REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANZA IS GETTING HOT: ABOU MKALI- WATAELEWA

12:56:00 AM Add Comment

ABOU Ni Moja Kati Ya wasanii wanaofanya Vizuri katika Jiji la Mwanza.
Awali ameweza Kufanya Vema na Track Tofauti Ikiwemo BONGO MOVIE, TAMALA, na Nyinginezo.

Awali, ABOU (T.I.M) aliwahi kufanya kazi Pamoja na KUNDI la WAKUBWA WA JIJI, na kutoa Mikwaju kadhaa Ikiwemo MUDA NDIO HUU, HAPA HAPA, na FANYA ambazo still Ziko Hot.
Hivi sasa Ni SOLO ARTIST akiwa Chini ya BIG ENTERTAINMENT hapa hapa Jijini Mwanza.

Hii Ndo Video yake ya Kwanza akiwa kama SOLO ARTIST

RIHANNA HAJISIKII VIBAYA ENDAPO CHRIS BROWN ATAFUNGWA JELA…

12:38:00 AM Add Comment

YES!...Hatuna Budi kusema AHSANTE MUNGU kwa Yote yanayotokea Ingawa Inauma…

TTM tumebaini Kuwa FEBRUARY 20 Itakuwa Ni Siku ya Mkali wa POP na R&B Nchini Marekani, CHRIS BROWN, kupandishwa Kizimbani, na endapo mambo hayataenda Vizuri, basi ataishia Nyuma Ya Nondo, yaani Jela…

Lakini kwa Wakati Huo Huo, Tukabaini Kuwa, Siku Hiyo Hiyo ya FEBRUARY 20, itakuwa Ni BIRTH DAY ya Aliyekuwa Mpenzi wake, RIHANNA.

SASA, Chanzo Kimoja ambacho kipo karibu na Rihanna, kimedai Kuwa, Hit maker Huyo wa MAN DOWN amesema kuwa hatojisikia Vibaya Kusikia BREEZY amehukumiwa Kifungo Jela kutokana na makosa yanayomkabili, na wala Suaal Hilo halitomzuia yeye Kuenjoy BATA la BIRTHDAY PARTY Yake Siku Hiyo.

Muda wa BREEZY kutoka katika REHAB ambayo alikuwa akisaidiwa kuondoa tatizo la Kuwa na hasira kali, utamalizika Februrari 20, ambapo Moja kwa Moja atapanda Kizimbani Kujibu Mashitaka Kadhaa ambayo yanamkabili likiwemo la Kumpiga mmoja wa Shabiki zake ambaye alitokea katika Picha ambayo Breezy alikuwa anapiga na Mabinti Fulani ambao pia Ni Sehemu ya mashabiki Zake.

Tofauti na Kosa hilo, Brown ambaye Hivi sasa Albam yake ya X Iko Sokoni, pia atakabiliwa na Kesi ya Kumpa kifinyo Rihanna, pamoja na makosa Mengine Tofauti ambayo aliyafanya wakati bado ishu yake na Rihanna haijatolewa hukumu.

Pia Chanzo Hicho kiliongeza Kuwa, Rihanna atakuwa anatimiza Umri wa Miaka 26, na Kadri anavyokua, ndivyo anavyobadilika na Kuachana na mambo ya Awali.


HIVI SASA Stories zinazosambaa kwa kasi Mujini Ni pamoja RIHANNA Kubiringika na DRAKE ikiwa Ni mara ya Pili Tena baada ya Miaka Kadhaa iliyopita “Kuchoporoka” naye.

LIL KIM NI MAMA KIJACHO…

12:31:00 AM Add Comment

HABARI za Fasta ambazo zimefika Kunako dawati la TTM, ni Kwamba The QUEEN of Brooklyn, LIL KIM Ni Mjamzito.

Lil Kim Alionesha wazi kuwa ni “Mama Katumbo” katika maonesho ya BLONDS FASHION SHOW, iliyofanyika Usiku wa FEBRUARY 05 Mwaka Huu huko jijini New York.


Hakuna taarifa yoyote ama Neno lolote lililotolewa na KIM kuhusu Ujauzito, na hata baba wa Mtoto Huyo, lakini tambua Tu kwamba huyo atakuwa ni mtoto wake Wa Kwanza

BEYONCE AACHIA NGUO ZA NDANI SPECIAL KWA VALENTINE’S DAY

12:26:00 AM Add Comment

IKIWA imesalia Siku Moja tu kuweza Kuadhimisha Siku ya VALENTINE (VALENTINE’S DAY), Celebrities Wengi Duniani tumekuwa Tukiwaona wanaanda Special Songs kwa ajili ya mashabiki zao hasa Katika Siku hiyo Pendwa Duniani.

