REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

EXCLUSIVE : SHEIKH FARID AHMED ALIYEANZISHA FUJO ZA UAMSHO ZANZIBAR, AACHIWA HURU

1:46:00 AM Add Comment

Sheikh Farid Hadi Ahmed  mmoja kati ya viongozi wa ngazi za juu wa UAMSHO visiwani Zanzibar nchini Tanzania  ameachiliwa huru jana usiku, baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi la nchi hiyo kwa muda wa siku tatu. 

Taarifa kutoka Zanzibar zinasema kuwa, Sheikh Farid Hadi Ahmed amethibitisha mwenyewe wakati  alipowaambia waandishi wa habari jana usiku  kwamba,  askari kadhaa wa jeshi la polisi ndiyo waliomkamata siku ya Jumatano usiku, na kumpeleka mahala asipopajua kwa mahojiano. 

Wakati jeshi la polisi likiendelea kumhoji kwa siri kiongozi huyo wa UAMSHO,  Mussa Ali Mussa Kamishna wa Polisi Zanzibar aliviambia vyombo vya habari kuwa,  jeshi hilo halifahamu mahali alipo kiongozi huyo, na kwamba litaendelea na zoezi la kumtafuta. 

Kutoonekana kwa Sheikh Farid Hadi kulipelekea kuibuka ghasia na vurugu mjini Zanzibar, na  kusababisha  askari mmoja wa jeshi la polisi kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Hapo jana baada ya mshuko wa sala ya Ijumaa, askari polisi walipambana na Waislamu wenye hasira  katika maeneo ya Mji Mkongwe Town wakilalamikia kutoonekana kwa kiongozi wao.

MISS KARUNI aichafua campu mulla

1:17:00 AM 1 Comment



Haya, safari Hii Ni kwa Huyu Mkenya na Mrembo anayejiita BIKRA KUTOKA KENYA, Ndani ya Kikundi ch a CAMP MULA, Miss Karun. Hebu Muoneni alivyofanya.

MNADA BANNER