REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NEYO:Nimeshawahi Kuoa Nikiwa na Miaka 19

3:53:00 AM Add Comment
KABAAAAANG

Licha ya kujulikana kwa kufunguka na kuweka wazi mambo mengi ya kimapenzi katika nyimbo zake, nguli wa r&b Neyo ameweza kuficha siri yake kubwa kwa miaka mingi.


TMZ wameripoti kuwa Neyo amefunguka kuwa alishawahi kuoa akiwa na miaka 19, lakini ndoa yake haikudumu na ilivunjika kwa mda mchache baadae kwa kuwa alikuwa akipenda kuingia katika kazi ya muziki lakini mke wake alikua hataki kabisa na hakuwa akimpa sapoti.

"sasa hivi nipo hapa nilipo, na sijui yeye yuko wapi" alisema kwa utani.
kwa hivi sasa mshindi wa tuzo za Grammy, ameshaendelea na maisha yake ya kimapenzi na ana watoto wawili na girlfriend wake wa kitambo Monyetta Shaw

HOT HOT YA LEO; MARC ANTHONY NA MTOTO WA BILLIONEA

3:39:00 AM Add Comment

WAKATI mamito Jeniffer Lopez "J.Lo" akizidi kula Mahaba ya Kijana Mdogo ambaye Pia ni Danser wake, Marc Anthoni hi sasa anafaidi ladha za Kimahaba toka kwa Mwanadada CHLOE GREEN ambaye inasemekana kuwa anatokea katika Familia ya "Mpunga Balaa"

Kwa Taarifa yako na kama ulikuwa hujui, Mwanadada CHLOE ni Mtoto wa Billionea Nchini Uingereza, anyefahamika vema kwa Jina la SIR PHILIP GREEN. Hebu Cheki hii Picha ndo Utaniambia Huyu Mzee ni Noumar..


MPEKUZI : MWANAMKE ABAKWA BAADA YA KUWEKEWA MADAWA YA KULEVYA

3:19:00 AM Add Comment

HUYU ni  mrembo aliyekuwa amepata  mwaliko toka kwa jamaa mmoja ambaye  walijuana  katika  birthdaya  ya rafiki yake.....

Inadaiwa kuwa Binti huyu  anasifika  kwa  kuwachuna wanaume  wanaoingia  katika  anga  zake  na  kuwatelekeza.Bahati mbaya  msimu  huu haukuwa  wake  baada  ya  kuwekea  madawa  ya  kulevya  katika  kinywaji  chake na hatimaye kumnonihino......


Binti hakuweza  kuusoma  mchezo  maana tayari  pombe ilikuwa imeshaanza  upanda  kichwani....Baada  ya  muda, mrembo  alikuwa  hoi  bin  taabani  na  ndipo wavulana hao walipombeba na  kumbaka  na  kisha  kumwacha      

AFYA; TOHARA KWA WANAUME

3:12:00 AM Add Comment
                  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Husein Mwinyi

Na Beatrice Moses

SERIKALI imejiwekea lengo la kutahiri wanaume milioni 2.8 ifikapo mwaka 2015, baada ya kufanikiwa kuwatahiri 287,055 kati ya mwaka 2010 na 2012.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ikifafanua kuwa huduma ya tohara ya kitabibu kwa wanaume ilianzishwa mwaka 2010.

Imetekelezwa zaidi mikoa ambayo ilibainika kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

“Iligundulika kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU ambako kuna kiwango cha chini cha tohara kwa wanaume.  Mikoa hiyo ni ya  Iringa, Njombe, Simiyu, Geita, Katavi, Mbeya, Rukwa, Tabora, Kagera, Mwanza na Mara,”  inaelezwa taarifa hiyo.

Inaelezwa kuwa Serikali ilifanikiwa kuwafanyia tohara wanaume hao kwa kutumia njia ya kuwaelimisha kwa kuwaelezea umuhimu wa tohara na hatari inayowakabili kwa kuendelea kuishi bila kufanyiwa tohara hasa kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwamo VVU. 

Pia, taarifa hiyo inaeleza kuhusu mpango wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mwaka 2005, wajawazito 11,435 ambayo ni asilimia tisa ya wenye maambukizi ya virusi.

Inasema walipatiwa dawa za ARVs kuzuia maambukizi hayo kwenda kwa mtoto.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, wizara hiyo inaendelea kutoa kupaumbele maeneo ya kudhibiti magonjwa ya ngono, utoaji ushauri nasaha na huduma kwa wagonjwa wa nyumbani, elimu na habari, tiba na matunzo, huduma ya maabara kwa wagonjwa waishio na VVU.  

