REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TEKNO ATHIBITISHA KUPIGA SHOW MWANZA FEB. 13, 2016- "MWANZA, YOUR BABY IS COMING!!"

11:27:00 PM Add Comment
Tekno/Instagram
Na Baba Juti
HIT MAKER wa "Duro" TEKNO Kutoka Nchini Nigeria, anatarajia kupiga Bonge la Perfomance katika Jiji la Mwanza February Hii.

Kupitia Tamasha la MUZIKA FESTIVAL (Load To Jembeka Festival) ambalo limeandaliwa na STR8 UP VIBES na JEMBE NI JEMBE, Tekno akiwa na Msanii Seyi Sheyi Kutoka Huko Huko Nigeria, watapanda Jukwaa la JEMBE BEACH RESORT (Jijini Mwanza) February 13,2016, kwa ajili ya kuwa "kitu Roho Inastahili" Wakazi wote wa Jiji la Mwanza.

Kupitia Instagram account yake Tekno alitoa Taarifa "Mwanza, Your baby Is Coming"
Tofauti na Msanii Huyo, Wasanii wengine watakaoshusha Burudani ni Pamoja na OMMY DIMPOZ Pamoja na JUMA "NATURE" KASSIM "KIROBOTO"

Wasanii Kutokea Mwanza,watakaopanda Jukwaa Moja na Tekno, ni Pamoja na COYO MC, JIMMY CHANSA, YOUNG RAFA,JJ BAND-THE MAMBAZ na  DOGO D

Burudani na Mikuno Itashushwa na JEMBE DJS kutoka 93.7 JEMBE FM-MWANZA
Kiingilio ni Shilingi 10,000 Kwa Upande wa Kawaida, na VIP ni Shilingi 30,000.

Tamasha Hilo limepewa Nguvu na STR8 UP VIBES, JEMBE NI JEMBE, 93.7-JEMBE FM, JEMBE BEACH RESORT

STILL TOO COLD IN PARIS: TIZAMA PICHA 9 ZA SHILOLE AKIWA PARIS , UFARANSA

11:02:00 PM Add Comment









TUHUMA MPYA: FAIZA ALLY AANAMDAI MUIGIZAJI HUYU MILION 22?..GABO AMETAJWA

7:24:00 AM Add Comment
Faiza Ally/Instagram

Na Baba Juti
JIONI Hii wakati napita Pita katika Mtandao Wa Instagram, Nilifanikiwa kukutana na Post Hii ya Mzazi Mwenzake Na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mheshimiwa Joseph "Sugu" Mbilinyi, Faiza Ally,

Katika Ujumbe Huo, faiza, alionekana kulalamikia Mmoja kati ya Waigizaji wa Bongo Muvi, Kwa madai kuwa, amempatia Silingi Milioni 22 katika Muvi yake (Faiza) lakini Mpaka Hivi sasa, hajaipata na badala yake, hupewa Kalenda ya "Kesho"
Jackson anayedaiwa na Faiza Ally

Ingawa Black touchez hatujafahamu Kiundani zaidi Kuhusu hilo, lakini Tunaimani Kuwa, Huenda Hii BABY MAMA DRAMA, ndo Ikawa Kitu Husika ambacho Kinazungumziwa, maana Wiki kama 9 zilizokata, JACKSON alikuwa akipost Kuhusu Usahili wa Wahusika katika Filamu Hiyo

Nukuu:
Wewe kijana @jacksonkabirigi nimeweka milioni 22 kwenye movie yangu hlf unazarau na humalizii kazi yangu kila siku KESHO KESHO! Nasema nimechoka nakupa siku 3 tu!!!! Baada ya hizi siku kuisha utaenda kuozea jela! Hela zangu sio makaratasi najua na nimesikia kuwa huna utamaduni wa kumaliza kazi lkn kazi yangu utamaliza hata kwa kusimamiwa na walinzi! @jacksonkabirigi @jacksonkabirigi kwa kuwa huoni umuhimu wa mawasiliano basi kwa kupitia hapa naamini ujumbe utakufikia sasa ole wako usinipe kazi yangu kwa wakati - @farajikakingo @majagking @gabozigamba1 hawa watu naamini wana kujua na ujumbe utaupata........!

WEUSI HAWANA ACCOUNT WALA UKURASA WA FACEBOOK

6:06:00 AM Add Comment
Weusi/Google

Na baba Juti
Kupitia account yake ya Instagram, Nikki Wa Pili akiwakilisha kundi la Weusi, alitoa taarifa kuwa, Kundi La Weusi hawafanyi Biashara Yoyote Kupitia Mtandao wa Facebook.

