REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAJANGA: BEYONCE AFUNGULIWA MASHTAKA

12:33:00 AM Add Comment

Unaweza Ukashtushwa na maamuzi ambayo Mashabiki hawa  wa Beyonce walichokifanya, lakini ukweli utabaki Pale pale…

TTM tumeinyaka kuwa  MASHABIKI wawili wa Beyonce wamechukua uamuzi wa kumfungulia Muimbaji wa kike nchini Marekani, BEYONCE “Mrs Carter”, baada ya Kujeruhiwa katika Show yake.
SASA Baada ya Kupata info Hizo, TTM tuliingia kazini na kuweza  kusaka chanzo cha hayo yote na hatimaye kupata Mtonyo kamili wa Ishu Nzima.

Kwa Mujibu wa maelezo  kutoka kwa wafungua Mashtaka hayo, RAQUE CASTELLANOS na GABRIELLA DAVIDSON, inasemekana kuwa walielekea kunako Eneo la United Center katika Jiji la Chicago Mwezi December Mwaka jana, kwa ajili ya kufuatilai Show ya Bibie huyo Beyonce, wakiwa na Tiketi zao mapema, na hatimaye kuwahi kabisa eneo ambalo lipo karibu na STAGE,ili waweze kushuhudia Vizuri kila kinachoendelea.

Wawili hao waliendelea Kusimulia Kuwa, wakati wako pale kunako STAGE mapema kabisa, Ghafla Milango ya Mbele Ilifunguliwa kwa Fujo na kasi ya Ajabu na kundi la watu ambao bila shaka walikuwa ni Mashabiki wa Beyonce Pia, huku likiwavamia wawili hao mahali walipokuwa.

Aidha Baada ya RAQUE na GABRIELLA kustaajabu kinachoendelea, Ghafla walijikuta wakisukumwa na kukanyagwa huku na kule, jambo ambalo liliwaletea majeraha makubwa na hasa Athari ya Kiafya, ikiwemo kupoteza Fahamu, na Kujeruhiwa Vibaya katika baadhi ya Viungo vya Mwili hasa maeneo ya Mifupa.

Katika Kuhitimisha, Wanawake hao wawili walidai kuwa, Sababu ya wao kumfungulia mashtaka Beyonce, Ni maandalizi Mabovu ya Sehemu ambayo Mkali huyo wa DRUNK IN LOVE alitakiwa kupiga Show, huku kukiwa hakuna Ulinzi wa kutosha na hasa mazingira ya kiusalama kwa Mashabiki wake.


Aidha baada ya Tukio hilo kuwakuta Warembo hao wawili, hatimaye walikimbizwa katika Hospitali iliyokuwa maeneo hayo kwa ajili ya matibabu, na wala hawakushuhudia Show ya Beyonce waliyoilipia mapema kabisaaa, kutokana na Mbwadidi hilo..

FAT JOE HAKUTEGEMEA KUFANYA COLLABE NA ALIYEKUWA HASIMU WAKE, 50 CENTS.

12:28:00 AM Add Comment

SONGERA ZIGI ZIGI Kwa Big Bway FAT JOE na 50 CENTS kumaliza Mbwadidi lao, na kuamua Kupiga Mzigo Pamoja, jambo ambalo liliwashtua Wengi.

KUPITIA moja Ya Interview Nchini marekan, Fat Joe ameelezea Hisia zake baada ya kukutanishwa na hasimu wake aliyekuwa akimchukia kupita Maelezo, 50 CENTS katoka Track iliyopewa Jina la FREE AGAIN, iliyokuwa Chini ya Miliki ya DJ KAY SLAY.

FAT JOE alimiminika kuwa, Kiukweli kabisa alishtuka kusikia kuwa Yupo katika Track Moja na Huyo hasimu wake, JACKSON CURTIS ambaye sasa Hivi anashughulikia Project yake Mpya ya ANIMAL AMBITION, maana ni kitu ambacho hakuwahi Kukifikilia hata Kiduchu.

Tofauti na Kushtushwa kwake, Fat aliongeza kuwa, anaamini pia hata mashabiki wake na wale wa 50 Cents hawakutarajia kama kitu hicho kingetokea, kutokana na Jinsi walivyokuwa katika BIG BEEF ambalo kila mtu alitarajia huenda Jamaa hawa wangekutana Sehemu na kutibuana Kidogo tu, basi Risasi ama Visu ama Ngumi Zingejazwa Kwenye Mwili wa Mmoja kati yao.


