REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

JIDANGANYENI MUWAZINGUE WA AFRIKA KUSINI..ITAKULA KWENU, HII INAMHUSU D’BANJI

6:01:00 AM Add Comment

Na Black Touchez
KUMEKUWA na taarifa kuwa, Msanii D’Banj Kutoka Nchini Nigeria, yuko katika mahusiano na Binti kutoka Nchini Afrika ya Kusini , anayefahamika kwa Jina la BONANG MATHEBA, ambaye pia Ni Mtangazaji wa RADIO na TV.

SASA, baada ya Info hizo Kuenea zaidi huku na Kule Bloggers kadha wa kadha wa Nigeria, walianza kuandika Info hizo kwa ajili ya wasomaji wao Huku wakiaandaa Vichwa Vyao Vya habari kuwa D BANJ NA MREMBO WA AFRIKA YA KUSINI KATIKA MAHABA MAZITO

·        Usiwakosee Heshima Wa-South.
BAADA ya Bloggers Kuandika Hivyo, hatimaye alitokea Blogger mmoja kutoka Nchini humo humo Afrika Kusini, aliyeamua kutokulikalia Kimya taifa la Nigeria hasa Blogger kwa namna ambavyo wanamuita Bibie Huyo.

Jamaa huyo anayefahamika kwa jina SIBONGILE MAFU, aliamua kutumia account yake ya Twitter na kuwashangaa Bloggers hao ambao wanashindwa kutambua hadhi na Heshima ya Mrembo Huyo ambayo ni Kama Malkia wa Urembo Nchini Humo.
Jamaa huyo aliandika kama Ifuatavyo:

 ‘Bonang is referred to as D’Banj’s ‘pretty South African girlfriend’ by these Nigerian tabloids. Do they not know our queen?’

BONANG ambaye ni Mdandio Mpya wa D’BANJ, kama ulikuwa hujafahamu, ni Mmoja kati ya watangazaji wanaopendwa sana Afrika ya Kusini, Mwenye sauti Nzuri na Tabasamu tamu sana.


Tofauti na Hilo, Shemeji yetu Mpya, Ni balozi Mkubwa (BRAND GLOBA AMBASSADOR) wa Vipodozi vya REVLON, Mshindi Wa Tuzo ya Mburudishaji Africa ya Kusini, Pia ni Malkia wa Mitandao ya Kijamii Afrika ya Kusini.

BIFU KWISHA: CHAMELEONE NA BEBE COOL KUPIGA COLLABO

8:01:00 AM Add Comment




T
ANGIA wamefukuza Pepo la Uhasama na Uadui baina yao, Finally Tumeweza kunasa Mtonyo kuwa BEBE COOL pamoja na DR. JOSEE CHAMELEON Wanataraji kushusha Mkwaju wa pamoja maarufu kama Collaboration.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Big Eye, inasemekana kuwa wawili hao tayari wameshaingia Studi na Huenda wameshakamilisha Project yao, ambayo any Time, itaweza kudrop kunako masikio Yetu


Ikumbukwe kuwa, hiyo itakuwa ni Collaboration yao ya Kwanza, tangia waingie kunako “Tafaruku na Noma” kama Sio Bifu, ambvapo awali wawili hao waliwahi kupika Kitu kinafahamika kwa Jina la BOGOLAKO REMIX, mkwaju ambao ulikuwa ni wa Bebe Cool, na Ulifanya Po asana kuliko Headlines.

MENEJA WA RADIO NA WEASEL AZUA BALAA UK

7:55:00 AM Add Comment



T
UNAJUA kuwa, radio na Weasel walikuwa wamepigwa Stop kutia “Milonjo” yao kunako Nchi ya Uingereza, lakini taarifa zilienea kuwa Finally wamesamehewa.


Lakini Moja ya hatari Nyingine ambayo hatujui kama itazua Msala ama Lah kwa wasanii hawa na Timu Nzima, ni baada ya kudaiwa Kumtwanga Mwanamke Mmoja wa’Kidhungu” kutoka Nchi Hiyo Hiyo ya Malkia.

·        Mtonyo Kutoka Kwa Wadaku:
WAFUKUZA MAPEPO ambao wamedhamiria kufukuza Pepo Mchafu waSkendo katika Sekta ya Burudani, wamedaka Mtonyo Kuwa, Meneja wao WEASEL & RADIO (GOOD LIFE), anayefahamika kwa jina la CHAGGA, alimzingua Mwanamke wa UK aliyekuwa anajaribu kujifyatua “SELUFII” na wasanii hao waliokuwa Nchini Humo Kikazi.

Mtonyo unazidi kumiminika kuwa, Meneja huyo alijikuta akipigwa na Butwaa baada ya raia waliokuwa Eneo la Tukio kumtaka aombe msamaha na kuapa kutorudia tena kwa wanawake wa UK kuwazingua na hata Kuwasukuma, maana Sheria Nchini Humo Ziko Hot kuhusu kuwaonea wanawake

Sababu ambayo Meneja Chagga alijikuta akimsukuma Mwanamke Huyo, ni kwamba Eti wasanii wake walikuwa wamechoka Haswa, na walitakiwa Kupumzika.


