REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA: MEYA JERRY SLAA ALIVYOFUNGUA OFIS MPYA ZA MULTICHOICE KARIAKOO

11:53:00 PM Add Comment






HABARI ZA ASUBUHI : NAPENDA SANA KILIMO JAMANI, BASI TU NINASHI TOWN

11:37:00 PM Add Comment



BAN KI MOON: BIASHARA YA MAGENDO YA BINADAMU

11:27:00 PM Add Comment


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka zifanyike juhudi zaidi kwa shabaha ya kupambana na magendo ya binadamu ulimwenguni.

Ban Ki moon amesema kuwa, kuna udharura wa kuwepo ushirikiano kati ya nchi, asasi na taasisi zote ulimwenguni kwa shabaha ya kukabiliana na vitendo hivyo hatari kwa amani na usalama wa dunia.

 Amesema kuwa, magendo ya binadamu huharibu uchumi wa mataifa, kwani mapato ya mabilioni ya dola yanayotokana na biashara hiyo haramu, hutumiwa katika muamala wa kununua na kuuza madawa ya kulevya na jinai nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Kupambana na Jinai na Mihadarati  ya Umoja wa Mataifa  iliyotolewa mwaka 2012, watoto wadogo wanaunda  moja ya tisa ya wahanga wa magendo ya biashara ya binadamu ulimwenguni kote kati ya mwaka 2007 hadi 2010.

MALI: JESHI LAWAFUATA WAASI

11:18:00 PM Add Comment


Vikosi vya jeshi la Mali hii leo vimeelekea kwenye mji wa kaskazini mashariki wa Kidal ikiwa ni kabla ya muda uliopangwa na serikali wa kuukomboa kutoka katika mikono ya waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga

Vikosi vya Ufaransa vilivyokuwa vikipambana na waasi kaskazini mwa Mali viliwaruhusu waasi wa MNLA kudhibiti mji wa Kidal katika miezi ya hivi karibuni, lakini serikali ya Mali inataka kuudhibiti mji huo kabla ya uchaguzi wa rais na Bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai. Waziri wa Ulinzi wa Yamoussa Camara alisema bungeni mwezi huu kwamba, swali kuhusiana na kudhibitiwa mji wa Kidal na waasi wa MNLA litajibiwa ifikapo Mei 15.

Waasi wa MNLA walikataa wito wa serikali ya Bamako wa kuweka chini silaha, wakisema kuwa watakabiliana na jitihada zozote za serikali za kudhibiti tena mji wa Kidal, lakini walisema mlango wa mazungumzo ya kisiasa na serikali upo wazi.

Katika upande mwingine Rais wa Chad ametangaza kuwa, askari wa nchi hiyo waliokuwa wakipigana nchini Mali na makundi ya waasi, wanaanza kurejea nchini kwao.

MNADA BANNER