REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MARIAH CAREY HATIMAYE AMEIUZA PETE YA UCHUMBA ILIYOZUA MGOGORO

2:56:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
HATIMAYE Mariah Carey amefikia uamuzi mzito wa kuuza pete ya Uchumba ambayo alivalishwa na aliyekuwa mchumba wake, Bilionea James Parker 

Kama ulikuwa hufahamu, James Parker alimvalisha Mariah Carey Pete hiyo yenye thamani ya USD Milioni 10 mwaka jana, walipokuwa katika mahusiano ya kimapenzi huku kukiwa na fununu ya kuwepo kwa ndoa ya kifahari, lakini mwisho wa siku ilishindikana baada ya wawili hao kuingia katika mgogoro

Baada ya vuta nikuvute za huku na kule, James Parker alihitaji arudishiwe pete yake ya uchumba, lakini Mariah Carey aligoma kata kata na mahakama kumkubalia kuwa Mariah abaki na Pete hiyo

Sasa Taarifa ambaoz tuko nazo mpaka hivi sasa, ni kwamba, Mariah Carey na Management yake, wameamua kuiuza pete hiyo kwa mkwanja wa hasara kabisa ambao ni USD Milioni 2.1 kwa moja ya duka ambalo hujihusisha na Biashara za vito vya thamani

Hiyo pia inaripotiwa kuwa, Mariah alifikia uamuzi huo sio kwa sababu ya njaa zake, la hasha, bali ni kwa sababu alitaka kufutilia mbali kumbukumbu za Ex wake huyo


NYOSHI EL SADAAT: "SIKUMBALIANI NA UCHUNGUZI WA MADAKTARI, NISAMEHEWE"

2:34:00 AM Add Comment

Na Hezron Munis : SOURCE: Mtanzania Digital 
#WatuWaMungu chezeeni kote ila msichezee vitoweo maalum vya watu, maana unaweza kujikuta ukiwaumiza kwa namna moja ama nyingine pale unapozungumzia Kitoweo chao kwa njia tofauti kabisa

Kipindi cha Nyuma kidogo, ilikuja kuwekwa wazi kuwa Mnyama Nguruwe husababisha Ugonjwa wa HOMA YA NGURUWE ikiwa ni baada ya maradhi hayo kuonekana na madaktari kuthibitisha tatizo hilo kuwepo na hata kuanza kupiga marufuku ulaji wa Nyama hiyo usio salama, lakini bado waungwana walikula

Sasa Safari hii, imekuja kubainika kuwa Ugonjwa wa Ebora unasababishwa na Mnyama anayeitwa Nyani, na Mnyama huyo huwa ni kitoweo kwa Wale raia wa Nchi ya Kongo

NYOSH EL SADAAT, Ex member wa FM ACADEMIA ambaye pia ni Mzaliwa wa Kongo, ameonekana kuwa na shaka juu ya uchunguzi wa madaktari ingawa hapingani nao hasa kuhusu kitoweo cha Nyani

Kwa msisitizo zaidi, Nyoshi alisema kuwa yeye kama yeye anagonga fresh tu nyama ya nyani na anashindwa kuelewa kwa nini madaktari wanasema inasababisha ugonjwa wa Ebola ili hali nyama hiyo ilikuwa ikitafunwa vzuri tu tangu enzi za mababu

QUEEN DARLEEN-"MIMI NI MWANAMKE, NINA HISIA PIA"

2:18:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi 
#WatuWaMungu tunaamini kabisa wengi hamjapata kumsikia Queen Darleen akizungumzia Mahusiano yake ya kimapenzi na hata kupost picha za kimahaba mahaba akiwa na Boyfriend wake

Hii imekuwa ikitoa maswali mengi tu kuhusu Maisha ya Queen Darlee ambaye hivi sasa yuko chini ya Record label ya WCB, hasa katika masuala ya kimahusiano huku wengi wakidai kuwa bibie huyu ni kauzu sana kiasi kwamba ni ngumu mwanaume kumuingia kirahisi na kumtamkia hisia zake

Ukiachilia mbali ukauzu, Wengi huhisi kuwa Hit Maker huyu wa Track ya MANENO MANENO ni mkorofi sana kiasi kwamba hata akiwa katika mahusiano huenda akaonesha ubabe na hata kumfyatua makonde Mpenzi wake

Lakini kwa upande Queen Darleen, amedai kuwa yeye ni Mwanamke kama walivyo wengine na ana hisia za kimapenzi pia. Hivyo kama akitokea mtu ama mwenyezi Mungu akambariki mchumba, basi ataolewa

"NIMECHUMBIWA MARA 3, NA BOYFRIENDS ZANGU WANNE KUOMBA NIWAZALIE WATOTO"- NICKI MINAJ

1:56:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu hakuna mtu ambaye huwa ankutana na changamoto nyingi sana chini ya Jua hili kama Mtu maarufu katika sekta yoyote ile ile, lakini anafahamika tu katika kona mbali mbali

NICKI MINAJ ambaye aliamua kuisogeza album yake aliyoipa jina la QUEEN mpaka AUGUST 10, inawezekana kabisa akawa ameamua kuhusisha Nyimbo nyingi za kuwahamasisha akina mama kuwa imara na kuepukana na unyanyasaji ambao unafanywa na baadhi ya wanaume hasa katika mahusiano yao ya kimapenzi ama ndoa

Katika kuwahamasisha zaidi wanawake hasa kutambua umuhimu na hadhi yao kwa wanaume, Nicki Minaj ametweet kuwa amewahi kuchumbiwa na wanaume watatu kati ya wote ambao amekuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi, huku wanne wakimtaka wazalie mtoto, kitu ambacho hakuona umuhimu wake na badala yake akaamua kutolea nje

Tunamnukuu

"Tambua thamani yako. Nimechumbiwa mara 3, Boyfriends zangu wanne waliniomba niwazalie watoto. Kihisia, kiakili na kimwili nimeonewa na kudhalilishwa. nilionesha tabasamu la uongo ingawa sikuwa na furaha.  Nimedhalilishwa, nimeonewa sana"


MNADA BANNER