Lakini kwa Upande wa BEYONCE “Mama Blue Ivy”, imekuwa tofauti baada ya Kuachia Bidhaa zake Mpya, Nguo za Ndani, Special kwa Wote wanaompenda na wanaokubali Kazi zake.

Beyonce ameachia set kadhaa za Nguo Hizo za Ndani, ambazo zitakuwa Maalum kwa Jinsia ZoteMbili, Ya Kike na Ya Kiume., na Kishawishi Kikubwa cha yeye Kufanya hivyo, ni Track yake ya MINE

NGUO Hizo za Ndani, Zinapatikana kwa Gharama ya Dola 40 zaKimarekani, sawa na Takribani 60,000 za Kitanzania.


NICK MINAJI IS TOTALLY BACK…..KWENYE GAME

12:21:00 AM Add Comment

BAADA ya Kumsikia Kwenye KOLABLE Mbali mbali ikiwemo Tape Out Ya Rich Gang na Nyinginezo Kibao, Finally ONIKA TANYA MARAJ kwenye Stage “NICKI MINAJ”, amethibitisha Ujio Wake Mpya Kwa Mwaka 2014

Nicki Ambaye amejipanga balaa, na anarudi Tena Kuchafua Till You Get Down akiwa na Albam Mpya itakayoitwa THE PINK PRINT

Tofauti na Hilo, TTM tumebaini Kuwa, kuna Uwezekano Mkubwa wa Female Rapper Huyu Kuachia ALBAM na MIXTAPE  kwa wakati Mmoja ili Kupata Nice Fleva.

Ili Kuthibitisha makali hayo, NICKI hivi sasa ameachia Video Mpya Siku ya jana, ambayo inafahamika kwa Jina la LOOKING BACK NECCAH, ambapo TTM imetulazimu tuliweke Sawa Jina hilo Ambalo linautata Kidogo hasa Kwa Maadili ya Kitanzania na taaluma Yetu Kiujumla.

ALBAM ya THE PINK PRINT kutoka Kwa Nicki ni Moja kati ya Albam ambazo zinaweza Kutoka sambamba na Albam ya YMCMB FAMILY “RISE OF AN EMPIRE”

ISHU YA RIHANNA KUFULIA …IMESUKUMWA HADI MAHAKAMANI

12:14:00 AM Add Comment

UNAWEZA Kudhani tunakuchora, lakini ukweli halisi ndio Huo,

The Po p Female Singer, RIHANNA, amefunguamashtaka Dhidi Mhasibu Wake, kwa Kumpa Ushauri Mbaya ambao ulimpelekea Kufulia mwaka 2009.

Hali hiyo ambayo imeonekana Kuwashangaza Wengi, imefikiwa Na Mrembo huyo baada ya kubainika Kuwa ilifikia Muda akafulia kabisa na Hakuwa na Mkwanja jambo ambalo lilimpa wakati Mgumu kuweza Kusurvive Kimkwanja.

Katika Kufahamu ukweli juu ya Mtonyo Huo, TTM Iliamua Kuzama Ndani kabisa na kuchimbua maelezo zaidi, ambapo tul;ibaini kuwa, Ni Kweli RIRI ameamua Kufungua Mashitaka dhidi Mhasibu wake 

Huyo,ambaye alimpa Ushauri Mbovu wa Kiuchumi.
TTM Pia Imebaini kuwa, katika Moja ya Ushauri alioutoa Mhasibu huyo, Ni pamoja na Kununuliwa kwa jumba La kifahari lililomgharimu Dola za Kimarekani Milioni 7.5, kipindi hayuko katika Soko lake hasa Kimuziki, na hakuwa na uwezo wa Kugharamikia Kitu Hicho.

Mnamo Mwanzo wa Mwaka 2009, RIHANNA ambaye Jina Lake halisi ni ROBBIN FENTY, alikuwa na Dola Milioni 11 katika Account yake ya Bank, lakini alibakiwa na Dola Milioni 2 kufikia Mwisho wa Mwaka huo wa 2009, baada ya kutumia Vibaya Pesa zake katika Gharama zisizo na maana pamoja na TOURS ambazo hazikufanikiwa


Aidha ilimlazimu MKALI Huyo wa DIAMONDS, MAN DOWN na NEW HIT ya Hivi sasa, CANT  REMEMBER  TO FORGET YOU, kuuza Jumba Lake Hilo na kupata hasara ya Dola Milioni 2 katika Mchakato wa Uuzaji, jambo ambalo limemlazimu Kufungua Mashtaka Dhidi ya Mhasibu wake, kwa kumshauri vibaya katika matumizi ya Fedha

MNADA BANNER