Pia Fat Joe Ameongeza kuwa, kitendo cha Yeye na 50 Cents Kupatana na hata kushiriki katika Track Moja, basi inadhihirisha Kuwa Umoja zaidi katika Muziki wa Hip Hop, na Kuna mambo Mengi mazuri ambayo Mahasimu wasioivana wanaweza kuyafanya Kama kilichotokea Kwake na 50 Cents

BEYONCE HATOHUDHURIA NDOA YA KELLY ROWLAND

12:25:00 AM Add Comment

Infact Ni wengi ambao Tunaamini kabisa kwamba Beyonce na Ndugu yake KELLY Rowland ambao wote kwa Pamoja ni Ex Members wa Ex Crew ya DESTINY’S CHILD, hawana maelewano Mazuri Kiasi hicho ingawa Wanapiga Story za hapa na Pale.

Kitengo Cha Chimbua Chimbu kimrpata mtonyo kuwa kuna Uwezekano mkubwa wa Beyonce kutokuhudhuria Ndoa ya Kelly, kutoakana na Mpangilio wa Tukio Zima.

Akitolea maelezo Suala hilo ambalo kuna Baadhi walitarajia kukutana nalo huku wengine wakiamni huenda Ndugu hao watakuwa pamoja, Kelly Rowland amesema kuwa, maamuzi aliyoyafanya, hayatahusisha Sababu za Kutokuelewana na Beyonce, infact Hayo yote ameshayasahau, na hayatilii maanani.

Kelly ambaye hivi Karibuni atafunga Ndoa na Mchumba wake TIM WITHERSPOON amedai kuwa wanahitaji Ndoa ambayo itakuwa ya Amani, katika Siku yenye Amani kabisa.

Hivyo Ndoa Hiyo itashuhudiwa ama itahudhuriwa na watu wachache sana ambao ni Mama Wa Pande Zte Mbili. Hivyo hawana mpango wa kuongeza Idadi nyingine ya watu, kwani Suala la Ndoa ni la wawili Binafsi.

Tofauti na hayo, Kelly aliongeza kuwa , Ndoa ni zawadi kutoka Kwa Mwenyezi mungu, na walengwa huwa ni wawili tu, ambao wanakubaliana kuishi pamoja katika Shida na Raha, hivyo Yeye na Mumewe Mtarajiwa wanahitaji kutengeneza historia ambayo Itabaki katika maisha yao Binafsi pamoja na wazazi wao.

Alipoulizwa kuhusu BLUE IVY kurusha yale maua wakati wawili hao wanapiga Agano lao, Kelly alicheka, na Kusema kuwa, hilo swali hawezi kulijibu Muda Huu…


Uhusiano wa Members wote watatu waliokuwa wakiunda kundi la DESTINY’S CHILD, yaani BEYONCE, KELLY ROWLAND na MICHELLE, ilivurugika, baada ya Beyonce Kujiondoa katika kundi hilo, na kuanza kufanya kazi zake Binafsi Chini ya Mumewe JAY Z, kipindi hicho akiwa Ni Mchumba wake

SABABU ZA DULLY SYKES KUAHIRISHA KUACHIA TRACK ALIYOMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ, HII HAPA..

12:20:00 AM Add Comment

TTM tulisikia Juu kwa juu kuwa DULLY SYKES ameahirisha Kuachia Track ya CHIPOLOPOLO ambayo amemshirikisha rafiki yake Diamond Platnum, badala yake ataachia Ngoma nyingine inayofahamika kwa jina la TOGOLA Mwezi huu.

Sababu ya Msingi ambayo Prince Dully Sykes ameitaja, ni kubadilika Kwa soko la Muziki hapa nchini Tanzania. Hapa Tunamnukuu

 “Kutokana na muziki kubadilika, unajua mimi nafanya muziki kutokana na jinsi unavyobadilika. Jinsi muziki unavyobadilika imebidi nifanye hivyo. Ni uchaguzi tu wa nyimbo kwa sababu nina nyimbo nyingi kwa hiyo sioni sababu za kung’ang’ania wimbo mmoja wakati nina nyimbo nyingi.”


Hata hivyo, mkali huyo amesema Chipolopolo ipo na anaeitaka atampatia na kwamba tayari wimbo huo upo kwenye miito ya simu. Ameongeza kuwa wataufanyia video baadae lakini sio kwamba utakuwa umetoka officially.


Akiongelea kuhusu maana ya Togola, Dully amesema hata yeye hafahamu maana yake na ni neno limekuja tu kama ilivyokuwa ‘Shikide’ lakini ameambiwa kuwa Tanga neno Togola ni salamu.

MNADA BANNER