wa ONE-TIME-HEDGE-FUND, amejitokeza na kudai kuwa, amefungua mashitaka ya madai dhidi ya Dr. Dre na Jimmy Lovine hasa Kuhusu Beats By Dre na Beats Electronic ambayo itapigwa Bei Kwa Kampuni ya APPLE kwa Mkwanja Mrefu haswa.

LAMAR anawatuhumu wamiliki hao wa BEATS ELECTRONICS kwa kukiuka makubaliano yao ambayo pia yalikuwa Ndani ya Mkataba, hasa ikiwa ni baada ya Kuuza pasipo kumpa taarifa, huku akihitaji malipo ya Asilimia akadhaa kwa kuwa na Mchango katika Kufanikisha Beats By Dre.

Pia data Zinaeleza kuwa Miaka 8 Iliyopita, yaani Kuanzia Mwaka 2006, Dr. Dre na Jimy Lovine, waliwahi kumshtaki Lamar na washirika wake, ikiwemo kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi kipindi hicho, kwa madai kuwa alikuwa akitengeza Bidhaa Nyingine iliyokuwa na Mfumo wa kampuni ya BEATS ELECTRONIC, jambo ambalo lilikuwa ni Nje ya Mkataba wao.


Hata hivyo Lamar bado anadai Kuwa, anahitaji kulipwa Asilimia 20, kwa Ushirikano alioutoa mpaka Dre na Lovin wanakutana na kutengeneza kitu Kimoja, pamoja na kila alichokichangia katika Kampuni hiyo

NICKI MINAJI NA FORBES, WANA JAMBO

7:47:00 AM Add Comment

Muda Kidogo hivi umepita baada ya Jarida la FORBES kuchapisha habari yenye Kichwa Cha habari kuwa, HIP HOP INASHIKILIWA NA MWANAMKE MWEUPE, MWENYE NYWELE NYEUPE KUTOKA AUSTRALIA, ambaye bila Shaka alikuwa Ni IGGY AZAELA

Tofauti na Hilo, jarida hilo bado lilidai kuwa NICKI MINAJI Hivi sasa ni kama ameshuka baada ya kukaa Kimya Kwa Muda mrefu bila Kutoa ngoma Yoyote Mpya, jambo ambalo si Kweli, kwani Nicki ameshaachia Mikwaju kadhaa ya HIP HOP, ikiwemo L.A.N (Na Usitake Nitaje kirefu Chake).

Lakini baada ya watu Kibao kulalamikia Ishu hiyo hasa Tittle la jarida hilo, baadaye Forbes walibadili TITTLE na kuandika. MSANII MPYA ASIYELINGANISHWA NA WENGINE: MWEUPE, MWENYE NYWELE NYEUPE, TOKEA AUSTRALIA

Sasa Kunako Moja ya interview baada ya kuulizwa kuhusu Ishu Hiyo kunako Moja ya interview Nchini marekani, Nicki Minaj alijibu kwa Kucheka, huku akisema kwamba, Kampuni ya FORBES kiujumla, inatakiwa  kuwa na Hofu kuhusu Mkwanja atakaoupata atakaoupata, pindi atakapouza Kinywaji chake cha MYX FUSSION kwa Dollari za Kimarekani MILIONI 250.

Aidha Minaji ambaye hivi sasa ameshaachia Track yake ya PILLS & POTIONS imeshaachiwa rasmi, amesema kuwa kila Mtandao unauwezo wa Kuandika Chochote kile kuhusu Hip Hop, na hakuna tatizo juu ya hilo, Lakini kwaSuala la Iggy Azaela, Hakuna Kitu kama Hiyo.


Hata Mie Pia Ntakubali Kwaaa Kweli.

PICHA: MUONEKANO WA KIM KARDASHIAN KABLA YA SIKU YA NDOA, NA MAHALI AMBAKO ATAFUNGIA NDOA

7:15:00 AM Add Comment





















VIDEO YA MFALME YA MWANA FA, KUFANYIKA KENYA

6:47:00 AM Add Comment

DAR ES SALAAM, Tanzania.
Tunajua unajua kabisa  kwamba Kwaju la MFALME la Mwana FA , limekuwa moja kati ya talk of the Town tangia limeanza kubang kunako Mitaa Kibwena Tu hapa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa info ambazo TTM tumezinyaka, ni kwamba, Video Ya Track Hiyo, inatarajiwa kufanyika Nchini Kenya, off course FA mwenyewe kamiminika.

Director atakayesimamia Mzigo huo ni  KELVIN BOSCO, jombaa ambaye amepika Video ya ASNATE, ya Kwake Ambwene Yesaya-AY.
Kunako kwajju hilo ambalo hivi sasa Lina Downloads na Requests za kutosha, Sauti ya G. NAKO imesikika Pia.

ALL THE BEST LSA FA

MNADA BANNER