REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

RIHANNA NA SHAKIRA KUELEWEKA JANUARY 13…

1:49:00 AM Add Comment

KAMA utakuwa unakumbukumbu Nzuri, Hope utakuwa unaelewa kuwa COLLABLE ya Shakira na BEYONCE “BEAUTIFUL LIAR” ilisumbua Vibaya sana
Sasa basi, TEAM TUKO MBELE Tumepokea data Kuwa, Shakira Huyo huyo ambaye Umemmis muda Mrefu sana, anakuja Once Again ndani ya Collable na Rihanna “Riri”
Track Hiyo ambayo inatarajiwa Kuachiwa rasmi JANUARY 13 mwaka Huu, itabeba TITLE la “CANT REMEMBER TO FORGET YOU”, na Itapikwa Kunako Studio za Rock nation huku Wengi wakitarajia kuwa “The Colombian Hot Chick” SHAKIRA atafanya utuindu wake Ule ule, si Kwenye Audio Tu, bali hata Kwenye Video.

Hii Itakuwa Ni Track ya Kwanza kwa Rihanna Ikiwa ni Ndani ya Mwaka 2014, wakati SHAKIRA kwake itakuwa Ni Track ya Kwanza tangia ajifungue Mtoto wake wa Kwanza,

Pia Single Hiyo inatarajiwa Kupatikana Kunako ALBAM ya Shakira ambaye alivunja Balaa katika Beatiful Liar ya Beyonce Mnamo Mwaka 2007, na Kushika nafasi ya 3 katika Chart za BILLBOARD 100

MTOTO WA MIAKA 12 AMSHANGAZA JAY Z…

1:45:00 AM Add Comment

WAKATI MSODOKI “YOUNG KILLER” akishangazwa na Mtoto wa Kitasha Kutoka USA akipita na Mistari yake ya JANA  NA LEO alomshirikisha QUICK RACKA na STAMINA, Jayz Imemtokea akiwa On Stage baada ya Mtoto mmoja anayesadikika kuwa na Miaka 12 Kupita na Mistari ya Track ya CLIQUE
Tukio Hilo Limetokea wakati Jigga Baba Blue Ivy alipokuwa katika Tour yake ya MAGNA CARTER WORLD TOUR huko GREENSBORO, ambapo Fan Wake huyo Mtoto aliyefahamika kwa jina la JUSTIN, alionesha Ishatra zilizoeleza kuwa NINAWEZA KURAP KWA AJILI YAKO
Baada ya Jay Z Kumuita Bwana Yanki Huyo kwa Stage, watu Wengi walionekana Kushangilia sana na Kupiga Kelele Nyingi wakiashiria kuwa Dogo kavuta Hisia zao kwa Ujasiri aliouonesha.
JUSTIN alipokabidhiwa MIC Tu, basi alianza Kupita na Acapella ya CLIQUE huku watu wakipiga Kele Zaidi.
Aidha wakati Dogo anaendelea, JIGGA alimuambia Bwanamdogo Huyo Kutokuflow Ile Mistari inayohusu MADAWA YA KULEVYA, badala yake arudi kule kwenye Kunakozungumzia Numbers, jambo ambalo Justin Hakulaza Damu.

Lakini baada ya Jay Z kumshukuru Yanki huyo na Kumpa Bonge la Hug, Still Justin alionesha kutoridhishwa na Kumchania mistari tu, bado aliomba akutane naye Back Stage, jambo ambalo JAY Z hakulitolea Nje

DMX MZUNGUMZIA EMINEM, PAMOJA NA KUWA MCHUNGAJI

1:39:00 AM Add Comment

WALA USISHTUKE, labda DMX ameoneshwa Ishara kadhaa na Mwenyezi mungu baada ya kuziomba kupitia Track yake ya Kipindi Cha nyuma ya LORD GIVE ME A SIGN
Kupitia Interview na 359 HIP HOP, DMX alipata nafasi ya Kuzngumzia masuala Kadha wa Kadha kuhusu Muziki wake pamoja na Mengineyo.
KUHUSU MABADILIKO KATIKA RAP GAME
DMX ambaye hivi sasa ameamua kurejesha Heshima yake ya kipindi cha awali, amesema kuwa Gemu hivi sasa limebadilika kwa Kiwango kikubwa sababu kumekuwa na watu Wengi, ambapo kati yao wanafanya Vizuri sana huku wengine wakifanya mafyongo. Lakini Ndivyo game lilivyo, lazima Changamoto kama hizo Zitokee..
MAHUSIANO YAKE NA EMINEM, PAMOJA NA KUJIITA MUNGU WA RAP
Kipindi Kirefu Kidogo kumekuwa na Uhusiano Usio mzuri baina ya EMINEM na DMX, jambo ambalo wengi wamekuwa wakisubiri Muafaka
Lakini akizungumzia Juu ya Hilo, DMX amedai  Anafahamu kuwa Eminem Ni Msanii Mwenye Kipaji, na wanamahusiano mazuri. Pia DMX amesema kuwa hatotaka Kusikia akilizwa kuhusu Beef lake na Eminem
KUHUSU KUWA MCHUNGAJI.

Katika Hilo, Eminem Amesema kuwa anaamini katika Imani yake, na Atakuwa Mchungaji katika Kutoa Taarifa Mbali mbali hasa Za Mwenyezi Mungu pamoja kuepukana na Masuala ya Kisheitwaini

MNADA BANNER