REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NISHA: NILIFUKUZA MAWAZO YA MAFANIKIO, ILA SIO MAWAZO YA FURAHA

8:26:00 AM Add Comment

  Na Baba Juti  
TUMPONGEZE Sana Muigizaji wa Filamu za Tanzani (BONGO MOVIES) Nisha Bebe, ambaye kwa Nguvu aliztumia mpaka hapo alipo, amefanikiwa Kufungua Salon ambayo Mpaka hivi sasa inaonekana kufanya Vizuri

Kama utakuwa Umetembelea Instagram account Yake, utakuwa umeona namna ambavyo anafanya Kazi kwa kila watu wa kila aina ikiwemo kuwapamba Maharusi na Mengineyo

Katika Moja ya Post Zake, Ukiachilia Mbali ile ya Kukukaribisha Katika Salon Yake, Nisha ambaye pia hufanya Vizuri sana likija Suala zima la Comedy, amesema kuwa Nguvu zake na kutokukata tamaa, ndiko kumemfanya akafikika hapo alipo nab ado anamshukuru sana Mwenyezi Mungu

Kipindi cha Nyuma Kidogo, Nisha Bebe aliwahi kutengeneza Vichwa Mbali mbali vya Habari kwa Kudai kuwa Ex-Wake alimuingilia Kwa Nguvu Kimwili na kumpa Ujauzito, kitu ambacho kiliamsha Hisia za Watanzania Wengi hasa ambao wanamfuatilia bibie Huyu

Kitendo Chake cha Kulia mara kadhaa na kupost Instagram, kuliwafanya Wengi wamuonee Huruma na kuhisi kuwa Pengine Rapper Nay Wa Mitego ambaye aliwahi kuwa na Mahusiano ndiye muhusika wa Tukio Hilo, Ingawa kwa Upande wake alikana kabisa na kudai yeye hahusiki

Fina;lly, Nisha Hivi sasa ana Salon yake na anapamba Maharusi, kitu ambacho tunatakiwa kumpomngeza kwa kweli


NISHER : VIDEO YA YOUNG DEE NI KALI !!!!!

8:04:00 AM Add Comment
DIRECTOR NISHER (Photo: Nisher Instagram)

  Na Baba Juti  
INGAWA imekuwa ni Adim,u kidogo na sio kitu cha kawaida ama Utamadunni wa Directors wa Hapa Nchini Tanzania kukubali kazi za Wenzao, Wiki Hii limetoka Hili Jipya na tunaomba Tushare kwa Pamoja

Director ambaye anasifika kwa Kuachia Video Kali ambazo zina Ubora wa hali ya Juu, NISHER hatimaye amekubaliana na Watanzania walio Wengi kuwa Video ya BBM (BONGO BAHATI MBAYA ) ya Rapper YOUNG DEE a.k.a PAKA RASTA ni Kali sana na Director anastahili kupata Pongezi zake

Kupitia Instagram account Yake, Nisher alisema kuwa, Bila Unafiki wa aina yoyote, Director wa Video Hiyo MSAFIRI a.k.a TRAVELLAH kutoka KWETU STUDIO anastahili Pongezi, sababu Video Ni Kali

  Tunaomba Tunmnukuu  


A post shared by NISHER (@nisherx) on

#LoveKitaa : NI KWELI MABINTI WA MALIMBE WANARINGA KIASI HIKI?

6:59:00 AM Add Comment

  Hit Zone (JEMBE FM 93.7 MHz-Mwanza)  
KIPINDI Cha HIT ZONE kupitia Segment yake ya "LOVE KITAA" iliwatembelea Wakazi wa Mtaa wa MJENGONI ulioko katika Mazingira ya Malimbe karibu na Chuo Kikuu cha MT> Augustine (SAUT) na kupiga Story Nyingi sana hasa kuhusu Maisha na Vitu Pekee ambavyo hupatikana katika Mtaa Huo

Licha ya Kwamba yamezungumzwa Mengi na Wakazi wa Mtaa huo (Mjengoni), Love Kitaa ilikuja kubaini kuwa, asilimia kubwa ya Wasichana ambao kwa namna moja ama Nyingine ni wanafunzi wa Chuo Hicho, hulaumiwa kwa Kudaiwa kuwa "Wanaringa Sana" na kujiweka katika Hadhi Fulani, ha;li ambayo huwafanya wananchi wa Kawaida hasa wa Kiume, kushimndwa kujiweka Karibu nao

   WASIKILIZE HAPA KUPITIA LOVE KITAA YA HIT ZONE  

NEW VIDEO: AKA - CAIPHUS SONG

2:36:00 AM Add Comment

   Na Baba Juti  
#WatuWaMungu tunajua Mmemmis sana Rapper AKA kutokea SOUTH AFRICA...licha ya kuwepo kwa Majukumu ya Hapa na Pale, Migogoro ya Kimahusiano na Mengine, Finally ameshusha Video yake Hii Hapa

  ITIZAME   

MAMBO YA WALIMWENGU : NAS NA NICKI MINAJ NDIO COUPLE MPYA HAPA MJINI?

