REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HAWA NDIO FISI WALIOKUTWA NA SHANGA PAMOJA NA ROZALI KIUNONI. MKOANI MWANZA

7:14:00 AM Add Comment

NA G-SENGO
MSAKO wa Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.

Maajabu hayo yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya 12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.

Msako huo wasiku tatu ulioanza juzi (Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa Kijiji hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe, wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao 50.

Habari za ndani kutoka Kijijini humo zimesema kwamba, kabla ya wananchi hao kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi wanadaiwa kumilikiwa na watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina, wazee wa Kijiji na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na nguvu za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.

Kwa mujibu wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho ambao hawakutaka majina yao yaandikwe, walisema kuwa makamanda wa jadi wanaoongoza msakao huo pamoja na mbwa wao, wana kinga za kupambana na imani za kishirikina vinginevyo wasingeweza kuua fisi wenye shanga na Rozali wanaotumiwa kishirikina.

Diwani wa Kata ya Hungumalwa Shija Malando akizungumza na waandishi katika Kijiji hicho jana, alisema wananchi walifikia maamzi ya kufanya msako huo wa siku tatu, baada ya kundi kubwa la Fisi hao wanaokadiliwa kuwa zaidi ya 80, kuwa tishio kwa watoto na mifugo.


Alisema kuwa, kwa muda wa miaka miwili iliyopita hadi sasa, licha ya wanyama hao kuharibu hekali moja ya matunda aina ya Tikiti Maji yaliyokuwa yamelimwa na mwanchi mmoja, wameua ng’ombe 109, Mbuzi 135, kondoo 127 na Nguruwe 15 katika Vitongoji hivyo.

“Njooni muone maajabu haya.” Alisema Malando na kufafanua “Jana (juzi Jumapili) wananchi walifanikiwa kuua fisi kumi wawili kati yao wakiwa na maajabu. Mmoja aliukuwa na Rozali kiunoni na mwingine akiwa na shanga kiunoni huku uume wake ukiwa umetahiriwa kama binaadam.”

Alisema fisi waliokutwa na vitu hivyo kiunoni, kwa imani za kabila la Kisukuma, wanadaiwa kumilikiwa na baadhi ya watu wenye imani za kishirikina na kwamba, waliuawa majira ya saa 8 hadi saa 10 mchana kwenye eneo la mlima wa Mwanzabalemi.

Alifafanua kuwa, fisi kumi waliuawa (jumapili) siku ya kwanza ya msako huo na wengine wawili waliuawa jana asubuhi na kwamba maeneo ya milima ya Mwanangi katika Kijiji cha Buyobo na Kitongoji cha Mwanzabalemi yanasadikiwa kuwa na fisi wengi zaidi.

“Pamoja na kushambulia mifugo wetu, ilifika mahali wananchi walikuwa hawawezi kutembea kwa uhuru nyakati za usiku na baadhi ya watoto wanaosoma mbali kukatisha masomo kwa kuhofia kuliwa na fisi hao.” Alieleza Mwenyekiti wa Kijiji cha Hungumalwa, Clement Kaswahili.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwang’ombe Joseph Kisena alisema hadi kufikia leo (siku ya tatu ya msako huo) watakuwa wameua fisi wengi zaidi kutokana na ushirikiano mzuri wa Vitongoji hivyo vinavyotumia mbwa 50 na siraha mbalimbali za jadi ikiwemo mikuki, mapanga na marungu.

Kisena alisema, pamoja na maajabu ya fisi kuvaa shanga na Rozali kiunoni ambayo wamejionea na kuzua imani za ushirikina kwa baadhi ya wananchi, hawatarudi nyuma, hadi walitokomeze kundi la wanyama hao ambalo ni tishio kwa wananchi na mifugo wao.



BAADA YA KUDAIWA KUMTELEKEZA MTOTO WAKE KATIKA GRADUATION YAKE, 50 CENTS AJIBU TUHUMA..

6:56:00 AM Add Comment

ATLANTA, Marekani
50 CENTS amejitokeza na Kudai kuwa hakumtelekeza mtoto wake siku ya graduation yake, kama ambavyo mwanae huyo alilalamika.

Marqiuse Jackson, hivi majuzi alikuwa anahitimu masomo yake ya Diploma huko nchini marekani, lakini jambo la kushtua ni kwamba, Marquise alipost Picha Huku akionekana Kulalamika baba yake 50 Cents kutokuhudhulia, huku akipata Kampani ya kutosha toka Kwa mama yake na dada yake.

50 Cents  anadaiwa kujiskia Vibaya baada ya kuona Picha ya Mtoto wake Huyo akiwa amemkumbatia mama yake huku akionekana Kulia, na amevalia Joho, na kuandika maneno makali kama yale.