“Hamasa kwa Watanzania imekuwa ikiongezeka hasa baada ya kampeni iliyoongozwa na Rais (Jakaya Kikwete) mwaka 2007, idadi ya vituo vya upimaji iliongezeka kutoka vituo 521 mwaka 2005 hadi 2,200 mwaka jana,” inasema taarifa hiyo na kuongeza:

“Iidadi ya wananchi waliopatiwa huduma hiyo nayo imeongezeka kutoka watu 365,189 mwaka 2005 hadi watu 17,008,475 Machi mwaka jana

KENYA: NONINI AVUNJA RECORD KWA KUPATA MKWANJA MWINGI ZAIDI

3:08:00 AM Add Comment


KWA UFUPI
GOD FATHER WA GENGE wa kuitwa Nonini hatimaye amevunja Record ya kuwa Msanii anayelipwa fedha Nyingi zaidi Nchini Kenya

Taarifa hizo za kuvunja Rekodi hiyo zimetolewa Mapema Mwaka katika Ripoti ya MCSK (Music Copyright Society of Kenya) Nchini Kenya

 Wasanii wengine ambao wametambuliwa kupata Fedha Nyingi pia na MCSK ni Pamoja na Msanii JAGUAR, WYRE "The Love Child" na Marehemu ANGELA CHIBALONZA ambao walichukua nafasi za Pili Tau na Nne

BAVICHA: "TUTAKOMAA NA WAZIRI KAWAMBWA"

2:57:00 AM Add Comment


BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha),  limewatumia waraka viongozi wake wote wa mikoa na wilaya, unaowataka kujiandaa na maandamano ya kushinikiza viongozi wa juu katika  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, kujiuzulu.

Pamoja na kushinikiza viongozi hao kujiuzulu, Bavicha pia inaitaka Sserikali  kutangaza matokeo hayo ni janga la Kitaifa na kuiweka elimu kipaumbele cha kwanza katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/14.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya  mtihani wa kidato cha nne, uliofanyika kote nchini  mwaka jana.

Matokeo hayo  yalitangazwa na Waziri wa  Elimu na Mafunzo ya Ufundi,  Dk Kawambwa ambaye alisema zaidi asilimia 60.6 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo wamepata sifuri.
Waraka huo ambao Mwananchi ilifanikiwa kuupata jana ukiwa umesainiwa na Katibu Mkuu wa Bavicha,Deogratias Munishi, unawaagiza viongozi hao kufanya maandalizi  ya haraka ili kujiandaa na maandamano kama Dk Kawambwa hatajiuzulu wiki moja ijayo.


“Kwa waraka huu ndugu viongozi, mnaombwa kufanya yafuatayo; kuanza maandalizi ya maandamano haya ya kudai elimu bora kwa vijana wa Tanzania, na pia hatma ya waliofelishwa na Serikali ya CCM kwa kuwasiliana na hao waliofeli katika maeneo yenu ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha sahihi zao kama sehemu ya wao kuthibitisha kuitaka Serikali iwajibike” ilisema sehemu ya waraka huo.

Waraka huo pia umewataka viongozi hao kuwahamasisha wananchi kuunga mkono azimio hilo kwa kuwaelimisha vijana na wazazi wao kupitia  vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.

Akizungumzia waraka huo, Munishi alisema huo ni mwanzo wa utekelezaji wa azimio alilolitoa hivi karibuni la kuaanda maandamano.

MWANANCHI

KENYA: CAMP MULLA KUJA NA VIDEO YAO YA AMANI inayoitwa "IF YOU BELIEVE"

2:48:00 AM Add Comment
NA Frank M. Joachim "hasta La Vista Baby"
KUNDI linalotazamwa zaidi Barani Afrka kwa Kufanya vizuri katika Music Industry, CAMP MULLA toka Kenya, hivi sasa wapo katika harakati za Kuachia Video yao mpya ya Aamani itakayokwenda kwa Jina la "If you Believe"

Kundi hilo ambalo limekuwa likifanya vema katika Tasnia hiyo na kujiweka katika takwimu za Muonekano wa Kimataifa, wameamua kufanya Kichupa hicho ambacho BT imetafsiri kuwa kitu kikubwa zaidi licha ya Muonekano wa Video hiyo kuonekana Simple hasa katika Maandalizi yake.

 Tofauti na Yote, BT pia imebaini kuwa Lyrics (Mashairi) za Mkwaju huo zimekuwa ni moja kati ya Vitu Vikali vitakavyopifanya VIDEO hiyo kuwa Bora zaidi kama zile za FRESH ALL DAY, HOLD IT DOWN, PARTY DONT STOP na hata FEEL NO PAIN.

Hizi ni Picha za Utengenezaji wa Video Hiyo












MNADA BANNER