2:26:00 AM Add Comment

   Na Baba Juti  
#wATUwAmUNGU HII NI FUNUNU Mpya ambayo sijui tunatakiwa kuiamini, ama Hatutakiwi kuiamini kwa Hivi sasa

Kumekuwa na Minong’0m0 kwa Muda kadhaa kuwa Rapper Nas na Rapper Mwenzake wa Kike huenda wakawa “Wanatinduana” kitu ambacho mpaka sasa kimechukua Mishangao Mingi sana kutoka kwa Watu.

Kama utakuwa Umetembelea Instagram account Ya Nick Minaj mpaka hivi sasa, utakuwa umekutana na Post ambayo ilizidi kutufanya wengi tuanza kuhoji ni kitu gani ambacho kinafichwa Hapa
Hit Maker huyo wa PILLS & PORTION, alipost Picha yake akiwa amekamatiliwa Vizuri na Nas, kitu ambacho kiliashiria kuwa mahaba yanaweza kuwepo

   Katika Picha Hiyuo, Minaj aliandika kama Ifuatavyo  

“ WAFALME pekee ndio huwatambua MALKIA. Sweet Chick Life ina Chakula Bora zaidi. HONGERA NAS….”


Ingawa kuna Baadhi ya Watu ambao walijitahidi kuhiosi kuwa huenda hakuna kinachoendelea bali ni Kubust Mgahawa wa Nas, lakini kuna wengine bado wanahisi ni kweli kuwa NAS anamchapa Nicki Minaj

NGOJA KWANZA: DESIGNEER NDO KWISHA?...TIZAMA ALICHOKIFANYA HAPA !!!!

2:20:00 AM Add Comment

  Na Baba Juti  
KUNA hofu kubwa kwamba huenda Utamu na uzito wa Hit Maker wa Panda umefikia Mwisho kwa Hiki ambacho kinaendelea kutokea

Katika Jukwaa La HONDA ndani ya ACE THEATER, Desigheer alishindwa kuamsha Mizuka ya watu ambao walikuwa wamehudhuria katika Shughuli Hiyo maalum

Kwa Mujibu wa Video Clip ambayo Team Hit Zone tumeinyaka kama Kithibitisho, Designeer alijitahidi kuingia na Mzuka, lakini mambo yakawa Tofauti kabisa sababu watu walikuwa wamekaa na alikuwa ananyanyuka ambaye alikuwa anahisi ni bora ampe support tu.

Tofauti na Wasanii Wengine, endapo watapanda kwenye Stage basi Camera za Simu huupamba ukumbi Mzima, kwa Designer Simu zilitumiwa na Raia waliokuwepo kuchat na Ndugu zao tu, na si vinginevyo, ingawa kuna baadhi walishow Love kiasi kidogo sana

Designeer alijitahidi sana kuwaimbisha na kuwafanya japo wacheze na kunyanyua MIKONO JUU, hali haikuwa hivyo na watu walipigwa Doro kama Kawaida


Inasemekana kuwa hii ni Show ya Tano Designeer anafanya na kuambulia Pachungu

    TIZAMA ALICHOKIFANYA    

MURDER INC: INARUDI RASMI LAKINI SASA…..

2:17:00 AM Add Comment

Na Baba Juti: 
#WatuWaMungu tunaamini kabisa katika Records Labels ambazo zilisumbua Sana sana kipindi Cha Nyuma, kwenye Tano Bora, isngeacha Kuitaja MURDER INC ambayo ilikuwa na Wasanii wakali JA RU:LE pamoja na ASHANTI
.
Lakini Baada ya Kukaa Kimya kwa Muda Murefu huku wasanii wakifanya Shughuli zao Nyingine, hatimaye tamko Rasmi Limetolewa kuhusu Ujio Mpya wa MURDER INC

IRV GOTTI ambaye ndiye Mmiliki wa Record Label hiyo Kupitia Instagram aliandika Kuwa, MURDER INC Itazinduliwa Upya na Kuanza Kupiga Kazi upya kwa Nguvu zote, hivyo wadau wa Kazi zao wakae tayari kwa ujio huo ambao hautowafanya walaumu kilichofanyika

Lakini Ndugu zangu, kama Mlikuwa mnatarajia kusikia kuwa Ashanti na Ja Rule watakuwepo kuamsha kunako MURDER INC, kitulizeni kwanza , kwa sababu GOTTI anakuja na wasanii wengine kabisaa, ambao ni Wapya

Tunamnukuu: 

“ Niko Mbioni kuzindua Tena MURDER INC RECORDS. Nina wasanii wapya, na Muziki Mpya. Harakati ni Zile Zile, na Hii Ndiyo Record Labe yenye Kipaji Duniani kote. Kila Mtu alifurahia sana kipindi Cha Nyuma. Nilikuwa nikimsaidia kila mtu aliyenijia na kulia Shida zake. Nilikuwa nikipanga na kujikuta napoteza vitu vingi ilimradi kila mmoja apate chakula. Nilimpongeza kila mtu aliyestahili. Wala siku hata na Mfupa wa Chuki  ndani ya Mwili wangu. Napenda kuwaona Marafiki zangu wanashinda na kula vizuri. Lakini sasa hivi, ni zamu yangu sasa. Pesa yangu ni haki yangu”

MNADA BANNER