REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UPO HAPO!?: REMY MA KASEMA KUWA HUWA HAMFIKIRII MSANII YEYOTE AKIWA ANAANDIKA WIMBO, MAANA HAILETI MAANA YEYOTE KWAKE

12:59:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
WATU Wa Mungu kama mmepata Bahati ya kusikiliza Brand New Sh**t ya Remmy Ma Na Lil Kim, basi kuna namna ambavyo utakuwa uatafakari hasa kile ambacho umekisikia  ndani yake

Collable hiyo ambayo imepewa jina la WAKE ME UP ilikuwa ikisubiriwa kwa hali na mali, ukizingatia REMY MA na LIL KIM ni Wakongwe na wana historia zao katika Upande wa Hip Hop kwa Wanawake, maana hata Uzito wa Mashairi yao huwa ni balaa kupita maelezo

Lakini baada ya Kuachiwa, kuna baadhi ya waungwana walipongeza kile kilichofanyika lakini kama kawaida ya wengine, waligundua makosa mengi na hata kudai kuwa Mzigo huo sio mkali hata kidogo maana hakuna ukubwa wowote

Baadhi walianza kumponda Remy Ma wa sasa Hivi na Lil Kim wa sasa hivi wakidai kuwa Makali yao ya kipindi cha Nyuma yamepewa changamoto kubwa sana na kizazi kipya cha Female Emcees.

Sasa kubwa zaidi, watu walidai kuwa, Mkwaju huo moja kwa moja umemlenga Nicki Minaj ukizingatia wote wawili, yaani Remy Ma na Lil Kim waliwahi kuingia katika Msuguano mkali sana na hata hivi sasa bado kuna kila chembe chembe ya uhasama Juu yao

Katika kuliweka Sawa Jambo Hilo, Remy anadai kuwa ameshachoka kusikia kuwa kila baadhi ya Track atakazofanya zinamdiss Nicki Minaj. Hata kama ameshirikiana na Lil Kim, bado anavutiwa na namna ambavyo wawili hao wamefanya kazi. Hivyo kwa upande wake, akiwa anaandika wimbo na hata kuurekodi mpaka kuuachia, huwa hamfikirii msanii wa kike ama kumchana mtoto wa kike. yeye anachokifanya, ni kile ambacho wasanii wengi kama vile Jay Z, J Cole, Kendrick Lamar na wengine watamsifia na kusema kuwa , daah huyu Demu ni balaa. Hivyo huwa hafikirii kabisa Jinsia yoyote ile hasa ya Kike, sababu haileti Mantiki yoyote Kukichwa Chake

HUYU NDIYE MWAFRIKA SASA !!!: LUPITA ACHUKIZWA KUFANYIWA PHOTOSHOP

12:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
KAMA kuna baadhi ya Binadamu ambao wanavutiwa sana na Photoshop na hata kulazimika kufanya kila wawezalo ili wawe na muonekano tofauti na wa kwao, basi hii ni tofauti kwa Bini huyu ambaye ana asili ya Kenya

Mkali w Filamu kutoka Hollywood, LUPITA NYONG'O ameamua kung'aka vya kutosha baada ya Jarida GRAZIA UK kumfanyia Editing ambayo hakufurahiwa nayo katika Front Cover yao.

Kwa mujibu wa amalalamiko ya Lupita Nyong'o ambaye alivuma sana kunako Filamu ya 12 Years A Slave, Jarida hilo lilimuomba kwa ajili ya kuonekana katika ukurasa wa mbele kabisa , na yeye hakuona hiyana, ila wamemchefua zaidi baada ya kumfanyia Photoshop ambayo anaamini kabisa imeuficha uhalisia wake

Lupita aliongeza kuwa, Wahusika wa jraida hilo, waliweka Ngozi ya Kung'aa sana tofauti na Ngozi yake ambayo ni Nyeusi kiuasilia, lakini pia walimfanyia photoshop kwenye muonekano wa Nywele zake, kwa kuondoa zile alizokuwa nazo, na kubadilisha kabisa kwa kuweka za kwao ambazo walizitaka, kitu ambacho hajavutiwa nacho hata kidogo

Lupita ameongeza kuwa , ingawa hakupewa taarifa za kufanyiwa marekebisho hayo, bado hatokubali hata kidogo kwa baadhi ya watu wachache wanaojaribu kuficha urithi wa mtu hasa kiuasilia maana ni kama kupoteza ukweli na kujaza watu uwongo

MNADA BANNER