REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

YOUNG DEE: " MADEE NAKUPENDA SANA DINGI !! "

1:02:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
WAUNGWANA wengi wanafahamu kuwa kumekuwa na maneno ya kurushiana ya hapa na Pale baina ya Ma-young kadhaa wa hapa hapa Nchini tanzania ambao wote wanafanya muziki wa Hip Hop.

Ma-young hao ni pamoja na Young Killer-Msodoki, Young Dee-Paka Rasta, na Janjaro, ambao maneno yao yamekuwa yakizunguka huku na kule kwenye vyombo mbali mbali vya habari na hata kupitia Mitandao ya Kijamii

Hii yote ni kutokana na Rappers hawa kufananishwa ama kushindanishwa ili kufahamu nani ni mkali kuliko mwenzake, kitu ambacho kimekuwa kikitoa Majibu mbali mbali na madongo ya hapa na pale

Young Dee amekuwa akisema mara kwa mara pindi anapoulizwa, kuwa asifananishwe na watoto hao, huku Janjaro akionekana kurusha na yeye madongo yake, lakini hiyo bado ni jambo ambalo lipo tu.

Ingawa imekuwa ni utaratibu wa Waungwana wengi wa Kitanzania, kluwa Fulani akikwazana na mtu fulani, basi hata marafiki au watu wa Karibu kwao na wenyewe hupachikwa katika mgogoro huo, kitu ambacho imekuwa tofauti kwa Young Dee

Kupitia Instagram account yake, Young Dee aliamua kuanika hisia zake kwa MADEE ambaye ni Mlezi wa Janjaro (ambaye wanarushiana maneno) kitu ambacho kimeleta taswira nyingine tofauti.

Kupitia Instagram yake, Young Dee alisema kuwa anampenda sana Madee ambaye hivi karibuni pia kaachia Video yake inayoitwa SEMA.

Aliandika Hivi:
"Dingiliiii amekuletea jambo!!!!! @madeeali nakupenda sana Dingi! Ebu gusa link on his bio kuona video yake mpya #SEMA 💯🙌🏽"

Ujumbe huo umekuatana na Comments Nyingi ambzo zimeonekana kufurahia hali hiyo licha ya kuwepo kwa minong'ono kibao
 

MNADA BANNER