REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WHAT'S NEW TODAY: JUX AMETULETEA "AFRICAN BOY 2017" AMBAZO ZINAONEKANA HIVI

5:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu hakuna kitu kitamu na kinavutia kama kuona Vijana wa Kitanzania wanapiga "Mihanyo" yao na kujikita katika Ujasiliamali Mrefu

Off Course Every Body Knows about Frican Boy Collection ambazo zimekuwa zikichukua nafasi kubwa katika Soko la mavazi hapa Nchini tanzania


Ila Kupita "WHAT'S NEW TODAY" ndani ya Mnada, Msanii JUX ameshusha Collection Nyingine (AFRICAN BOY COLLECTION 2017) kwa wale ambao mnapenda sana African Boy Brand

Bei zake Ni Kama Ifuatavyo:    
TSHIRT 35,000/= Tshs
VEST : 35,000/= Tshs

KOFIA : 25,000/= Tshs




TUMEVUJISHIWA !!!!! : COYO AMEJIBU HAPA KUHUSU KUVURUGANA NA MENEJA WAKE KID BWAY (AUDIO)

5:15:00 AM Add Comment

 
SOURCE : JEMBE FM  
#WatuWaMungu Kuanzia Eid Mosi, kuna Kitu kilikuwa kinazunguka Huku na Kule kama Mlikuwa hamjui, na kwa Bahati Nzuri na sie tukapenyezewa Hii Info

Ishu Kubwa ilikuwa inamhusu COYO (Zamani Coyo Mc) ambaye hivi sasa anafanya Vizuri na Mkwaju wa ZIWAFIKIE

Tulipenyezewa Ujumbe Mfupi wa Maandishi na Moja kati ya Wadau ambao Ulikuwa unafafanua Hivi
" Mambo Vipi Baba Juti. Heri ya Sikukuu ya Eid Mzee Mwenzangu Naitwa REUBER ZOLA BOY (Jina Langu Lifiche tafadhari). Niko Dar Kwa Hivi sasa ila ni Mkazi wa Mwanza. Tangu nimekuja Dar, nimefanikiwa kuwa Karibu na Wasanii wa Mwanza na hata kujua kila ambacho wanakifanya Mzee Mwenzangu. Sasa, mlishawahi kufanya Interview hapo JEMBE FM na Coyo, mkamuuliza kuhusu Mahusiano yake na Meneja wake. Kiukweli, hapa nilipo, niko Na Wasanii kutoka Mwanza, tunakula Mambo Yetu Kidogo... nawasikia wanasema eti COYO MC katibuana na Meneja wake, yule KID BWAY.. Ishu kubwa ni Mkwanja..eti Coyo MC hajalipwa Chochote tangu ameachia Track zaidi ya kuvalishwa Manguo, kupigishwa Picha za Art Work, kusaidiwa Mahali pa Kuishi na mengineyo. Na huyu anayeongea ni mmoja kati ya Wsanii ambaye alishawahi kupita Mikononi mwa Kid Bway, wakatibuana...sasa, hebu Muulize Coyo kama Ni Kweli. Mzux Mzee"

Sasa Baada ya Kukutana na Message Hiyo, tukasema ngoja tumsake COYO Mwenyewe ili afunguke Vizuri kabisa... Na Yeye akazungumza kama Ifuatavyo


AUDIO : THE KISSER STRAWBERRY X FUTURE JNL - MONEY ( BONUS TRACK)

3:24:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu kutoka Mwanza, anaitwa The Kisser Strawberry ambaye ameshusha Bonus Track Hii inayoitwa MONEY. Amemshirikisha Future JNL... Isikilize na Kisha Uipakue

BOBI WINE : MIE NI MSHINDI TAYARI...NASUBIRI KUTANGAZWA

3:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
SOURCE : URBAN TV-UGANDA  
#WatuWaMungu Mkali wa Dance Hall Nchini Uganda BOBBI WINE amedai kuwa, yeye Ni Mshindi tayari, na anasubiri tu Kutangazwa

Akizungumza kwa Ujasiri Kabisa, Bobbi Wine ambaye Jina lake katika Passport ni ROBERT SSENTANI KYAGILANYI amesema kuwa Hivi sasa anatarajia tu kutangazwa, Maana yeye ni Mshindi tayari

katika matarajio Yake, Bobbi Wine ameahidi kuleta Umoja na Nguvu kubwa kwa wananchi ambao tayari walikuwa wameshakosa matumaini ya Umoja wao


AMANI: MIE NI MKE WA MTU HIVI SASA

2:33:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu THE GOOD NEWS ni kwamba AMANI kutoka Nchini Kenya Hivi sasa ni Mke Wa Mtu !!!

