REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BONGO MOVIES: KAJALA HUYU HAPA TENA

6:59:00 AM Add Comment

NA FRANK M. JOACHIM.
“HOT BABE” wa Bongo Muvi, Kajala Masanja, ameamua kuonesha mabavu yake kwa ukali na kwa mpigo, baada ya kutoa Guud Info kuwa kuna “Muvi “ Mpya ambayo hivi karibuni itaingia Sokoni.

Kajala ambaye Thisi time ameamua kusaka “Mpunga” kwa Nguvu zote, amepost kupitia account yake ya Instagram kuwa, anatarajia kushusha “Nyuu-Kitu” ambayo itakwenda kwa jina la PISHU.

Katika Cover ya Filamu hiyo, inaonekana kabisa kuwa, “Vichwa” vichache na Vikali vitakavyoonekana “Inside The Muvi” ni pamoja na HEMEDI “PII-HECHI-DII” pamoja na Mchekeshaji Maarufu Nchini, SENGA


TUNASUBIRI MAMA !!!

UNATAKA KUJUA ANAPENDA SANA TRACK GANI?..CHUKUA HII HAPA

6:52:00 AM Add Comment

NA FRANK M. JOACHIM
IN CASE weye Msanii haukubali sehemu ya kazi zako ambazo umeshawahi kufanya, basi “You are Wrong” sana kuhusu Rehema wa Chalamila, Iko Hivi……..

Kuna Mikwaju kibao sana ambayo Ray C aliweza kufyatua enzi hizoooooo..akiitwa “Kiuno Bila Mfupa” (Sasa hivi, mhhhhhhhhh), na aliweza kufanya “vere-guuud” kunako soko la Muziki wa kizazi kipya kabla akina Linah na akina Recho hawajaingia.

Moja kati ya “noma” ambazo alisumbua nazo sana, ni pamoja na SIKUHITAJI, UKO WAPI, MAHABA YA DHATI, NA WEWE MILELE, MAPENZI MATAMU, na Nyinginezo Nyiiingi sana

Sasa Kupitia Istagram account yake, Ray C ambaye this Time amejikita zaidi na harakati za kupiga Vita madawa ya Kulevya hasa kwa Vijana, amesema kuwa, Ngoma ambayo Anaikubali mpaka hivi sasa, ni NA WEWE MILELE.

Cheki alichokiandika hapa:




MSIMRUHUSU FLOYD MAYWEATHER KUINGIA KATIKA CLUB ZA WACHEZA UTUPU (STRIP CLUBS)

6:12:00 AM Add Comment

NA FRANK M. JOACHIM & TMZ
BAD LUCK kwa Club yoyote ambayo ni maalumu kwa ajili ya Wacheza Utupu Maarufu kama Strippers, itakayomruhusu Bondia Floyd Mayweather Jr kuingia Ndani..Zima tukupe Ful-Data

Idara ya Polisi Katka Jiji la Las Vegas kupitia METRO POLICE DEPARTMENT, wametoa taarifa kwa Club za aina hiyo ambazo zinapatikana “Area” hizo kutokumruhusu Mkali huyo wa Masumbwi, eti kwa sababu  huwa ni mdharirishaji hasa kwa akina dada ambao hucheza watupu.


Licha ya kuwa Floyd mwenyewe anasema “Hakuna kitu kama hiyo”, bado “Talantalila” zinamiminika kuwa, Floyd hupenda kutumia Jina na Maguvu yake kuwasumbua akina dada hao na hata kuwavunjia heshima, kitu ambnacho kinawaudhi hasa walengwa


Aidha kuna uongozi mmoja wa STRIP CLUB moja nchini Marekani umedai kuwa, Floyd aliwahi “Kutia Timu” katika Moja ya Club za aina Hiyo, lakini hakufanya chochote ati!

MAMA MZAZI REEVA YUKO TAYARI KUKUTANA USO KWA USO NA OSCAR PISTORIUS, BAADA YA KUMUUA MTOTO WAO

6:04:00 AM Add Comment

NA FRANK M. JOACHIM & DAILY MAIL
MAMA MZAZI wa Marehemu REEVA STEEN KAMP anayesadikika kuuawa na Mchumba wake OSCAR PISTORIUS, yuko tayari kuonana na Oscar.

Akizungumza na THE GUARDIAN, JUNE STEENKAMP, amesema kuwa, licha ya Kuwa “Mwanariadha-Mlemavu” huyo ameshaanza kutumikia Kifungo chake,bado anahitaji ifike siku ambayo haijulikani, akutane naye na kumuuliza kwa nini alimuua binti yao.


Siku ya Hukumu, Oscar alisimama kunako “Kizimba” na kuomba radhi hadharani kwa kile ambacho alikifanya dhidi ya bibie Reeva, ambaye alikuwa ni Mwanamitindo

June SteenKamp na Mumewe Barry SteenKamp, wameonekana kukubali kukutana na Oscar, na wanahitaji muda huo ufike, ingawa hawajui ni kipi ambacho Pistorious atakijibu hasa kuhusu Kifo cha Mtoto wao.

June ameongeza kuwa, hajui kabisa ni kipi Oscar atakachowaambia, kwa sababu hata Neno “SAMAHANI/NISAMEHE”  bado halitoshi.


Aidha Bado inaonekana kabisa kuwa Wazazi wa Reeva hawajaridhika hata kidogo na adhabu iliyotolewa juu ya Kifungo cha Oscar Pistorius

MNADA BANNER