Hata Hivyo, TTM imebaini kuwa, 50 Cents alidai kuwa hakuambiwa ni lini, na Ni wapi ambapo Mahafali ya Mwanae yalifanyika, tofauti na hilo angehudhulia.

FIDDY amekuwa katika kutokuelewana na mama wa Marquise, na Dio maana huenda hakupewa hata hiyo taarifa kuhusu Graduu ya Mtoto Wake huyo wa Kwanza, iliyofanyika katika Shule Moja huko Jijini ATLANTA

CHECK PICHA ZA MTOTO HUYU WA 50 CENTS




RAY JAY ATATOA ZAWADI KWA KIM KARDASHIAN. NI FAIDA ILIYOPATIKANA KATIKA MKANDA WAO WA NGONO

6:44:00 AM Add Comment

KUNA UWEZEKANO MKUBWA, Ray J akawa ana lake jambo baada ya Kuamua Kufanya kitu ambacho wengi tuklikuwa Tumeshaanza kukisahau

Ray J ameahidi kumpa Kim kardashian zawadi ya Faida aliyopata katika Mkanda wao wa Ngono uliovuja Miaka kadhaa iliyopita.

Ishu hiyo iliyoteka Vichwa kibao Vya habari Duniani, Inasemekana Kuwa, itafanyika katika Ndoa pamoja na Sherehe ya Kufunga Ndoa kwa kanye West na Kim kardashian, ambapo Ray J amesema atatoa Zaidi ya USD LAKI 40, ambazo amezipata ndani ya Miezi Minne
Pia ray J ameshusha Hesabu zake ambazo amezipata Kuanzia mwezi January ambazo Ni kama Ifuatavyo

-- January  $6,135.60
-- February $20,097.31
-- March $9,674.76
-- April $10,931.52

Aidha Kwa mujibu wa Mtandao wa VIVID ENTERTAINMENT, inasemekana kuwa Video Tape Hiyo ambayo ilifanyika 2007, imeuza mpaka Kupata Kiasi cha USD MILIONI 50

Hata hivyo Mitandao ya kidaku ilijitahidi kumtafuta Kim kardashian Ili kuzungumza kama atapokea zawadi Hiyo toka kwa ray J, lakini hakupatikana.


Pia Ray Jay amedai kuw3a, kama Kim hatopokea Zawadi hiyo, basi ataipeleka katika kituo cha Kulea watoto yatima ambacho Kim Kardashian anakipenda.

LUPITA NYONG'O NA EMINEM, USO KWA USO

6:32:00 AM Add Comment

Muigizaji aliyepata umaarufu zaidi kupitia filamu ya 12 Years a Slave amepewa nafasi nyingine ya kuigiza katika filamu nyingine kubwa itakayowahusisha watu maarufu akiwemo rapper Eminem.

Kwa mujibu wa Fashion Times, Lupita anatarajiwa kuigiza kwenye filamu ya ‘Southpaw’ kama mfanyakazi wa mcheza masumbwi ambaye alikuwa juu na akashuka ghafla ambaye anafanya juu chini kurudi kwenye rekodi yake ya awali.

Katika filamu hiyo itawahusisha watu wengine maarufu akiwemo rapper Eminem, Jake Gyllenhaal, Forest Whitaker, Rachel McAdams na wengine.  

Lupita pia amepata shavu la kuigiza kwenye flamu nyingine mbili ambazo zimetajwa kuwa ni ‘A Most Wanted Man’ na ‘Taken’

HUDDAH MONROE HUYU HAPAAAAAAAAA

6:28:00 AM Add Comment

Nani Asiyemfahamu HuddaH…nani ambaye hajamsikia Huddah Kwa muda mrefu?

Mitaa ya Kenya kuna habari zilizovujishwa na shushushu mmoja aliyeripoti kwa mtandao wa Ghafla akiambatanisha na picha kuwa mshiriki wa BBA ‘The Chase’ Huddah Monroe amefulia.

Kwa mujibu wa taarifa za mdaku huyo, mrembo huyo amefukuzwa kwenye nyumba ya kishua baada ya kushindwa kulipia kodi na hivyo amehamia maeneo ya Parklands na anaishi na mwanaume ambaye hafahamiki.

Picha hizo zinamuonesha Huddah akiwa amekumbatiwa na mwanaume huyo na nyingine wakiwa wamekaa na amemshika mabegani.

Hata hivyo sio kila ushahidi wa picha halisi ni wa kweli, mrembo huyo alipotafutwa alikanusha na kuzifanyia utani taarifa hizo na kudai kuwa yeye anaishi Kilimani na sio Parklands na kwamba mtu anaeonekana nae kwenye picha hiyo ni ndugu yake.


“He’s crazy! I live in Kilimani. That’s my cousin’s pal and that’s his house in Park Road.” Amesema Huddah Monroe.

MNADA BANNER