WAFUKUZA MAPEPO Bado wanafuatilia kama Tukio Hilo linaweza kuwafanya RADIO, WEASEL na Timu Nzima Kufungiwa Tena Kwenda UK, ama LAH

EMINEM NI MWIZI WA NYIMBO?

7:53:00 AM Add Comment



M
UNGU tusaidie sana Mwaka Huu usiandamwe na Pepo la Wizi wa Nyimbo ambalo limeutafuna sana Ulimwengu wa Burudani Ulimwenguni Kote hasa kwa Mwaka 2014.


Lakini moja kati ya taarifa za Wizi wa Wimbo ambazo zinaufungua Mwaka 2015 kwa mara ya Kwanza kabisa, ni Kuhusu Rapper EMINEM ambaye huenda akafikishwa Mahakamani  kwa Tuhuma za Ku-sample wimbo wa RAP GOD bila Idhini wala Taarifa

RAPPER RAYMOND JONES kutoka kunako kundi la Muziki la HOT STYLES, wameamua kufungua Madai ya takriban USD MILIONI 8 dhidi ya Eminem na Record label yake, kwa tuhuma za kutumia Vionjo vya Wimbo wao katika Mkwaju wa RAP GOD uliofanya Poa kupita maelezo kwa Mwaka 2014


Mkwaju ambao Vionjo vyake vinadaiwa Kuibiwa, unafahamika kwa Jina la LOOKIN BOY, Hot Styles wamemshirikisha Rapper Mpotevu, Young Joc

MATONYA !!!!!!! KWANINI LAKINI

7:49:00 AM Add Comment

MOJA kati ya Vitu ambavyo vimeweza kushtua Timu Nzima ya Jam Session na Kitengo cha WAFUKUZA MAPEPO, ni kuhusu Taarifa ambazo zinazidi kusambaa katika Mitandao ya Kijamii hata Meseji za Kawaida kuhusu Kifo cha Msanii wa Bongo 

Flava, MATONYA.

Na Hii imeweza kuzua Maswali Mengi sana kuhusu kile ambacho Kimeweza kumkuta Mkali huyu wa vaileti na Mikwaju Mingine kama Vile DUNIA MAPITO, na Kadha wa kadha

·        Kutoka Kwa Wadau Wa Burudani
Moja kati ya Vitu ambavyo WAFUKUZA MAPEPO tumekuwa tukishindwa kujibu, ni Maswali kuhusu Kifo cha Msanii huyu Matonya, ambaye inaonekana kuna taarifa Fulani hivi zinazidi kuenea kuhusu Kufariki kwa Matonya.

Jana kunako Kipindi Cha jam Session, ziliweza kuingia SMS zaidi ya Kumi, ambazo zilikuwa zikiuliza kuhusu kufariki kwa Matonya, kama kuna Ukweli au lah, jambo ambalo lilitoa wazo la kuanza kutafuta undani wa Tukio hili, kwa Msaada wa Internet

·        Picha  Ya Matonya Imeonekana
KATIKA Hangaika za Huku na Kule, WAFUKUZA MAPEPO walikutana na Picha kunako Mtandao wa Instagram, kupitia account ya Mtu Mmoja anayefahamika kwa jina la ALMASI MZAMBELE (@almasmzambele) inayomuonesha mtu anayesadikiwa kuwa ni Matonya, akiwa amelala Chini akiwa Chakali bin taabani

Mtu huyo anaonekana akiwa amevalia CAR WASH Za Kisasa Nyekundu ya JORDAN-23, Boxer Nje Nje, Suruali aina ya Jeans-Nyeupe na Raba Nyekundu.

Katika Picha Hiyo, Mtu huyo aliandika Hivi;
Huyu ndio msanii MATONYA ambae kupitia picha hii imesababisha amezushiwa kufa leo hii, kiukweli mimi nampenda sana msanii huyu na ninazipenda kazi zake, Kiufupi jamaa anajua anachokifanya kwenye muziki. Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo tukio hili la matonya kukutwa amelala chini ktk mazingira ya aina hii si mala ya kwanza, swali ni je? kwanini msanii huyu mkubwa ambae amefanya makubwa katika muziki na anazidi kufanya makubwa mpaka sasa kujiingiza ktk ulevi wa kupindukia. Naomba tujadili kwa pamoja pia waweza kuwa tag watu 5. By ALMAS MZAMBELE BOSS OF ALL BOSSES

·        Kama Kweli Ni Matonya:
SASA, Kama Kweli Mtu huyo ni matonya, na hiuyo Picha Kweli inamuhusu Yeye, kwanini hali hiyo itokee kwa Msanii mwenye Heshima kali na Ya pekee kama Yeye?


Kuna Taarifa za uhakika kuwa matonya Yuko hai, lakini bado Hatujathibitisha kama kama Kweli Huyo ni Matonya, ukizingatia Simu yake haipokelewi baada ya Kujitambulisha Sie ni akina nani na Tuna Shida gani.

MNADA BANNER