Cecilia Wairimu Maarufu kama Amani, alithibitisha Hilo hasa kuolewa na Mfnayabiashara Kutoka Nchini Nigeria anayefahamika kwa jina la Chinasa Udeala, na Ndoa yao Ilikuwa ni Ya Siri Sana


Awali zilikuwa zinasikika tu Kichini Chini kuwa Amani ambaye ni Ex- wa AY, aliyewahi kuvuma na Mikwaju kama Vile MISSING MY BABY, USINDE MBALI, na BAD BOY, amekuwa katika Mahusiano ya Kimya Kimya na Mwanaume Kutoka Nchini Nigeria, kitu ambacho alikuwa hajawahi kukizungumzia hata Kidogo

Tunamnukuu
" Kila Kitu kimekamilika> Nimeshaolewa Tayari, na ni mke wa Mtu sasa Hivi. Najua Watu wengi wanatamani kuona Ndoa Yangu ilikuwaje, lakini mie Ni Mtu Msiri sana katika Mambo yangu Binafsi> Ndio maana hunioni nikifanya Interview katika Nyumba yangu ama katika Vitu vyangu vya ndani"

Katika hatua Nyingine, Amani amesema kuwa Mume wake huyo ni Mtu ambaye anapenda, anamjali na hata kumuonesha mahaba ya dhati.

Akizungumza kuhusu Kuchumbiwa, Amani anadai kuwa, Tukio hilo lilifanyika Mwaka Jana

 Tunamnukuu
" Siku Hiyo ambayo sikuiotarajia, alinichukua na kunitoa out kwa ajili ya Chakula cha Jioni. Tulikuwa wawili tu, akapiga Goti, akaniuliza swali hilo na kunipa Pete Hiyo"

Lakini Kuhusu Mume Wake huyo kumruhusu ama kufurahia Maisha na shughuli za Kimuziki za Amani, Bibi huyo alisema Hivi

"Kiukweli kabisa, hana tatizo na mie kufanya Muziki. Ila ilifikia Muda nikahisi kabisa kuwa ninahitaji kujikita katika Biashara zangu. Na ninahitaji Muda Pia kwa ajili ya Familia yangu na ninahitaji Muda kwa ajili yake"



DAH !!!: MNAOPENDA KUTUMIA APP ZA MAPENZI...KUNA HILI LINAWAHUSU

1:37:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Binti wa Miaka 18 amehukumiwa Kifungo cha Miaka 20 Jela baada ya Mahaklama kubaini na kuthibitisha kuwa alihusika katika Wizi na kumpiga Risasi Kijana Mwenzake  Kupitia App ya Mahusiano ya Kimapenzi.

Hakimu MATTHEW FOXMAN  kutoka CENTRAL CALIFONIA, alitoa Hukumu Hiyo kwa Mshtakiwa huyo anayetambulika kwa jina la KY'ANDREA COOK, na kuiacha Familia yake akiwemo mama yake Mzazi ikilia na kuhuzunika kwa Uchungu

Taarifa kamili zilifafanuliwa Kuwa, Mnamo mwezi March mwaka 2017 Ky'andrea akiwa ni Mwanafunzi wa MAINLAND HIGH SCHOOL Huko Huko Nchini Marekani, alimrubuni Kijana mwenye Miaka 27 kupitia Mtandao wa unaopatikana katika Smartphone "MEET ME " ambao ni maalum kwa Mahusiano.

Katika Makubaliano yao, Wawili hao walikubaliana kukutana katika eneo linaloitwa SOUTH DAYTON, ambapo Jamaa huyo anayetambulika kwa jina la PERRY NIDA alitarajia kumuuzia Bangi na kisha Kwenda kufanya Tendo la Ndoa kama ambavyo walipanga.

Lakini kama unavyojua Michezi hii ya Sikufahamu , hunifahamu, Jombaa Nida aliamua kumtanguliza Kijana wa Miaka 17 anayeitwa IMANNUEL PURSEL kama "Chambo", na Ndipo Chambo huyo alipopigwa Risasi na Boyfriend wa Mshtakiwa ambaye alikuwa akisubiri kuwaibia kama ambavyo walikuwa wamekubaliana na Mshtakiwa

Mama Mzazi wa Mshtakiwa alimwaga Kilio Mahakamani wakati Binti yake anapelekwa Rasmi Gerezani.

Kijana aliyepigwa Risasi Hali yakle inaendelea Vizuri sasa Hivi....



MNADA BANNER