REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

VIWANGO VYA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI SIKU YA LEO

2:36:00 AM Add Comment

KATIKA SOKO LA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI Nchini Tanzania, Kwa Viwango Vilivyowekwa na BENKI YA TANZANIA (BOT), Ni kama Ifuatavyo

FEDHA                                    INANUNULIWA  KWA..    INAUZWA KWA…

SHILINGI YA KENYA                18.71                              18.88
SHILINGI YA UGANDA            0.64                                0.65
DOLLA YA MAREKANI            1626.65                         1642.92
POUND YA UINGEREZA         2728.22                          2755.83
EURO                                       2244.29                          2267.06
YEN YA JAPAN                       15.86                              16.01
RUPIA YA INDIA                      26.62                              26.88
RANDI YA A.KUSINI                153.63                             155.10


UNADHANI MAKAHABA WAKISTAAFU, WANAELEKEA KUISHI WAPI?

2:33:00 AM Add Comment

KUNA Swali ambalo unaweza kujiuliza mpaka sasa, kwamba, Akina dada wanaofanya Biashara ya Ukahaba, wakishazeeka na Kustaafu, Nini hatma yao?

Mpiga Picha Mmoja nchini Ufaransa, maefanikiwa Kugundua mahali ambako makahaba wanaozeeka na Kustaafu Shughuli ya Kuuza Mwili, huko Nchini Mexico.

Katika Jiji la Mexico lililoko Nchi ya Mexico, Imebainika Nyumba Moja kubwa na Nzuri ambako Makahaba Wote wastaafu wanaishi hapo.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyoifikia Ijumaa Mseto, inasemekana Kuwa, Wastaafu wa Ukahaba wanaoingia Katika Eneo hilo, Ni wale tu, wanaoanzia Umri wa Miaka 50 na Kuendelea, na Wanapata Huduma Zote Muhimu sambamba na Vipodozi mbali mbali.


Jumba hilo lilifunguliwa rasmi Mwaka 2006, na mpaka hivi sasa, jumla ya Wazee zaidi ya 250 waliostaafu Ukahaba, wameshapitia eneo hilo.




HAKUNA KUFANYA MAPENZI MPAKA TUMALIZE WORLD CUP- KOCHA WA MEXICO

2:29:00 AM Add Comment

KOCHA wa Timu ya Taifa ya MEXICO, amewapiga marufuku wachezaji wa Timu yake Kushiriki Tebndo la Ndoa katika kipindi cha mashindano ya Kombe la dunia Mwaka huu Nchini Brazil.

Akizungumza na Gazeti la REFORMA, Kocha Huyo amedaiwa Kuwaagiza wachezaji wake kutokujihusisha na Suala la kufanya mapenzi, na badala yake wanatakiwa kujikita zaidi na kuelekeza Macho yao katika Soka hasa Michuano Hiyo ya Dunia

Aidha Kocha huyo anayetambulika kwa Jina la MIGUEL HERRERA, ameongeza kuwa, kama Mchezaji hatovumilia kutokufanya mapenzi kwa Mwezi Mzima ama Siku 20, basi hajajiandaa kuwa Mchezaji Professional.

Mexico Inatarajia Kukutana na Timu ya Brazili katika Kundi A, pamoja na Coratia na Cameroon

MASE AMPIGA STOP WIFE WAKE, KUINGIA KANISANI, BAADA YA KUKAMATWA KWA KOSA LA KUNYWA POMBE

2:20:00 AM Add Comment

NEW YORK,Marekani.
Nikema Praise The Lord Unasema ..AMEN, hiyo Ndiyo kanuni Yetu watu wa mungu tuliokoka, na kujitolea kumpenda Mungu kwa Nguvu Zote, haijalishi maisha tunayoishi lakini Hebu Sikia Hii Kutoka Kwa Ukaribu.

