REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KELLY ROWLAND : NILIKUWA NIKIPATA WAKATI MGUMU KUFANYA TENDO LA NDOA BAADA YA KUJIFUNGUA

2:18:00 AM Add Comment

  Na Baba Juti  
#WatuWaMungu hasa kwa Jinsia ya Kike, sijui kama mmeshawahi kukutana na hali hii, hasa kwa wale ambao tayari wameshajifungua na wanaishi na Waume zao

Kelly Rowland, Ex-Member wa Kundi La Destiny’s Child na Bibie aliyeafanya Poa kwenye Chorus ya DILLEMA ya Bwana Mkubwa Nelly, ameamua kushea na sisi hili jambo ili tujue

Mama huyu anadai kuwa, ilikuwa ni Ngumu sana kwa Upande wake kuvumilia kutokufanya Tendo la Ndoa Mpaka Njia yake ya Uzazi-yaani Uke Wake ukae Sawa

Kelly Rowland anadai kuwa, kuna Muda alikuwa anapata hamu kubwa sana ya Kufanya Tendo la Ndoa na Mume wake, lakini bwana mkubwa alikuwa anakataa kata kata mpaka mzigo upone ndo akunjuke Fresh


Tofauti na hilo, Kelly alikuwa anafikia Muda anajiona kuwa sasa Mvuto umesepa baada ya kujifungua na Mume wake hamtamani tena, lakini alikuwa akipokea Jibu la faraja kutoka kwa Mjoba Huyo kuwa “Bado ni Munono” tu, yaani yuko Sexy

VITA KALI: JAY Z NA KAMPUNI YA PERFUME KATIKA BALAA ZITO

2:13:00 AM Add Comment

  Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Nchini Tanzania hivi sasa tunafurahia Tu Perfume za Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya a.k.a Bongo Flava, Diamond Platnumz, lakini Nchini Marekani, kunako Perfume ambazo zina jina na Picha ya Jay Z, imekuwa Ni Ngumu Kumeza

Rapper Jay Z bado yupo katika Mgogoro Mkubwa  na mfanya Biashara ambaye alikuwa ni Partner wake katika Mchongo wa Manukato

Mwaka 2016, Mmiliki wa PARLUX FRAGRANCES, alimburuza mahakamani Rapper Jay Z kwa Madai kuwa, amesitisha Ghafla Mkataba wao wa Kibiashara kinyume cha Makubaliano yao, pamoja na kuwafanya waingie hasara ya Pesa Ndefu sana, kitu ambacho Jay Z amekipinga kwa asilimia 100

KESI YENYEWE
Bwana PARLUX anadai kuwa Mwaka 2012, waliingia katika Deal na kusaini Mkataba wa kutumia Jina lake na Picha yake katika Manukato yao waliyoapa jina la GOLD JAY Z na katika Uzinduzi wao

Katika Deal Hilo, Jay Z alitakiwa kupost Picha na Brand yao kwenye Mitandao ya Kijamii, pamoja na kufanya Promotions za kuwepo katika Kila Launching watakayoifanya , ili kuboost mauzo ya Bidhaa yao

Mlalamikaji aliendelea kumimina hoja zake kuwa, baada ya Muda kadhaa kupita, walimsaka Jay Z aweze kutokea katika Bidhaa zao Nyingine, bwana mkubwa alibana kabisa na wala hakutokea hata kidogo.

Tofauti na Hao, Mlalamikaji anadai walijitahidi pia kumualika katika Shughuli mbali mbali kama Vile Mikutano, Makongamano, Lakini hakutokea hata kidogo, na hakuwa akipost ama kufanya Promotions kama alivyotakiwa, kitu ambacho kimewafanya kuingia katika hasara kubwa, maana walitarajia kupata mauzo ya mpaka kufikia USD Milioni 50 ndani ya Miaka miwili

Hivyo wanataka Jay Z awalipe kiasi cha USD Milioni 18

  UPANDE WA JAY Z   
KATIKA kujitetea, Jay Z anadai kuwa , Partner wake ndiye aliyevuruga na kwenda Kinyume na Mkatabaama Makubaliano yao

Jay Z aliongeza kuwa, Kampuni hiyo ilishindwa kumpatia Pesa za mahitaji ambayo yalihitajika katika Promotions pamoja na kuipigania Bidhaa ambayo alitakiwa kuisimamia. Pia aliongeza kuwa, Walitakiwa kumpatia  USD 750,000 katika Mwaka wa kwanza, na ndani ya Miaka 5, alitakiwa kupewa USD Milioni 1.75 lakini ilikuwa kinyume

Katika kukazia Zaidi, Rapper huyo ambaye ni Mume wa Beyonce, alisema kuwa, Kampuni ilishindwa kumpatia USD Milioni 5 ili kutangaza Uzinduzi wa Manukato hayo katika Mwaka wa Kwanza. Na Ndani ya Mwaka wa Pili, Walishindwa kumpatia USD Milioni 6 kwa ajili ya Promotion

Lakini kitua mabcho jay Z anamaind ni kwamba licha kuharibika kwa Makubaliano hayo, Kampuni bado inatumia Jinan a Picha yake kujipatia Mafaida Kibao, kitu ambacho hata yeye hakubaliani nacho

MNADA BANNER