REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

USWAZI TAKE AWAY: SOKO LA BUGARIKA LILIVYONUSURIKA KUUNGUA

11:54:00 PM Add Comment

USIKU wa kuamkia Jumapili ya Leo, majira ya Saa 3:34 Usiku, Soko Tegemezi la Mtaa Wa Bugarika,Jijini Mwanza almanusura Liteketee kwa Moto Baada Duka Moja Kushika Moto na Kusababisha Maduka Mengine Mawili Kuanza Kushika Moto.

Mpaka Mwandishi wa BLACK TOUCHEZ anafika Eneo la Tukio, Moto Ulikuwa bado unapamba Moto huku Hofu kubwa ya Wakazi wa Mtaa Huo, ni Mashine ya Kusaga, ambayo Ilianza Kushika Moto katika Paa Lake.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Kwa Mashuhuda waliozungumza na BLACK TOUCHEZ, wanasema kuwa, Awali ulisikika Mlipuko Mkubwa Kutoka katika Duka Hilo, na Kusababisha PAA la Duka Kufumuka kwa Kasi ya Ajabu.

“Baada ya Kusikia Mlipuko huo wa Kwanza, Ghafla Tulisikia Mripuko Mwingine Tena, ambao ulifumua Paa Hilo Moja Kwa Moja na Moto Kufumuka kwa Kasi” alisema Shuhuda aliyejitambulisha kwa Jina la KULWA.
































Baada ya Jitihada za Dhati Kufanyika, hatimaye Gari la Zima Moto liliwasili Eneo la Tukio na Kufanikiwa kuokoa Robo tatu ya Mali za Wafanya Biashara ambao Wana maduka Katika Eneo Hilo.


































Mpaka Hivi sasa, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa ya Chanzo cha Kutokea kwa Moto Huo, Ingawa Baadhi ya Mashuhuda wanadai Kuwa, ni SHOTI YA UMEME iliyotkea katika Duka Hilo lililoteketea

HATA hivyo, Mpaka Hivi sasa, Taarifa Zinaeleza kuwa, Hakuna Mtu aliyepoteza Maisha katika Ajali Hiyo, ingawa kuna watu wawili (Mume na Mke)b ambao wamejeruhiwa, wakiwa katika Hatua za Kufunga Duka lao, ambalo lilipata Shoti ya Umeme
 


WEEKEND ROUND UP: KIJANA HUYU AMEKUTANA NA ADHABU HII BAADA YA KUJARIBU KUIBA FUNGUO ZA DALA DALA KATIKA GARAGE MOJA HUKO JIJINI MBEYA

2:43:00 AM Add Comment






 PICHA ZOTE NA MBEYA YETU

MNADA BANNER