Nikki alipost Screen Shot ya Ukurasa wa Facebook ambao unatumia Jina la JOH MAKINI-MWAMBA WA KASKAZINI, na kuthibitisha kuwa, Ukurasa huo ni Feki na kamwe hawafanyi Biashara katika Mtandao wa Facebook

NUKUU:
MATAPELI MATAPELI..WEUSI HATUFANYI BIASHARA YOYOTE KUPITIA FACEBOOK...UKI DILI NAO UMEPIGWA

UJAUZITO WA TATU KWA FLORA MVUNGI: KWANI KUZAA NI KOSA?, AU KUNA MTU NIMEMUOMBA HELA YA KUTUNZA WANANGU?

6:02:00 AM Add Comment
Flora Mvungi/Instagram

Na Baba Juti
TAARIFA ya Ujauzito wa Flora Mvungi, ikiwa ni Baada ya Kumaliza takriban Mwaka Mmoja tangia amejifungua Mtoto African, ilizua Gumzo balaa katika Mitandao ya Kijamii, hasa ikiwa ni baada ya H.Baba kutoa Taarifa Hiyo.

Maoni ya Wengi yalionekana kama kumuandama sana Flora Mvungi , Huku Wengi wakidai kuwa, alitakiwa apumzike Kidogo, na hiki Ndicho alichojibu.

NUKUU
"Hahahhahahahahhahaah nacheka kwa raha yaani nafuraha sana mana naona watu maneno yanawatoka kila kona..kwani kuzaa ni kosa?au kuna siku nimemuomba mtu hela ya kutunza wanangu??waja mna tabu sana,jamani hebu tusipangiane jinsi ya kuishi,,kingine siko nje ya ndoa na hata ingekuwa nje ya ndoa pia ni watoto wangu..mwakereka na nini??
Hhahaaaaaa yaani mtasema sana..
Khaaa hamuachi"

50 CENTS: MSITUMIE VINYWAJI VYA DIDDY...NDIYE ALIYEMUUA TUPAC

5:58:00 AM Add Comment
50 Cents/Google

Na Baba Juti
BIFU la Diddy na 50 Cents linaweza lisiwe la Kibiashara Tena, hasa Baada ya 50 Kukazia tuhuma ambazo zinamuandama Rapper P. Diddy Hivi sasa.

Juma lililokata, Taarifa Zilianza kuenea kuwa, kuna Askari wa Zamani wa Jeshi la Polisi Nchini Marekani, Los Angels-LAPD, ambaye ametoa Ushahidi kuwa, Rapper Sean Combs-P. Diddy, alitoa USD Million 1 kwa ajili ya kuhakikisha Mauaji ya TUPAC yanafanyika.
Sean "Puff Dady" Combs/Google

Ushahidi huo ambao umepatikana katika Documentary ambayo inaandaliwa, kuhusu Mauaji ya Pac na Biggie, ndiyo ilyozua kizaa zaa, mpaka 50 akaanza kumchokonoa Hivyo.

Kupitia Snap Chat account yake, 50 alipost Video Clip ambayo inamuonesha akimshutumu na kushangazwa na Taarifa za Diddy Kumuua Tupac.

Tofauti na Hilo, 50 aliingia katika account yake ya Instagram, na kupost picha ya Diddy, Biggie na Tupac na kuandika kuwa, "no Puffy Juice, He Killed Your Favourite Rapper"

MAJIBU YA DIDDY.

Mpaka Hivi sasa, Diddy hajajibu Chochote kuhusu Tuhuma Hizo, ingawa Mashabiki zake bado wanamuomba azungumze chochote kuhusu Madai Hayo.

JOSEE CHAMELEONE: TUHESHIMIANE.. NINALIPIA KODI

5:44:00 AM Add Comment
 
Jose Chameleon/Google

Na Baba Juti.
BLOGS zimeanza Kumuandama Tena Jose Chameleone licha ya Kuzichimba Mkwara Mzito.
Safari , Hii, Moja Kati ya Bloggs za Kidaku Nchini Uganda, ilipost Taarifa Kuwa, Josee ni Msanii ambaye halipi Kodi, jambo ambalo limemfanya Akamatwe
.


Kupitia Ukurasa wake wa Facebook, Chameleone ambaye alionekana Kukerwa sana na taarifa hiyo, aliandika kuwa, watu wale wale (blog) ambayo iliandika Taarifa ya Uwongo kuhusu utata ulipo baina yake na Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA), wamerudi tena na taarifa hizo hizo za Uwongo kuhusu yeye kukwepa kulipa Kodi

Lakini Tofauti na Hilo , Jose Chameleone aliongeza kuwa, Blog Hiyo imetumia maneno korofi ambayo yanamkwaza

Hivyo anaomba kila Mtu amuheshimu Mwenzake, Maana analipia Kodi kama inavyotakiwa.
Tembelea Instagram account yangu @babajuti

PICHA & VIDEO. HUYU NDIYE CHUI ALIYEINGIA SHULENI NA KUJERUHI WATU 6

5:31:00 AM Add Comment
 CHUI Mkubwa alivamia Shule ya VIBGYOR (VIBGYOR INTERNATIONAL SCHOOL) iliyoko Kundalahalli iliyoko Bangalore- India, na Kujeruhi watu 6








MNADA BANNER