RAPPA na MCHUNGAJI Mase ambaye hivi majuzi tu Nilikupa Story kuwa anarejea katika game na Albam Mpya, Amempiga Stop Mke wake kuingia, ama kukanyaga, ama kulisogelea kanisa lake, ikiwa ni baada ya kukamatwa akiwa amelewa.

Awali kulikuwa na info kuwa, Baba Mchungaji Mase, pamoja na Mkewe ama mama Mchungaji TAWYLA BETHA walikuwa tayari kupeana Talaka, lakini baadaye ikasemekana kuwa wawili hao wamerudisha mahaba yao.

Mke Wa mase, aka mama Mchungaji, alikamatwa Mwezi uliopita kwa Kosa la Kupiga kilevi na kuendesha gari, jambo ambalo ni Kinyume cha Sheria za nchi ya marekani, na bila Ubishi, mke huyo wa mtumish Wa Mungu alipatikana na hatia.

Chimbua Chimbua katika kutoa Hitimisho, Ilmemimina Info kuwa, Mase aliamua kumpiga Stop Mamito wake huyo, baada ya kuliaibisha kanisa, na kusaliti Imani ya Mwenyezi Mungu.

HALELUYAAAAA

ILLUMINATA ANAHITAJI MENEJA.

2:16:00 AM Add Comment

DAR ES SALAAM, Tanzania,
Back in 255, Area Code ya SAY YES TO BABIES and SAY NO TO UZEE….
Rapa wa kike anayekuja in High Speed with Untouchable Flows, ILLUMINATOR, amemiminika na kusema kuwa Hivi sasa anahitaji Meneja ambaye ataweza kumsimamia katika kaz zake Mbali mbali hasa za Kimuziki, TTM Tushaidaka Kudadadeki.

Akifafanua kuhusu hilo Suala, ILLU ambaye ni best Friend Wa Miss Koi Koi, My Natty E, amesema kuwa Game la Muziki wa Kizazi kipya, Ni Gumu sana, Kiasi kwamba anahitaji kumpata Meneja ili kazi zake ziweze kusimama vilivyo, na aweze kutusua katika Music industry hapa Bongo.

Aidha Iluminator ambaye Remix ya JONI yak wake Yemi alade imemfanya kuwa Tofauti, pia amesema kwamba, watoto wa kike hawatakiwi kuogopa hasa katika Vipaji Vyao, hivyo wanatakiwa kujitokeza kwa Wingi katika Fani Hasa ya Production, ili kuweka heshima kama Zilivyo Nchi Nzima.


Tofauti na Kurap, Iluminator ni PRODUCER, ambaye huwa anafanya kazi zake Mwenyewe katika Studio zake za SWAHILI SWAGGZ RECORDS

JOH MAKINI IS COMING MAZEE

2:14:00 AM Add Comment

DAR ES SALAAM, Tanzania
Msanii wa rap nchini John Saimon aka Joh Makini Mwamba wa kaskazini kwa sasa anampango wa Video ya  wimbo wake unaofahamika kwa Jina la ‘I See You’ hivi karibuni …TTM, tumenyaka Infoz Pia.

Akimiminika Kuhusiana na Hiyo Ishu, Joh makini amesema kuwa, Mkwaju huo Mpya Utakita kunako Hewa Muda Si Mrefu, na umepikwa na Producer Nahreel.

Aidha Joh ambaye aliweza kuvibratisha Hisia za wadau wa Muziki wake kupitia kwaju la KILIMANJARO MOUNTAIN na BYE BYE pamoja na NIKUMBATIE, amesema Hivi sasa anasubiri Muda wa kushusha Noma hilo Ufike, ili aweze kutimiza kile ambacho watu roho inataka.


Pia Akizungumzia Kuhusu Video ya NIKUMBATIE, Makin maesema kuwa, Kwaju hilo ni Kali sana, Hivyo Video yake haitakiwi Kuwa ya Kitoto. So kwa hivi sasa Yuko anapepesa macho kumpata Director Mkali atakayesimamia Mzigo..

MNADA BANNER