REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANAMKE AKAMATWA NA BUNDUKI....

10:17:00 AM Add Comment
IGP Said Mwema

SHINYANGA


Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Salumu Msangi alisema kuwa mwanamke huyo, Hollo Mabula (28), alikamatwa Novemba 5 usiku saa tatu nyumbani kwake katika Kijijji cha Ng’wang’wali, Kata ya Mwaswale.

Alisema kuwa mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa mmoja wa majambazi, alikamatwa na bunduki hiyo aina ya G.3 ikiwa na risasi zake 35 na risasi zingine 99 za SMG ambazo pia zinaweza kutumika katika bundukia aina ya SAR, alizokuwa amezihifadhi nyumbani kwake.

Kamanda alifafanua kuwa bunduki hiyo ilikuwa imefichwa chini ya uvungu wa kitanda chake ikiwa na idadi hiyo ya risasi na zingine zikiwa zimewekwa ndani ya soksi na kutundikwa juu ya dari.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiitumia silaha hiyo iliyofutwa namba zake katika vitendo vya ujambazi na ujangili ndani ya hifadhi ya Serengeti, Maswa Game Reserve na maeneo mengine.

Kamanda alifafanua kuwa, hata mume wa mwanamke huyo, Masanja Maguzu, aliwahi kukamatwa na bunduki ya SMG na risasi 622 na kufungwa jela miaka 15.

PADRI KUBURUZWA MAHAKAMANIA

9:42:00 AM Add Comment
Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Nchini Tanzania, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo



 TARIME, Musoma
PADRI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Nyamwaga, wilayani hapa, huenda akafikishwa mahakamani kwa madai ya kupora ardhi ya mwanakijiji mmoja, John Zacharia.

Kwa mujibu wa notisi ya siku 30 iliyotolewa na wakili wa mwanakijiji huyo, Mwehozi Charles kutoka kampuni ya sheria ya Nola, mteja wao atalazimika kumshitaki padri huyo kwa kukiuka makubaliano ya awali kati ya pande hizo.

Notisi hiyo inasomeka kuwa, pande hizo zilikubaliana kuelewana nje ya mahakama katika kesi ya msingi Na 58/2011 katika baraza la ardhi wilayani hapa, ambapo baada ya kufikia makubaliano ilikubaliwa kuwa padri huyo angefidia ardhi na miche ya kahawa 350 iliyokuwamo.

Zacharia alidai kuwa baada ya kufikiwa makubaliano hayo, hakutekeleza na badala yake akavamia eneo hilo na kuharibu miche hiyo na kuhamishia mawe na mchanga eneo hilo bila fidia yoyote, hali iliyosababisha hasara kubwa tofauti na makubaliano ya awali.

Inasemekana kuwa juhudi za kumchukulia hatua za kisheria paroko huyo katika kituo cha polisi Nyamwaga hazijafua dafu kutokana na kukaidi wito kutoka kwa mkuu wa kituo.

Alipotafutwa na gazeti hili, paroko huyo alidai hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa yeye si msemaji wa kanisa hilo, bali atafutwe askofu wa Jimbo la Musoma.

WALTER CHILAMBO MSHINDI WA EBSS 2012

9:05:00 AM Add Comment
 MSHINDI WA EBSS 2012 WALTER CHILAMBO
 CHIEF JUDGE Wa Mashindano Hayo, RITHA PAULSEN

 MCs Wa Fainali Hizo CAESAR DANIEL na VANESSA MDEE

 TOP 5 Walioingia Fainali ya EPIC BSS 2012


SALAMA JABIR "Sala Jay"

MNADA BANNER