REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ANKO ANAZIDI KUCHANUA TU....SAFI !!!

1:46:00 PM Add Comment



Huyu ni Anko Wetu, namzungumzia KINGSTONE, Mtoto wa Msanii wa Kizazi Kipya Nchini "Bongo" Tanzania, PIPI ambaye alimpata ndani ya Mwaka huu unaokimbia kama vile una matairi ya Tren,2012.
Hongera PIPI kwa kumtunza vema mpaka anakua Kiasi hiki....Mungu amlinde na ampe kipaji kama chako, au cha baba yake (kama ni kizuri lakini)

MINATO YA LEO :

7:38:00 AM Add Comment

Ahmad James Nandonde, Presenter Matata wa Victoria FM, hukooo...Musoma. Bro since namfahamu, huwa anapenda sana hiyo aina ya Kiatu, i mean Timber Land


Dyner Sembua, My Sister From another Mother. I admire her Talent esp[ecially akiwa Nyuma ya Mic, na akigusa Zile Fedal za Mixer...amaizin one. Mara ya Mwisho naachana nae, alikuwa anapenda sna kula Chips Mayai, thats why anaonekana Bonge Kidogo


Binafsi huwa namtania DORAH RODRICK "NARRATOR"... she is my Friend ambaye kwa sasa anaisaka Diploma yake ya Journalism pale Royal College of Tanzania. Dorah huwa anapenda sana "narration" (Usimuliaji) katika Vipindi vya Radio. Na anaweza hswa


 Hizi zote ni Mbwembwe tu...asikutishe wala nini...Goes by the Name Musa Omar, anakuja kuwashika Maprezenta wengine...Utamtaka


Ukimtizama sana, unaweza ukahisi yuko Deep anawaza life, But hapo ni Assignment za Chuo zimemchanganya kinoma noma..anasubiri Chips pale cafe..anaitwa TEDDY, Mwanafuzi wa Diploma in Journalism pale RCT

WEZI KWA NJIA YA MTANDAO NCHINI, HAWA HAPA

7:12:00 AM Add Comment


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

     TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 20/12/2012

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za wizi wa mtandao hususani katika maduka yanayotoa huduma za M-PESA,Tigo Pesa na Airtel Money katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma.
Watu hao ambao wanadaiwa kujipatia zaidi ya shilingi 1,730,000 /= kwa Mawakala wanne tofauti wanaotoa huduma hizo walikamatwa jana tarehe 19/12/2012 majira ya saa 12:00 hrs mchana.
Watuhumiwa hao ambao wanatokea Jijini Dar es Salaam majina yao ni Mohamed s/o Dotto @ Sefu, mwenye umri wa miaka (30) Mnyamwezi mkazi wa Kigogo, Mohamed s/o  Pazi, Mzaramo Miaka (28)  na  Ally s/o Mohamed miaka (25) ambao ni wakazi wa Ilala.

Wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kufanikisha wizi huo, moja ya mbinu ni kwenda kwenye maduka yanayotoa huduma hizo na  kumwambia wakala kuwa wanaharaka na kutaka kuweka Pesa kiasi fulani ambacho wanakuwa nazo mkononi na kuanza  kuzihesabu.
Mara meseji ya pesa toka kwa wakala zinapoingia katika simu zao, simu zao huita wakati huo huo na   kujifanya wanapokea simu huku wakisogea pembeni wakiongea na simu na kuondoka julma kwenda kuzitoa mahala pengine kwa haraka.

Wakala walioathirika na Wezi hao mpaka sasa ni Consolata d/o Martini ambaye duka lake liko eneo la Kuu Streetu shilingi 300,000/=, Perndo d/o Martin qambaye Duka lake liko eneo la CBE Tsh. 860,000/= Mlay s/o Felix eneo la Makole Tsh. 300,000/=, Masala s/o Mabula wa eneo la Changombe Tsh. 70,000/= na Duka la Lazia Shop ambalo liko Mtendeni Street Tshs 200,000/=.
Natoa wito kwa wamiliki na wakala wote wanatoa huduma hizo kuwa makini wanapoendesha shuguli zao, kwa kutoa taarifa za watu wanaowatilia shaka wanaofika kutaka huduma katika maduka yao mara moja ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.


[D. A. MISIME – ACP]
KAMANDA WA POLISI [M] DODOMA

CONTACT:     
 POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
 Phone:  0715 006523 – Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
 Phone:  0712 360203 – Silyvester Onesmo – Police  Konstebo           (PC)

HIVI NDIVYO DK BILALI ALIVYOWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA WATUMISHI

7:02:00 AM Add Comment






MNADA BANNER